Serikali yaagiza majeshi kununua viatu kutoka kiwanda cha Kilimanjaro Leather Industry

Baba Mtakatifu

JF-Expert Member
Dec 31, 2017
1,324
2,435
Waziri wa wizara ya mambo ya ndani Mheshimiwa Masauni ametembelea kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd ( KLICL) kilichopo mjini moshi na kuagiza majeshi yote yaliyo chini ya wizara kununua viatu kutoka kiwanda hicho kwa kuwa vina ubora wa hali ya juu.

Masauni ametoa maagizo hayo tarehe 2 julai 2022 baada ya kutembelea kiwanda hicho na kufanya kikao na viongozi wa kiwanda, Pia amejionea uzalishaji unavyofanyika katika kiwanda hicho cha bidhaa za ngozi,

Ameagiza kuanzia sasa majeshi yote yaliyo ndani ya wizara yake kununua viatu vinavyozalishwa hapo kwa kuwa vina ubora.

Sorce: Wizara ya mambo ya ndani
 
Wazo zuri ila asijekuwa tayari ana 10% yake hapo, ingependeza zaidi Waziri ahimize wajitokeze wawekezaji wengine wazalishe viatu kwa ubora ili nao wapate soko, maana majeshi yote kununua viatu toka kiwanda kimoja naona kama mahitaji hayatatosha.
 
Ni kiwanda cha serikali au binafsi?
Hata hivyo,kweli magereza wameshindwa kutengeneza viatu vyenye ubora,pesa ikabaki serikalini kweli?
 
Siyo tu kuwa mahitaji hayatatosha ila hila la nchi kuendeshwa kwa matamko ya watawala ni ukale unazidi kutudidimiza chini.Hili ni suala linatakiwa liangaliwa kwa upana na urefu na ikiwezekane waanze na polisi na pia wahakikishe mambo yote muhimu yamefanyiwa utafiti na kuzingatiwa, isije kuwa prons do not outweigh cons.
 
Waziri apongezwe, haina maana majeshi kuagiza viatu kutoka nje wakati serikali ina kiwanda na kinazalisha viati vyenye ubora ule ule
 
Waziri wa wizara ya mambo ya ndani Mheshimiwa Masauni ametembelea kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd ( KLICL) kilichopo mjini moshi na kuagiza majeshi yote yaliyo chini ya wizara kununua viatu kutoka kiwanda hicho kwa kuwa vina ubora wa hali ya juu.

Masauni ametoa maagizo hayo tarehe 2 julai 2022 baada ya kutembelea kiwanda hicho na kufanya kikao na viongozi wa kiwanda, Pia amejionea uzalishaji unavyofanyika katika kiwanda hicho cha bidhaa za ngozi,

Ameagiza kuanzia sasa majeshi yote yaliyo ndani ya wizara yake kununua viatu vinavyozalishwa hapo kwa kuwa vina ubora.

Sorce: Wizara ya mambo ya ndani
Majeshi yetu yana weledi Bila shaka they won't act on politics..Kama hivyo vifaa vina ubora unaotakikana is okay ila kama ni kinyume chake don't do that.
 
Ni kiwanda cha serikali au binafsi?
Hata hivyo,kweli magereza wameshindwa kutengeneza viatu vyenye ubora,pesa ikabaki serikalini kweli?
Ni ubia kati ya PPF (now PSSSF) na magereza. It is a leather complex comprising a tannery, footwear, leather goods and sole manufacture factories.
Cha viatu kina uwezo wa kutengeneza pea 4000 per day. Ni kipya na cha kisasa kilianza kuzalisha two years ago...
 
Kiwanda hiki ni cha Serikali na kipo chini ya Magereza. Mashine zake zilizofungwa zimenunuliwa Italy na lilikuwa Lengo la Late Maghufuli R.I.P kuwa majeshi yote yanunue viatu hapo. Lakini baada ya kufariki ,Wadau wamepindua meza safi sana Waziri kuhakikisha hili linafanyika.Maana kweli wanamitambo ya kuzalisha viatu vya aina zote vinavyovaliwa na Majeshi yetu yote 100% wanavyo
 
Majeshi yetu yana weledi Bila shaka they won't act on politics..Kama hivyo vifaa vina ubora unaotakikana is okay ila kama ni kinyume chake don't do that.
Mwaka juzi wamefunga mitambo ya kuzalishia viatu toka Italy! Ni kiwanda ambacho kinaweza zalisha viatu vya hali ya juu ata vikauzika kwenye soko la USA na EU. Ila kwa kuwa tu nchi ya Watu wa Madeal Serikali isipokuwa makini Kitakufa kwa kukosa soko.Hii nchi ni ya ajabu sana. Zanzibar wana kiwanda cha Sukari lakini Wahusika wanaagiza sukari Brazil .Tuna Viwanda vipya vya Sukari 2 ,huku bara figusi zilizopo mpaka muda huu, avijaanza uzalishaji Watu wanendelea piga mahela kwa kuagiza Sukari nje
 
Matunda ya JPM ,Kiwanda kipo poa sana na viatu ni vizuri sana.kiungwe mkono.
JPEG_20220702_154218_3335914807310648083.jpg
 
Viatu vyao ni vizuri ila sijui kama Jeshi hilo litanunua,viatu staff shoes vya hao magereza ni 60000 na vigumu kwa kweli sasa hao walinzi wetu wanapenda mteremko viatu vyao vya bei nafuu soli za yeboyebo wakinunua mniite mbwa.
 
swala la kununua sio la askari binafsi hiyo ni sare.

nashangaa ndugu waziri anatoa tamko badala ya kutoa maandishi kwamba sare ya viatu inayonunuliwa na askari wa wizara ya mambo ya ndani itokee hapo.

saaa kwakuwa wamejiandaa kununua viatu china vya elfu tatu tatu,anajua kabisa hilo inabidi awaachie askari wenyewe kuamua.
 
... huu sasa ndio uwekezaji. Serikali idhibiti uagizaji wa viatu toka nje by angalau 40% ili kutoa upendeleo wa makusudi kwa kiwanda hicho. Ila nao wasibweteke na monopolism; waongeze ubora na kushusha bei. Ni aibu yale matakataka yanayouzwa kule Kariakoo kuitwa viatu sijui yanatokaga nchi gani - "ngozi" ya ajabu kabisa.

Yaani bora kununua mtumba toka EU, US, UK, etc. kwa bei mara 10 ya matakataka ya Kariakoo. Kiwanda cha Moshi focus yao inatakiwa iwe quaity ya Ulaya na Marekani na sio products za ngozi tunazoona Kariakoo. Wakongo, wamalawi, wazambia, n.k. wa-opt products zao ikiwezekana wafungue branches Dar na Mbeya kulenga masoko ya kimataifa.
 
Umenena point mkuu
 
Umenena point mkuu
... Mkuu; for years nimekuwa nikiumia sana kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye mifugo wengi Afrika - ya pili au tatu nadhani - yet hatuoni manufaa ya kuwa na hao mifugo! One would expect Tanzania to be among the producers of the best leather products!

Badala yake tunaagiza mavitu ya ajabu kwa ajili ya matumizi ya ndani wakati tulitakiwa even ku-export! Kwa hili la kiwanda cha viatu/ngozi kongole nyingi kwa waliolianzisha! La muhimu mradi uwe sustainable ikiwezekana hata ku-hire experts toka nje. Dubai wanafanya hivyo na wako mbali sana.
 
Ni ubia kati ya PPF (now PSSSF) na magereza. It is a leather complex comprising a tannery, footwear, leather goods and sole manufacture factories.
Cha viatu kina uwezo wa kutengeneza pea 4000 per day. Ni kipya na cha kisasa kilianza kuzalisha two years ago...
Kama viatu ni vizuri vitanunuliwa siyo na majeshi tu bali hata raia. Suala ni kuviweka sokoni halafu wavaaji waamue.

Ukiona viatu vinapigiwa chapuo na Waziri mwenyewe ujuwe vina mushkeli. Waswahili walisema "kiizuri chajiuza na kibaya chajitembeza"
 
... Serikali idhibiti uagizaji wa viatu toka nje by angalau 40% ili kutoa upendeleo wa makusudi kwa kiwanda hicho. Ila nao
Hili ni wazo la KIPUMBAVU halitegemewi kutolewa kwenye karne ya 21. Hii siyo North Korea. Yaani unataka turudi kwenye uchumi wa kuvaa viatu sare kutoka Bora shoe na kumiliki redio sare kutoka RTC?

Kama hicho kiwanda hakiwezi ku survive competition basi peleka kwa wauza chuma chakavu
 
Back
Top Bottom