Elections 2010 Serikali ya umoja zanzibar kudhoofisha uwajibikaji

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
SERIKALI YA UMOJA ZANZIBAR KUDHOOFISHA UWAJIBIKAJI

Hivi CUF na CCM watakapokaa mezani na kuongoza serikali ya Zanzibar ni nani atakagua utendaji serikalini kama kweli unamhudumia raia mlengwa?

Wanasiasa wanaharakisha kugawana madaraka bila ya kwanza kutafakari mfumo huu wa serikali kwa namna ipi usije kudhoofisha siasa za ushindani bungeni…..

Kenya tumeyaona lakini hakuna tulichojifunza……….Hii kweli ni bongo……..
 
Hapa sikubaliani na wewe rafiki yangu. Kenya kuna mabadiliko. Siyo kama siku zile za Moi au hata za Kibaki kabla ya serikali ya umoja. Siku hizi Kenya kuna malumbano ya kimtizamo mengi ingawa mengi yanakuwa nje ya Bunge. Na wananchi mara nyingi wanajitokeza kuunga mkono mtizamo mmojawapo. Kwa mfano kura ya maoni kuhusu Katiba mpya juzi juzi. Kibaki hana uwezo tena wa kuburuza serikali/bunge kama huko nyuma. Na sasa wana Katiba mpya wako makini kuhakikisha kuwa mambo yanafanyika Kikatiba. It is not perfect but a good beginning. Hivi ni lipi jema kwa Zanzibar? Hali iliyokuwepo au kuanza kujaribu mfumo mpya?
 
Back
Top Bottom