Serikali ya Tanzania na Kitu Chenye Ncha Kali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Tanzania na Kitu Chenye Ncha Kali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Sep 19, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wakati wenzetu wa Kenya wanaimba nchi ya kitu kidogo.....Sisi wimbo wetu ni nchi yenye kitu chenye ncha kali. Sihitaji kusimulia mambo yote ya watu kuuwawa na kuonekana wamechinjwa au kuuwawa na kitu chenye ncha kali lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Nikikumbuka Igunga, Arusha, Morogoro, Iringa, Iramba watu wote inaonekana waliuliwa na kuumizwa na vitu vyenye ncha kali kwa maana hakuna aliwajibika.

  Ni vyema watanzania wenzangu wakaelewa kuwa chini ya serikali ya ccm kuna vitu vyenye ncha kali ( sharp objects) vinavyoua watanzania hasa pale panapokuwa na jitihada za chama cha upinzani kuwafumbua macho wananchi. Pale ccm wanapofanya mikutano yao vitu hivyo huwa butu.

  Kinachoniudhi au kilichoniudhi ni pale yanapotolewa maamuzi au hukumu zenye ncha kali kwa baadhi ya wanasiasa. Hivi juzi imetolewa hukumu ya kifungo cha miaka 5 kwa mwenyekiti wa CHADEMA Minkoto chato na wenzake wawili. Wananchi wanaelewa kuwa kesi hiyo ni ya kubambikizwa hasa baada ya Mshitaki kushinikizwa ashitaki ili Mwnyekiti huyo adhoofike........kwa maana kuna fununu za kuifanya Minkoto kuwa kata.....kwa maana hiyo Mwenyekiti huyo angekuwa diwani kutokana na kukubalika kwake.

  Hivyo njia mojawapo ya kudhoofisha CDM mahali hapo ni kutoa hukumu yenye ncha kali. Aliyeshitaki anajulikana mahali mbalimbali kwa kuhifadhi ng'ombe wa wizi. Kabla hajaamia minkoto aliwahi kuchomewa nyumba na ng'ombe 80 kuuliwa katika eneo moja liitwalo KATENDE lakini hakuwahi kushtaki.......ila kwa vile watu wamemfanyia mambo hayo ambapo kiongozi nio wa CDM basi ikaonekana ndo njia ya kumkamatia kwa kuwa mifugo ya huyo bwana iliuliwa na vitu vyenye ncha kali....hasa hasa mapanga!!

  Reaction ya Wananchi

  Kwa kitendo hicho mimi nimeshuhudia barua kutoka kwa wakili ikimuomba hakimu atoe nakala ya hukumu kwa hiyo tayari rufaa imeanza kukatwa. Ili rufaa hiyo ifanikiwe wananchi wameanza kuchanga michango ya hiari ili rufaa ifanikiwe......... wadau tunachangishana na wananchi kule maeneo ya minkoto wenye mapenzi mema na kiongozi wao wanachanga ilin kufanikisha rufaa hiyo.

  Hali kama hii inanipa moyo maana sijaona siku za hivi karibuni wananchi kuhamasika na kujitahidi kumtoa Kiongozi wao kwenye mikono ya WATU WENYE VITU VYENYE NCHA KALI.

  Nina imani tutashinda................pia aliyeshawishiwa kushitaki aliposikia kesi inaelekea mbele mahakama kuu....anampango wa kutokomea. Asikimbie akae tu.

  CCM stop using Sharp Objects to harm your Tanzanians
  [​IMG]
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  ilianza liwalo na liwe........sasa ni kitu chenye ncha kali
   
 3. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kitu kizito/flying object morogoro,iringa kitu chenye mlipuko kama vile hawajui walikwenda na mabomu,,chama cha vingwangala bhana (chai na vitumbua)
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hata ulimboka alipigwa na kitu chenye ncha kali
   
 5. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndiyo umeanza, mie napita tu subiri wanakuja.
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Usiogope kijana iko siku vitu vyenye ncha kali vitakuwa butu.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Nchi inajiendesha yenyewe isipokuwa kufungua warsha,semina,madaraja,barabara ndio wanaweza mkisumbua na upepo wenu mnapewa mipasho kupitia wazee wa Dar!
   
 8. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kitu chenye ncha kali...........my a,s
   
Loading...