Serikali ya Tanzania haijitoshelezi kwa chochote kile hata baada ya 50 yrs!!

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Wadau Great Thinkers................

Mara nyingi tumekuwa tumekuwa tukijiuliza na kuleta takwimu Mbalimbali kuhusu nchi yetu kudorora katika karibia nyanja zote za maendeleo. Mpaka leo hii naandika hii makala na kwa mustakabali wa Taifa letu pasipo kujali tofauti za vyama vyetu.............tujiulize kitu kimoja kuwa ni wapi....serikali yetu...katika kuwahudumia watu wake ni wapi inajitosheleza walau kwa asilimia 50%? Nina magazeti hapa nyumbani ya muda mrefu karibia nitatengeneza godoro la gazeti........maudhui yote yanaonesha wananchi watanzania wakilaumu ukosefu wa huduma bora, Taarifa za habari zote zinazosomwa asilimia karibia 85% ni malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa huduma na uonevu, Sasa niulize wapi kati ya haya maeneo hapo chini nchi yetu inajitosheleza walau kwa asilimia 50% baada ya miaka 51 ya Uhuru.....

1. Kilimo : Tuna mtaji kiasi gani katika kuhakikisha kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa nchi hii kinafanikiwa? Basi tuseme kila kata kuna bwana shamba/mifugo...............ndugu zangu vijijini wanafuga kuku karibia 50 lakini wote wanakuja kufa kwa minyoo........elimu ya kumchanja kuku hamna.........Tanzania.!!!!!! Mbole za ruzuku hakuna, zikipatikana zinapatikana zimechelewa........naishia hapo,... tunajitosheleza kwa namna gani?

2. Elimu : Hapa sisemi maana tunaushahidi wa kutosha kuwa walimu siku zote hawatoshagi, waliopo mishahara yao hafifu, hawana nyumba, maisha magumu, maabara tatizo, vitabu tatizo, kwingineko hata chaki ni issue kupatikana.......hapa na penyewe tunajitoshelezaje?

3. Maji : Tumezungukwa na mito na maziwa lakini tatizo la maji vipi................ni asilimia ngapi ya wananchi wanapata maji safi na salama? Angalia taarifa, soma magazeti, nenda mwenyewe kaangalie wananchi wanalaumu tu................wapi pa kujivunia?

4. Afya : Hapa cha kuzungumza sina.........bahati mbaya nafanya kazi sekta ya afya...............inafika sehemu hospitali hakuna panadol, gloves, watumishi hawatoshi na mbaya zaidi inafikia wagonjwa wa UKIMWI wanagawana dawa za ARVs wakati mtu alitakiwa apewe kopo lake peke yake.......akina mama wajawazito wanalala watatu kitanda kimoja..........hapa tunajitoshleza wapi?

5. Usafiri : Barabara, Reli, Viwanja vya ndege, Meli............................treni iliyokuwako zamani iko wapi,..............hapa naomba tuelezane wapi tunajitoshelza

6. Mahakama : Imefikia sehemu moja hakimu mmoja anasikiliza kesi za mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya wilaya. Anachofanya ni kupiga tarehe....watu warudi mahabusi waendelee kuitia hasara serikali kwa kuwalisha chakula watuhumiwa. Hata kesi ndogo za kuisha ndani ya wiki moja zinachukua miezi saba hadi mwaka.............tatizo nini........

7. Polisi : Matukio ya ajabu yanatokea lakini polisi watasema polisi hawana nyumba, vitendea kazi, mishahara midogo,

8. Halmashauri : Hapa nitaenda moja kwa moja hadi katika serikali za mitaa. Serikali haina watendaji wa vijiji, kata, wakutosha.......unakuta mtendaji mmoja anahudumia vijiji vinne na bado anakaimu mtendaji wa Kata. Hivi nini kinakosekana. Watu hawana ajira lakini kila sehemu unakuta vyeo vya Kaimu afisa elimu, Kaimu Bw. Kilimo, Kaimu, kaimu, kaimu, kaimu................aghhhhhhhhhhh. Watumishi ngazi ya Halmashauri ni tatizo. Mendeleo ya jamii tabu tu.........

9. Umeme : Hapa napenyewe nashindwa niseme nini. Ni asilimia ngapi ya watanzania wanapata hii kitu na tatizo ni nini?

Mimi naishia hapa GT nitajieni sekta yoyote ambayo walau nchi yetu tunajitosheleza kwa nusu. Naongea haya kwa uchungu...........tatizo nini jamani?

Sasa chini ni baadhi ya Raslimali tulizonazo :-

  • Ziwa Victoria
  • Bahari ya Hindi
  • Serengeti
  • Kilimanjaro Mt
  • Mikumi
  • Ngorongoro
  • Selous
  • Gombe
  • Manyara
  • Tarangire
  • North Mara Gold
  • Mwadui Diamonds
  • Kahama Gold Mine
  • Tanzanite
  • Geita Gold mine
  • Lake Tanganika, Nyasa
  • Land
  • Buzwagi etc
  • Misitu.japo shule hazina madawati!!!!!

Nimetaja hayo tu.............nimatumaini yangu mtaongeza memgine. Naomba hapa tushirikishane kama Watanzania tufanye nini hapa nani tumkamate, nani tumfukuze, nani tumfunge? Japokuwa wezi wanakamatwa wanaambiwa warudishe kidogokidogo!!!!!
 
Ndugu zangu akina Ritz, Macopolo, Bungeni nisaidieni maana mie humu huona kama mko karibu sana na viongozi wetu huko juu.
 
waroho wengi,walaji wamekubuhu,waporaji ndio mtaji Tanzania itajitosheleza kwa lipi MACCM magaidi wakiwa ndio watawala
 
Back
Top Bottom