Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,997
- 3,933
Kwa kutambua juhudi za dhati kabisa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya ndugu John Pombe J Magufuli katika kuhakikisha nchi inakusanya kodi vizuri ili kuleta tija katika Maendeleo.
Aidha, hakuna Nchi inayoweza kupiga hatua pasipo kuweka mizizi imara ya ukusanyaji kodi kwenye mizunguko mbalimbali ya kifedha.
Kuna hawa watu wanaojiita Madalali wa Nyumba, Viwanja, Mashamba na Vyombo vya Usafiri ambao kimsingi wanapata pesa kila wanapomfanyia kazi mteja na pesa hiyo haiendi Serikalini hata senti tano.
Kwa muktadha huo, Serikali inapaswa kuhakikisha hawa watu ;
1. Wanasajiliwa kisheria kwa kutumia Vitambulisho vya NIDA na wawe na Ofisi zinazofahamika na TRA pamoja na Serikali za Mitaa badala ya kuwa na page tu kwenye Social Media.
Hii itasaidia pia kuondoa ulaghai na watu " kupigwa". Nchi zote ambazo zimeendelea Madalali wote wamesajiliwa na wana Ofisi zinazofahamika; ukiwa unahitaji huduma basi unaenda Ofisini kwao.
2. Walipe kodi kama Wafanyabiashara wengine
3. Walindwe kisheria kuwa mwenye Nyumba yoyote anayetaka kuuza au kupangisha Nyumba lazima apitie kwa Dalali aliyesajiliwa na kuwe na makubaliano ya namna ya yeye atakavyopata malipo ya kazi yake.
4. Mteja aliyepatiwa huduma atapaswa kuwa Na Stakabadhi ya huyo Dalali itakayokuwa na Taarifa zake pamoja na namba ya usajili na ulipaji kodi
5. Kwenye Ofisi ya Dalali kuwe na Taarifa juu ya aliyepangishwa na mpangishwaji yeyote lazima awe na Kitambulisho cha Uraia au Kibali cha kuishi Nchini Tanzania kutoka Uhamiaji.
Uhalifu na Ugaidi umekuwa mwingi siku hizi ni lazima Serikali ifungue macho.
Rais Magufuli kupitia timu yako hili mlifikirie kuhakikisha Nchi yetu inaenda sambamba na mabadiliko ya kisasa .
Ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila Raia analipa kodi na pia kuondoa kabisa ulaghai na ujanja ujanja katika nchi pamoja na kuimarisha ulinzi hasa kwa kipindi hiki tunachoelekea cha Uchaguzi.
———————-
On date: 1 January 2020
Sent from my iPhone using JamiiForums