Kuna fununu kwamba Rais Kikwete anafikiria kuunda Serikali ya Mseto kwa kuwaingiza baadhi ya wapinzani ktk baraza la mawaziri akiwemo waziri mkuu!! lakini sijui kama katiba inaruhusu ingawaje ni jambo zuri ikiwa tu CHADEMA watakubali kujiunga na serikali hiyo lakini sitapendelea kama CUF nao wajiunge kwani kutakuwa hakuna upinzani bungeni!
Akiwashirikisha wapinzani ataleta ushindani katika utendaji na wananchi watafaidi huduma. Waziri wa upinzani atajitahidi kuonyesha chama chao kina watendaji.
Katiba yetu inapaswa kumruhusu raisi kuteua mawaziri nje ya bunge ili serikali nzima iwajibike kwa bunge kikweli kweli.
Kisingov
As long as some one is a member of Parliament basi anaweza kuwa waziri.. it doesnt matter from what Party. Lakini hivi jamani mawazo yenu yamekwenda wapi?? dont get too far ahead of urselves... Hamna kitu kama hicho. hapa jamaa atawarudisha some of the ministers ambao hawajaguswana skendo hii (labda na ile ya BOT anaweza akaizingatia) lakini hakuna uhakika... Lazma some of them warudi vinginevyo atapoteza power base.
Kuwapa nafasi wapinzani katika serikali sio wazo zuri kwa sasa. Kama ana nia ya kweli basi wabadilishe sheria iwe na proportional representative badala ya simple majority. Kuwaingiza sasa haitavipa afya na wataanza kusalitiana kwa ajili ya ulaji.
Wapinzani wa kazi gani kwenye serikali saa hizi? Kwani tuna mgogoro gani wa kisiasa unaohusisha upinzani? Wapinzani wasubiri kuunda serikali yao pindi watakaposhinda katika uchaguzi mkuu. Serikali ya mseto inaweza kuwepo pindi wapinzani watakapojitahidi wakachagulika kwa kiwango cha kuwa sare au kukaribiana sare na chama tawala. Mazingira ya sasa ya Tanzania si ya serikali ya mseto, hakuna mantiki hiyo.