Serikali ya Magufuli ni maskini wa hoja

Tukwazane Taratibu

Senior Member
Dec 20, 2012
195
537
SERIKALI ILIYOISHIWA HOJA HUZAA VIHOJA.

Siku hizi ukisikiliza hotuba za Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania pamoja na maandiko ya Vyombo vya Habari vinavyoiunga mkono Serikali kama vile Jamvi la Habari, Habarileo, Uhuru nk utasikia au kusoma madai yanayojirudia rudia kuwa kuna Watanzania wanatumika na mataifa ya Nje kuidhuru nchi yetu. Madai haya yanayotolewa bila ushahidi wowote ni madai yanayoonyesha ni namna gani nchi yetu imeua kabisa utamaduni wa kukosoana.

Wakati wa mjadala wa mabadiliko makubwa ya sekta ya Madini aliyoyafanya Rais Magufuli kufuatia amri yake ya kuzuia kusafirisha makanikia, tuhuma dhidi ya baadhi yetu zilikuwa kubwa mno kiasi cha watu kuonekana wasaliti wa nchi yetu. Katika moja ya hotuba yake, Rais Magufuli alifikia hatua ya kusema kuwa ‘ msaliti dawa yake inajulikana ‘. Haikuchukua muda Mbunge Tundu Lissu, aliyekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Serikali alipigwa risasi na kukoswakoswa kupoteza maisha. Licha ya matusi yote tuliyotukanwa, madai ya $490bn ambayo Serikali iliyatoa kwa Kampuni ya Barrick yalishuka mpaka $300m ambazo hazijalipwa mpaka sasa na wala hazionekani kwenye vitabu vya Serikali kama Mapato tarajiwa ( receivables). Vijana wanatania mitandaoni kuwa tumetoka ahadi ya Noah kwa kila Mtanzania na kufikia ahadi ya Balimi 7 kwa kila Mtanzania. Hata hizo Balimi hazijapatikana.

Wakati wa mjadala wa Ndege yetu kukamatwa huko Canada, pia zilitengenezwa nadharia kuwa mimi na Tundu Lissu tumelipwa na mabeberu ili kuzuia ndege ile. Kampuni iliyowasilisha amri ya kushikilia ndege ile ililipuliwa na bomu na nchi kuingizwa kwenye taharuki bila sababu. Hatimaye Serikali imelipa zaidi TZS 60 Bilioni ili Ndege iweze kuletwa nchini. Wakosoaji wa Serikali walikosoa namna Serikali inajiendesha kana kwamba Tanzania ni kisiwa na madhara yake ni nchi kupata hasara kubwa Sana. Hivi sasa kuna kesi kadhaa Marekani na Uingereza dhidi ya Serikali yetu kutokana na mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuiheshimu au Serikali ilifanya ubabe kuivunja bila kujali sheria za kimataifa. Jumla ya madai tunayodaiwa kwenye mahakama za nje ( ninayoyajua mimi na mengine kuthibitishwa na CAG kwenye Taarifa yake ya mwaka 2016/17 ) yanafika Dola za Kimarekani Bilioni 1.48 Sawa na Shilingi Trilioni 3.3 za Kitanzania [ Madai ya Standard Chartered Bank Hong Kong $614m+$148m, Madai ya Syimbion Power $600m, Madai ya Konoike $63m, Madai ya Airbus $59m ].

Hata sasa kwenye mjadala wa kutoonekana kwa matumizi ya TZS 1.5T Serikali imejaribu kutumia maneno hayo hayo ya kuwaita wakosoaji kuwa wametumwa. Majibu rasmi ya Serikali ndani ya Bunge yamewaita wakosoaji ‘ watu wasioitakia mema nchi yetu ‘. Rais naye alipokuwa anafungua tawi la Benki ya NMB Dodoma akasema ‘ watu wanatumwa na mabeberu ‘. Unachoshangaa ni Kwamba hoja hii ya 1.5T imetoka kwenye Ripoti ya CAG ambayo ndio mamlaka ya kikatiba kufanya Ukaguzi wa Fedha za Serikali. CAG ana mamlaka makubwa kiasi kwamba Rais hana mamlaka ya kumfukuza Kazi hata amchukie namna gani. Iweje utumie Ripoti ya CAG kuihoji Serikali uwe unatumwa na watu wa Nje?

Kwenye mjadala kuhusu zabuni ya pasi za kusafiria pia Gazeti la Jamhuri lilisakamwa na Gazeti la Jamvi kuwa wametumwa na mabeberu. Baadaye naona magazeti haya yalifanya mkataba wa amani ( ceasefire). Hata hivyo gazeti la Jamhuri lilikuwa linafanya Kazi yake ya kuhoji Serikali na kupasha Habari wasomaji wake.

Wakosoaji wa Serikali wanapohoji ni Kwa maslahi ya nchi na sio kwa kutumwa. Dhana kwamba watu wanatumwa ni dhana ambayo haina nguvu na inajaribu kuua Uhuru wa maoni na wajibu wa kukosoa. Kukimbilia kuita watu majina mabaya Kwa sababu ya kuhoji masuala ya Umma tena kwa ushahidi ni dalili za wenye mamlaka kukosa Majibu na hivyo kutumia nguvu dhidi ya wakosoaji. Nadharia kuwa ukosoaji ni kutumwa unaenda kinyume na Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ambao ulijikita kwenye ‘ kukosoa na kujikosoa ‘ ili kujenga Taifa imara.

Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amenukuliwa na wanazuoni akieleza kuhusu Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 “ Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambano dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo ya kuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi”. Mwisho wa kunukuu. Inashangaza kuwa wana CCM wanaotawala sasa wanatafsiri ukosoaji kuwa ni uadui na kwenda kinyume kabisa na misingi ya Chama chao.

Kwa upande wa Chama ambacho mimi ni Kiongozi wake, Msingi wa kwanza Katika misingi kumi ni UZALENDO. Msingi huu unasema, nanukuu “ Uzalendo ndio moyo wa kuanzishwa kwa chama cha Wazalendo ikiwa ni tamko letu rasmi la kuipenda nchi yetu na utayari wa kuipigania na kuilinda. Ubora na umakini wa maamuzi yetu kama chama utapimwa kwa kuangalia ni namna gani maamuzi hayo yana faida kwa taifa letu na wananchi wake kwa leo na kesho”. Hivi sisi ACT Wazalendo kama Chama hufanya ukosoaji kwa kuzingatia maslahi ya Nchi yetu. Kila jambo tunalipima kwa kuangalia nchi inapata faida gani. Tulipoamua kukosoa takwimu za Serikali kuhusu GDP ( Pato la Taifa ) tulijua iwapo Serikali itaendelea na sera fyongo za Uchumi, Wananchi wataumia na nchi itaumia. Tangu tumetoa Tamko lile la Kamati Kuu Serikali imelegeza udhibiti wa ujazo wa Fedha kwenye Uchumi na ukuaji wake umefikia 8% kwa mujibu wa Taarifa za hivi karibuni za Benki Kuu.

Tulipoamua kuzungumzia soko la bidhaa za mbaazi, choroko nk sio kuwa tunainanga Serikali bali tunataka Serikali itimize wajibu wake Kwa raia kufuatia kuanguka kwa soko la mbaazi lenye thamani ya $250m ( zaidi TZS 500 Bilioni) kwa mwaka.
Tulipoamua kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na uchambuzi uliofutia wa majibu ya Serikali kwa Hoja hiyo ya Ukaguzi lengo letu ni kuisimamia Serikali ambayo ndio wajibu wa Wabunge na Vyama vya siasa visivyo madarakani. Hatukutumwa bali tulijituma na kujiongeza kuonyesha kuwa Fedha za Umma hazisimamiwi vizuri na Serikali ya awamu ya 5 iliyo chini ya CCM.

Wakosoaji wa Serikali wanatimiza wajibu wao kama Wananchi. Hawatumwi na mabeberu. Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kutumwa na mabeberu kuchafua sura ya nchi ni uasi na adhabu yake ni kifo. Serikali badala ya kulalamika tu kwenye mikutano Kuwa wakosoaji wake wanatumwa, ichukue hatua za kisheria kuwashtaki hao wanaodhaniwa kutumwa ili wakosoaji wa kweli waendelee na wajibu wao. Tuhuma za kutumwa hakiwezi kuwa kichaka cha kujifichia na kukwepa kujibu Hoja za Msingi.

Wananchi sasa waanze kukataa nadharia za kitoto, zilizopitwa na wakati Kuwa wakosoaji wa Serikali wametumwa. Wananchi wahoji ushahidi wa madai hayo. Wasikubali tuhuma hewa zinazotolewa ili kuficha ukweli wa masuala yanayoibuliwa. Serikali ina Vyombo vyenye uwezo mkubwa wa kuchunguza, Wananchi watake ushahidi kutoka vyombo Hivi. Propaganda za ‘ wanatumiwa ‘ zikiachwa tu watu wataumia. Tutajenga Taifa la hovyo, la watu wasiohoji, wanaodanganywa tu.

Kwa mwananchi, hakuna uzalendo bora zaidi kuliko uzalendo wa kuikosoa Serikali ya nchi yako. Uzalendo mkubwa zaidi ni kuitetea nchi yako, si Serikali! NCHI yako.

Ndimi Zitto Kabwe (MB).
 
Weka audio au video Mkuu, andiko ni refu sana, umeandika ila ata robo sijafanikiwa kusoma, ila ujumbe umewafikia wahusika
 
Kumbe ni ujumbe kutoka kwa zitto! Yuleyule msaliti wa chama! Kesho na keshokutwa atalisaliti taifa. Msaliti ni msaliti tu. Au kashasamehewa?
 
Kachama ka ACT na Zitto wao wana ushawishi gani wa hoja?
 
Back
Top Bottom