Waziri wa elimu ameulizwa swali ni kwanini walimu wanadai hawajashirikishwa suala la elimu bure anapaniki.Jamani hawa watu wanajua wanachokifanya?
Suala la elimu bure ni mchakato unaotakiwa kujengewa msingi imara na ikiwezekana lipelekwe bungeni kutungiwa sheria,sasa pesa zinazotakiwa ni b30 lakini zimepelekwa b11.
Halafu kama ni kweli waalimu wanalalamika hawajashirikishwa, je hatuoni kama kuna tatizo hapa?
Nchi haiwezi kuedeshwa kienyeji au kibabe au kwa amri amri,suala la elimu bure ambalo ni Sera ya CHADEMA linahitaji kufanyiwa kazi na wadau wote wakiwemo walimu wahusishwe,huyu rais anaweza kutupeleka shimoni.
Hilo nalo nenokama wakweli walipe MADENI YA WALIMU KWANZA.
UKWELI daima ni UKWELI, na wewe nimekukubali KWELI NI MKWELI, hata kubenea wa kabla ya Lowassa sio huyu wa sasa anayemuandama Zuberi zitto kabwe na kumuacha Freeman aikaeli Mbowe aliyetorosha mabilioni ya shilingi kwenda nje ya nchi kinyemela. 😀😱Inawezekana kweli CDM wangeweza kutoa mchango mzuri kuhusu hoja ya elimu bure. Naomba wachangiaji mnisaidie kuelewa, CDM ipi tuiombe mchango wa mawazo yao hii ya Lowasa au iliyokufa ya Dr. Slaa. Kwa mtazamamo wangu hizi mbili zinatofautiana mno. Ni kama ninavyoliona Mawio na Mwanahalisi kabla na baada ya Ujio wa Lowasa CDM.