domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,588
- 1,760
Nchi ilipobadili utaratibu wa kurusha matangazo ya Televisheni kutoka katika mfumo wa analogi kwenda digitali, iliwalazimu wananchi wa Tanzania kuingia gharama zakununua vinga'muzi na hata wengine televisheni mpya kuendana na mfumo huo wa kidigitali.
Wananchi wakaingiwa na hofu kuwa itawapasa kulipia matangazo ya televisheni. Serikali kupitia TCRA ikawatoa hofu wananchi kuwa kutakuwa na stesheni ambazo hazitalipiwa.Kuna stesheni za ndani zikawa 'lebelled' local, stesheni hizo zilizokuwa labelled local wananchi wakaambiwa zitakuwa za bure au free to air, hivyo ukishanunua king'amuzi chako chochote basi LAZIMA hizo stesheni utaziona pasipo malipo yoyote.
Leo hii hayo yaliyozungumzwa na serikali nakuwekewa utaratibu hayafanyiki hivyo. Katika baadhi ya ving'amuzi vya Star Times haiwezekani kuona hizo stesheni za local kama huajlipia. Kwa mujibu wa Star Times wenyewe wanadai hilo ni tatizo la muda tu wanalifanyia marekebisho. Kama kweli marekebisho yanafanyika au la! sijui! lakini sasa yapata mwezi wa nne!
TCRA kwa upande wao wanakiri kulifahamu hili tatizo na wanakiri kulizoea na kuliona la kawaida. Nao wanadaai watakaa na Star Times kulizungumzia hilo.
Wakati TCRA ikiwa inafahamu hii dhulma hakuna taarifa yeyote kwa umma iliyotolewa aidha kuelezea mabadiliko ya utaratibu au kuonesha kutambua uwepo wa tatizo hili kwa sababu wanazozifahamu wao wenyewe. Hali ya kutotoa taarifa yeyote wala kuchukua hatua yeyote kunaweza kukaleta tafsiri nyingi tu miongoni mwa watu. Mfano mimi naweza kufikiri TCRA imelipuuzia hili suala kwa vile litakuwa linawagusa watu masikini, watu wa hali ya chini wasioweza kulipia kuangalia televisheni kwa kuwa watu wa hali ya chini si chochote wala silolote katika nchi hii kama ambavyo ilivyozoeleka.
Serikali ya awamu ya tano ambayo yenyewe imejinasibu kumuhangaikia mtu masikini aliyekuwa akiishi kama yuko motoni nae aishi kama yupo peponi imeshindwa kabisa kulishughulikia hili? Je ni kweli serikali hii ambayo kwa kiasi cha kutosha imejenga Imani kwa wananchi hasa masikini kwa kuwarudishia heshima imewekwa mfukoni na hawa Star Timeskiasi cha kuwafanya TCRA kutoishughulikia kero inayowakabili wananchi kwa kuizoea na kuifanya ya kawaida? Haki ya watu wanyonge ambayo haijatolewa kwa kipindi kirefu sasa ni haki iliyodhulumiwa. Nani atawalipa wanyonge haki hii?