Yes tupo msitari mmoja isipokuwa mimi nakataa kulazimisha kitu ili tuonekane tunafanya kama Ulaya.. Hii ndio nisichokubaliana nacho kwa sababu hata ukitazama heavy equipment wazungu wamezitumia sio kwa sababu walitaka kuwaondoa wakulima wadogo wadogo isipokuwa demand ya mazao yao iliongezeka kiasi kwamba jembe la mkono lisingeweza kutosheleza demand ya mazao yao...Hivyo utaalam wa kuunda heavy equipment ukachukua nafasi kwa sababu jembe la mkono halikuweza tena kutosheleza na ardhi ikatakiwa kubwa zaidi ili kuweza kuzalisha kiwango kinachotakiwa - Necessity was the mother of invention!Mkuu nadhani tupo on the same boat mimi siongelei kupunguza for the sake ya kupunguza.., pia siongelei kwamba hii issue itokee overnight.., hapana. Ninachosema mazao kama nafaka ambayo yanaweza yakawa produced efficiently using heavy machinery yafanywe hivyo (na sio na private sectors wala muwekezaji bali na state/vyama vya ushirika...) na profit yake hii yote iende kwenye services na welfare za wananchi (na pia hii itafanya chakula kishuke sana bei).., kwahiyo utaona na heavy production power ya hizi mashine individuals watakuwa hawana faida sana na kulima hizi nafaka swali linakuja watafanya nini..? majibu ni kama ifuatavyo:-
Kwahiyo mkuu mimi point yangu ya 10% ni kwamba ile efficiency kama taasisi kama mbili au serikali inaweza ikalima mwaka mzima na kulisha watu wote (kwa nafaka) kwanini wananchi wengine wasiconcentrate kwenye kulima vitu vingine ambavyo wanaweza kuvifanya effectively.
- Kwa kuwa na viwanda au food processing industries wanaweza kupata ajira
- Nafaka ndio itakuwa sio profitable kulima lakini kuna mazao ambayo ni valueable per hectare, mfano mboga, viungo maua, uyoga n.k. hawa wakulima au hobbyist wanaweza part time na efficiently wakalima haya mazao ambayo wakiuza yatawapatia faida huku wana uhakika kwamba mashamba ya ushirika/state yanawaletea chakula cha uhakika na faida inayopatikana inawasomesha na kuwatibu watoto wao na ndugu zao (yaani mzazi anao uhakika kwamba akizaa tu mtoto wake atafika university bila kuja na kudai ada wala usumbufu wowote
- Pia serikali inaweza ikasimamia mashamba makubwa ya mifugo ambayo yatahakikisha kuna nyama ya kutosha, maziwa pamoja na kusindika nyama (beef) n.k. hii itapunguza ila adha ya sasa kila mtu anataka mifugo mingi na kugombania sehemu ya malisho.., sababu as a community tutajua kwamba tuna uhakika wa nyama ya bei nafuu.
Ila what is happening now kwa kweli inatisha sana tena sana tunauza nchi yetu wenyewe mchana kweupe na viongozi wetu wanatuuza sisi na wajukuu zetu bila kutupa option.., Itakuja kufika wakati mtu elimu hauna, pa kulima hauna wala kazi ya kufanya haipo (unakuwa mtumwa kwenye nchi yako mwenyewe).., tunapoenda yaani hata wizo utakuwa ni career ujambazi utaongezeka, chuki, umasikini na matabaka makubwa sana..., kama baba yako ni masikini leo basi hadi kitukuu kitakuwa masikini...
Kweli we need to rethink before its too late
Tofauti na wao, sisi tunachogombea hapa ni ARDHI, hakuna mkulima wala mchuuzi mwenye nia ya kuongeza uzalsihaji hilo ndio ukweli, kinachofanyika leo ni udalali wa ardhi na viongozi wetu ndio macho yanawatoka..Serikali imeshindwa kutazama demand ya chakula badala yake wanatazama demand ya ardhi kuwa ndio biashara.. Kweli ni busara zaidi kuweka kilimo mikononi mwa serikali au wananchi wakafungua mashamba makubwa kwa sababu ndivyo alivyofikiria Nyerere kuhakikisha ardhi inabakia mikononi mwa wananchi (serikali), tunazalisha kulingana na mahitaji ili kukuza uchumi wetu lakini wazungu kama tabia yao ama kutokana na kushuka kwa uchumi wao miaka hiyo wakapunguza mahitaji ya mali za nje ikiwa ni pamoja na mazao yetu. Tulianguka lakini ukitazama kulikuwa na goals tumeweka na kuthamini ardhi na Uhuru wetu..
Binafsi ningependa kujua sababu hasa kwa nini kilimo kinakosa soko ndani ingawa demand ya vyakula imeongezeka kwanza kabla ya kuchukua hatua zaidi. Lazima kuna tatizo la kisera ambalo linawakwaza wananchi wakulima kujipanua ama kuweka nguvu zao ktk kilimo, ufugaji na uvuvi. Hii habari ya Kilimo kwanza ni policy mbovu ambazo zimetungwa na wanansiasa badala ya kupitia kwa mkulima. Halafu pia tukumbuke tu kwamba thamani ya shilingi inazidi kuporomoka vibaya sana wakati hali ya maisha inapanda kwa kasi muathirika mkubwa ni mkulima wa leo ambaye atanunua mahitaji yake kwa thaminisho la dollar.
Kwa hiyo vitu vyote vinakwenda sambamba, ili kuwawezesha wakulima tunatakiwa kuanzisha viwanda ndani nchini kulingana na mahitaji yaliyopo, tufiirie kujitegemea wenyewe. Necessity ipo! toka Ukulima hadi viwanda soko lipo kwa nini bado tunaagiza mali kutoka China, India na kadhalika wakati soko lipo ndani na hakuna sababu ya kimazingira, utaalam ama uwezo kuanzisha viwanda hivi bali tunataka kupanua kilimo, kupunguza ajira za wananchi wasiopungua asimilia 70 wakati hakuna viwanda wala ajira sehemu nyinginezo ni kujiongezea matatizo zaidi. leo hii nasikia zaidi ya asilimia 50 ya graduates wa University zetu hukosa ajira, hivi unafikiri hawa vijana wanafanya nini leo?