Serikali ya Kikwete impeleke Lowassa mahakamani

Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
392
Kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania alijiuzulu kwa tuhuma za Richmond hakuwahi kufikishwa mahakamani, na kwa kuwa inasemekana alikatwa jina kwa ajili ya tuhuma hiyo alipotaka kurusha kete kunia Urais wa JMT, napendekeza Serikali ya Kikwete imfungulie mashitaka na kumpeleka mahakamani mara moja kwa tuhuma tajwa.

Kinyume chake kuanzia leo ifahamike kuwa Lowassa yuko safi: wachafu wanajijua na walijificha chini ya mwavuli wa Lowasa.

Na ikiwa hali ndiyo hiyo, basi wamwache mzee wa watu aonje Urais wa JMT chini ya mwavuli wa UKAWA/CHADEMA ingawa nadhani hajawahi hata kuota maishani kuwa angeiacha CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo.
 
Serikali ya ccm ndo.watuhumiwa namba moja labda waende kujishtaki wenyewe
 
Kwa kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania alijiuzulu kwa tuhuma za Richmond, na kwa kuwa huyo mtuhumiwa kutoka wakati huo hakuwahi kufikishwa mahakamani, na kwa kuwa inasemekana alikatwa jina kwaajili ya tuhuma hiyo, napendekeza Serikali ya Kikwete imfungulie mashitaka na kumpeleka mahakamani kwa tuhuma tajwa.
Kinyume chake kuanzia leo ifahamike kuwa Lowasa yuko safi: wachafu walijificha chini ya mwavuli wake.
Na ikiwa hali ndiyo hiyo, basi wamwache mzee wa watu aonje Urais wa JMT chini ya mwavuli wa UKAWA/CHADEMA ingawa nadhani hajawahi hata kuota maishani kuwa angeiacha CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo.

Wengi hamfwatilii mambo... kesi ya Richmond iliwahi pelekwa mahakamani ila ktk mazingira ya Utata mshirika wa JK ktk kuileta hii kampuni nchini bwana Naeem Gire aliachiwa HURU!!!

CCM HAWANA UBAVU WA KUONGELEA WALA KUKEMEA UFISADI....
 
Ni kwa sababu hiyo Mkuu nasema basi wamwache Lowasa huru, kinyume chake bosi wake wa wakati huo awajibike.
JK namwonea huruma mwaka huu sijui kama atapata pa kutokea.
 
sakata la escrow mapendekezo ya bunge. kuna waziri wa ccm ana makalio utafikiri yuko kwenye mashindano ya africa university question .alivyo kaa tako mmoja kwenye kiti.SPIKA; wabunge mna semaje YEYE: yarudi kwenye vyombo vya uchunguzi.ccm mi sina hamnao
 
Kesi ikienda kwa pilato basi JK atalala segerea, hawawezi kamwe kupeleka mahakamani
 
Kwa kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania alijiuzulu kwa tuhuma za Richmond hakuwahi kufikishwa mahakamani, na kwa kuwa inasemekana alikatwa jina kwa ajili ya tuhuma hiyo alipotaka kurusha kete kunia Urais wa JMT, napendekeza Serikali ya Kikwete imfungulie mashitaka na kumpeleka mahakamani mara moja kwa tuhuma tajwa.
Kinyume chake kuanzia leo ifahamike kuwa Lowasa yuko safi: wachafu wanajijua na walijificha chini ya mwavuli wa Lowasa.
Na ikiwa hali ndiyo hiyo, basi wamwache mzee wa watu aonje Urais wa JMT chini ya mwavuli wa UKAWA/CHADEMA ingawa nadhani hajawahi hata kuota maishani kuwa angeiacha CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo.
Mkuu unadhani JK atasalimika?
 
Politics ? Kwa mpango huu CCM itatawala milele na milele hawa watu kwa nini hawakumfikisha mahakamani hata TUKUKURU hawana akili nzuri Lowasa president I doubt it
 
Lowasa safi
RICHMOND NI MAAGIZO KUTOKA NGAZI ZA JUU alipewa mamlaka na mkuu wa nchi na alimwambia asiache kusaini mkataba ule
 
Kwa kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania alijiuzulu kwa tuhuma za Richmond hakuwahi kufikishwa mahakamani, na kwa kuwa inasemekana alikatwa jina kwa ajili ya tuhuma hiyo alipotaka kurusha kete kunia Urais wa JMT, napendekeza Serikali ya Kikwete imfungulie mashitaka na kumpeleka mahakamani mara moja kwa tuhuma tajwa.
Kinyume chake kuanzia leo ifahamike kuwa Lowasa yuko safi: wachafu wanajijua na walijificha chini ya mwavuli wa Lowasa.
Na ikiwa hali ndiyo hiyo, basi wamwache mzee wa watu aonje Urais wa JMT chini ya mwavuli wa UKAWA/CHADEMA ingawa nadhani hajawahi hata kuota maishani kuwa angeiacha CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo.

KIAPO CHA KUTUNZA SIRI ZA SERIKALI ALICHOKULA LOWASA NDIO KINAMZUIA KUMWAGA MBOGA NA UGALI JINSI KIKWETE KWENYE RICHMOND KWA MAELEKEZO YAKE KWA LOWASA SAWA NA MAELEKEZO YA NYERERE KWA RASHIDI KUHUSU OPERESHENI VIJIJI LIKAMUANGUKIWA RASHIDI WATU WALIPOLIWA NA SIMBA.
UKAWA waitega CCM kusishinikiza serikali yake kumpeleka Mahakamani Lowasa kama jitihada za kumzuia asigombee uraisi baada ya Magufuli kupwaya kwa Lowasa, UKAWA wanaliongejea hilo ili Lowasa atoe siri zote na ushahidi wa kina jinsi Kikwete alivyoshiriki na kulazimisha uwepo wa Richmond na kumfanya Lowasa mbuzi wa kafara.
Vikao vya mkakati vya UKAWA wanataka kuitumia kete hiyo kubuaibisha mwenyekiti wa CCM na chama chake kuwa ndio waliopika Richmond na kumsulubu Lowasa "to save government face". Akizunguza na Zanzibar Post kwa masharti ya kutotajwa jina lake mmoja wa wana makakati anasema CCM ikiteleza kumpeleka LOwasa mahakani wakati huu itaumbuka, maana Lowasa kupitia wanasheria wa Chadema ataanika siri na shahidi wote alionao kuhusu Kikwete na Richmond, na hapo atakuwa hatatoa siri za serikali kwani atakuwa ametakiwa na mahakama kusema kweli na kweli tupu na huo ndio ukweli.
Mtoa taarifa huyo alisema Lowasa ni sawa na Rashidi Mfaume Kawawa waziri mkuu aliyemtangulia ambaye aliyepewa maagizo na Nyerere kuhusu operesheni vijiji, Kawawa akatekeleza wananchi walipoliwa na simba kwenye vijiji vya ujamaa hewa likamuangukia Rashidi na Nyerere akanyamaza kimya, lilofuata Kawawa nje kulinda serikali. Na mpaka amekufa Kawawa hakupata nafasi ya kulieleza maana atakuwa anatoa siri za serikali, sheria inaweza kuchukua mkondo wake.
Na Lowasa ni hivyo hivyo anakaa kimya akijua kuanika ushahidi hadharani ni kutoa siri lakini akitakiwa na mahaka kufanya hivyo atakuwa hajatoa siri ila ametii amri ya mahakama kwani mahakama siku zote inataka kutenda haki na haki haitatendeka kama ukweli hautajulikana.
CCM ni vyema ikakumbuka msemo wa watu wa pwani kuwa muungwana akivuliwa nguo huchutama, hasimami. sasa kama CCM itataka kusimama baada ya kuvuliwa nguo, nyeti zitaonekana na kutibua nyongo za wapiga kura, na kuinufaisha UKAWA maana ili Lowasa asishiriki uchaguzi inabidi kesi hiyo iende fasta na kuhukumiwa, na hapo ndio kina Lisu walipojipanga kuanika madudu ya Kikwete na CCM hadharani kuhusu Richmond, "Yaani uchaguzi wa mwaka huu kama sinema vile" anasimulia mtoa taarifa.
 
Ukweli ni kwamba Lowassa si msafi lakini ukweli usiopingika zaidi CCM can't risk taking Lowassa to court. Wataishia kupiga kelele majukwaani. Wakithubutu kumpeleka mahakamani Lowasa ndio siku utakayosikia kuwa watu wote halisi waliowahi kuhusika na ufisadi wa nchi hii watawekwa uchi mchana kweupe. Hakuna jiwe litakalosalia CCM kuanzia Mwenyekiti wao hadi shadadi wa mwisho
 
Back
Top Bottom