Serikali ya Kikwete impeleke Lowassa mahakamani

Kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania alijiuzulu kwa tuhuma za Richmond hakuwahi kufikishwa mahakamani, na kwa kuwa inasemekana alikatwa jina kwa ajili ya tuhuma hiyo alipotaka kurusha kete kunia Urais wa JMT, napendekeza Serikali ya Kikwete imfungulie mashitaka na kumpeleka mahakamani mara moja kwa tuhuma tajwa.

Kinyume chake kuanzia leo ifahamike kuwa Lowassa yuko safi: wachafu wanajijua na walijificha chini ya mwavuli wa Lowasa.

Na ikiwa hali ndiyo hiyo, basi wamwache mzee wa watu aonje Urais wa JMT chini ya mwavuli wa UKAWA/CHADEMA ingawa nadhani hajawahi hata kuota maishani kuwa angeiacha CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo.

atapelekwa tu alitumia madaraka vibaya
 
Lowasa aliwahi kusema kwenye kikao cha cc ya Chama cha zamani, Jk sinilikupigia cm ulipokuwa nje ya nchi? Kimya hadi sasa. lowasa kupelekwa Court ni kuumbua serikali
 
Kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania alijiuzulu kwa tuhuma za Richmond hakuwahi kufikishwa mahakamani, na kwa kuwa inasemekana alikatwa jina kwa ajili ya tuhuma hiyo alipotaka kurusha kete kunia Urais wa JMT, napendekeza Serikali ya Kikwete imfungulie mashitaka na kumpeleka mahakamani mara moja kwa tuhuma tajwa.

Kinyume chake kuanzia leo ifahamike kuwa Lowassa yuko safi: wachafu wanajijua na walijificha chini ya mwavuli wa Lowasa.

Na ikiwa hali ndiyo hiyo, basi wamwache mzee wa watu aonje Urais wa JMT chini ya mwavuli wa UKAWA/CHADEMA ingawa nadhani hajawahi hata kuota maishani kuwa angeiacha CCM iliyomlea na kumfikisha hapo alipo.

Wakimfungulia mashitaka tu mahakamani jua wamejishitaki wenyewe. Kila aliyetia mkono na mdomo kwenye hilo sakata la Richmond ataingia mahakamani.

Serikali mtajihukumu wenyewe jaribuni muuone huo mziki.
 
Back
Top Bottom