Serikali ya Kenya yarekodi ongezeko kubwa la matumizi kwa "burudani/sherehe" za Ofisi ya Rais, lengo la ukusanyaji kodi 2019/20 lashindwa kufikiwa

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,282
EbRNds_WkAAz1wJ.jpeg

Ofisi za Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wa Rais William Ruto zilitumia KSh1.18 bilioni kwa sherehe na maadhimisho mbali mbali, katika miezi tisa iliyopita hadi Machi 2020; hii ikiwa ni ongezeko la Sh422 milioni kutoka kipindi kama hicho kilichopita mwaka jana.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na jarida la Business Daily, takwimu zilizopatikana kutoka kwa Mdhibiti wa Bajeti zinaonyesha kwamba ofisi za Rais Uhuru Kenyata na Makamu wa Rais Ruto, ziliongeza matumizi kwa asilimia 55.6 ikilinganishwa na KSh758.2 milioni iliyotumika katika kipindi kama hicho.

Hazina ya nchini Kenya ilitangaza hatua mpya za kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma mnamo Septemba mwaka jana zilizojumuisha kupunguza gharama za matangazo, safari, mafunzo, na kulazimu ofisi za umma kununua samani zilizotengenezwa nchini humo.

Ongezeko la bajeti ya matumizi ya burudani inaonyesha kwamba ofisi mbali mbali za serikali bado hazifuatii wito wa hazina wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Takwimu hizo pia zilionyesha kuwa Matumizi ya "hospitality" kwa wizara, Idara za Majimbo na wakala (MDA) iliongezeka hadi KSh4,5 bilioni, ongezeko la asilimia 18 kutoka KSh3.8 bilioni lililotumika mwaka uliopita.

Bajeti ya burudani kwa ofisi ya Rais ya KSh1.18 bilioni ilichukua robo ya KSh4 bilioni bilioni iliyotumiwa na ofisi za umma kwenye sherehe na maadhimisho mbali mbali. Takwimu pia zinaonyesha watumizi wengine wa juu ikiwa ni pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani kwa KSh900.2 milioni, kushuka kutoka KSh1.08 bilioni zilizotumika katika kipindi kama hicho cha nyuma. Bajeti ya burudani ya Wizara ya Mambo ya nje iliongezeka kwa asilimia 69 hadi KSh604.4 milioni kutoka KSh357 milioni katika kipindi kilichopita.

Kutokana na Bajeti ya 2019/2020 mamlaka ya Mapato ya Kenya imeonekana kushindwa kutimiza lengo lake la ukusanyaji wa kodi hali inayoashiria kazi kubwa mbeleni. Ukusanyaji wa kodi unaonekana kutokuongezeka kwa miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka 2020 kabla ya janga la corona kuingia nchini humo.


Source: https://www.kahawatungu.com/uhuru-ruto-offices-increased-spending-entertainment-sh422-million-nine-months/

===
President Uhuru Kenyatta and Deputy President William Ruto spent Sh1.18 billion on parties and receptions, in the last nine months to March; a Sh422 million increase from the last similar period.

According to Business Daily, data obtained from the Controller of budget shows that the presidency, which comprises both President Kenyatta’s and DP Ruto’s office, increased the spending by 55.6 percent compared to the Sh758.2 million spent in a similar period last year.

The Treasury announced new austerity measures in September last year on advertising, trips and training as the State moved to limit the misuse of taxpayers’ funds. Among the measures was a directive to the government agencies to purchase only locally manufactured furniture fittings.

Read: Govt Suspends All Capital Expenditure In State Agencies To Support Big Four Agenda

The entertainment budget increase demonstrates that the various arms of government are yet to adhere with the calls by the President and the treasury to cut down on non-essential expenditure, as the state seeks to free up funds for development and essential services such as education and health.

The data also showed that Hospitality Expenditure for 71 ministries, State departments and agencies (MDAs) increased to Sh4.5 billion, an 18 percent increase from the Sh3.8 billion spent a year before.

The Presidency’s Sh1.18 billion entertainment budget accounted for a quarter of the Sh4.5 billion spent by public offices on parties and receptions.

Data also showed other top spenders including the Interior Ministry at Sh900.2 million, a drop from Sh1.08 billion spent in the previous similar period.

The Ministry of Foreign Affairs entertainment budget increased by 69 percent to Sh604.4 million from Sh357 million at the previous period.

The 2019/2020 budget revealed that the Kenya Revenue Authority had missed its tax collection target signifying a huge task ahead. The Tax collector posted a flat growth within the first three months of 2020, even before the crisis brought about by the Corona virus pandemic.
 
IMG_20200622_173551.jpg

Huyu kila akienda press...anakula milioni ya kujunulia chai na maandazi..unategemea nn
 
Back
Top Bottom