Katika hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa Mkoa wa Singida ameagizwa na ofisi ya Waziri Mkuu kuwa azunguke kwa wananchi katika mkoa wake kufuta kauli ya kuwa Mkoa wa Singida watu wasilime mahindi kama alivyokuwa ameamrisha. Je Mkuu wa Mkoa huyo atakuwa tayari kulamba matapishi yake? Yupo tayari kumwomba radhi Mbunge wa Iramba mashariki Mama Salome Mwambu aliyemkemea vikali na kumwambia katika Kikao kuwa watakaolima mahindi mwaka huu wakale kwa Salome Mwambu?. Kikwete hujamsaidia Mkuu huyu, dawa yake ni kumwondoa Singida, kwanza ashitakiwe kwa ukatili aliotufanyia Singida, Mtoto wake kamwagia vijana wetu wa Singda Sumu na hamjamtia hatiani. Hali hiyo nia ngumu, sitegemei kama atafanya mkutano wowote wa hadhara akasikilizwa. Kama familia yake inaongoza kutuua tutapata wapi nafasi ya kumsikiliza. Endeleeni kumwacha ila Singida tunajua kuwa Kikwete haututakii mema. Maana ungetutakia mema, kwa ubaya wa wazi tuliokueleza kwa njia mbalimbali yakiwemo magazeti, au hata barua unazopokea toka kwa mawaziri wako, huyu ungemwacha akachunge ng'ombe. La kama hamwezi kufanya vile kwa busara, mwacheni........... tutajitahidi hivo hivo kumwonyesha kuwa kwa kuwa hafai basi tutampa ushirikiano sifuri. Aombe radhi hadharani kwanza!