Serikali ya JK yaamuru mkuu wa mkoa kula matapishi yake

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Katika hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa Mkoa wa Singida ameagizwa na ofisi ya Waziri Mkuu kuwa azunguke kwa wananchi katika mkoa wake kufuta kauli ya kuwa Mkoa wa Singida watu wasilime mahindi kama alivyokuwa ameamrisha. Je Mkuu wa Mkoa huyo atakuwa tayari kulamba matapishi yake? Yupo tayari kumwomba radhi Mbunge wa Iramba mashariki Mama Salome Mwambu aliyemkemea vikali na kumwambia katika Kikao kuwa watakaolima mahindi mwaka huu wakale kwa Salome Mwambu?. Kikwete hujamsaidia Mkuu huyu, dawa yake ni kumwondoa Singida, kwanza ashitakiwe kwa ukatili aliotufanyia Singida, Mtoto wake kamwagia vijana wetu wa Singda Sumu na hamjamtia hatiani. Hali hiyo nia ngumu, sitegemei kama atafanya mkutano wowote wa hadhara akasikilizwa. Kama familia yake inaongoza kutuua tutapata wapi nafasi ya kumsikiliza. Endeleeni kumwacha ila Singida tunajua kuwa Kikwete haututakii mema. Maana ungetutakia mema, kwa ubaya wa wazi tuliokueleza kwa njia mbalimbali yakiwemo magazeti, au hata barua unazopokea toka kwa mawaziri wako, huyu ungemwacha akachunge ng'ombe. La kama hamwezi kufanya vile kwa busara, mwacheni........... tutajitahidi hivo hivo kumwonyesha kuwa kwa kuwa hafai basi tutampa ushirikiano sifuri. Aombe radhi hadharani kwanza!
 
Kwakuwa yupo pale kama kibaraka, yeye hufuata kila anacho agizwa bila kuhoji kwani asipo fanya hivyo kibarua kitaota nyasi.
Ndio tatizo la vyeo vya shukrani.
 
Ni hakika huyu mkuu wa mkoa wa Singida hafai maana mara nyingi amesababisha kutokuelewana kati ya wananchi wa wilaya anayotoka ya Simanjiro kama sikosei kuhusu migogoro ya ardhi. Unajua huyu mkuu kwa asili yao huwa mkuu katika ukoo akisema hakuna wa kumpinga kwa hiyo anachukulia watz wote ni wakuamrishwa. Chakufanya afukuzwe na wala siyo kuomba ardhi ili wengine wajifunze
 
Kwa nini huyo Mkuu wa Mkoa alipiga marufuku watu kulima mahindi? Na kwa nini Ofisi ya waziri Mkuu inataka abadilishe amri yake hiyo?
 
Maeneo mengi ni kame kule, mazao ya mtama ndiyo yanayohimili ukame zaidi. Tangu siku nyingi wananchi wa Singida wanashauriwa wasilime mahindi.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa Mkoa wa Singida ameagizwa na ofisi ya Waziri Mkuu kuwa azunguke kwa wananchi katika mkoa wake kufuta kauli ya kuwa Mkoa wa Singida watu wasilime mahindi kama alivyokuwa ameamrisha. Je Mkuu wa Mkoa huyo atakuwa tayari kulamba matapishi yake? Yupo tayari kumwomba radhi Mbunge wa Iramba mashariki Mama Salome Mwambu aliyemkemea vikali na kumwambia katika Kikao kuwa watakaolima mahindi mwaka huu wakale kwa Salome Mwambu?. Kikwete hujamsaidia Mkuu huyu, dawa yake ni kumwondoa Singida, kwanza ashitakiwe kwa ukatili aliotufanyia Singida, Mtoto wake kamwagia vijana wetu wa Singda Sumu na hamjamtia hatiani. Hali hiyo nia ngumu, sitegemei kama atafanya mkutano wowote wa hadhara akasikilizwa. Kama familia yake inaongoza kutuua tutapata wapi nafasi ya kumsikiliza. Endeleeni kumwacha ila Singida tunajua kuwa Kikwete haututakii mema. Maana ungetutakia mema, kwa ubaya wa wazi tuliokueleza kwa njia mbalimbali yakiwemo magazeti, au hata barua unazopokea toka kwa mawaziri wako, huyu ungemwacha akachunge ng'ombe. La kama hamwezi kufanya vile kwa busara, mwacheni........... tutajitahidi hivo hivo kumwonyesha kuwa kwa kuwa hafai basi tutampa ushirikiano sifuri. Aombe radhi hadharani kwanza!
Hii ni wapi tena? Singida kule ambapo ni ngome ya CCM?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom