Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 7,202
- 9,820
Kitendo cha Serikali kuanza kuzuia Watz wenye mapenzi mema kumwombea Rais wa TLS,Mbunge wa Singida Mashariki, Mwanasheria wa CHADEMA na Mnadhimu Mkuu wa KUB Mhe. Antipas Tundu Lissu zina akisi taswira hasi kwa jamii ya Kitanzania na ishara mbaya sana.
Baada ya TL kupigwa risasi 28-38 kuna Watanzania mamia kwa maelfu waliguswa na tukio hili na wakaamua kujitolea damu, kufanya maombi makanisani na kusoma albadir Misikitini ili kuonyesha mapenzi mema walokuwa nayo kwa Mtanzania mwenzao TAL. Jambo la kushangaza ni kwamba mambo yote haya yamekatazwa na kuzuiliwa na Serikali ya John Pombe Magufuli kwa sababu zisizo na msingi. Wakti Baba wa Taifa anaumwa, Mkapa anaumwa, Kikwete anaumwa, Marehemu Sitta anaumwa na Job Ndugai anaumwa, Serikali ilihimiza watu waombe ili kuleta uponyaji. Ni bahati mbaya tu Mzee Sitta ndiyo Mungu aliruhusu kumchukua. Leo iweje watu wazuiwe kuomba kwa ajili ya Tundu Lissu?? Kuna nini??
Kama serikali imefikia mahali pa kuzuia hata ibada kwa ajili ya kumwombea Mtanzania mwenzao aliyepigwa risasi 38 kama mnyama tena mchana kweupe kwenye viunga vya Bunge na hawa watu wasiojulikana wakatokomea kusikojulikana ni hali ya hatari sana. Kama sheikh, Padre, Askofu au Mchungaji na waumini wao watazuiwa kuombea ndugu zao walio wagonjwa, wenye shida na uhitaji kwa namna yoyote ile ni kwamba Serikali ya CCM sasa imeamua kupambana na Mungu.....!!!
Mungu siku zote huwa hataki kuwa beeped! Uki-beep yeye anapiga moja kwa moja. Sasa Serikali hii ya CCM na ya JPM imeamua kum-beep Mungu kwa kuzuia watu kufanya ibada zao kumwombea ndugu yao Antipas Tundu Lissu. Tusubiri, mbona ni swala la muda tu na Mungu atapiga!!Anguko lake CCM watajuta kwa kosa hili la kumpuuza Mungu wa Mbinguni..!!!
CCM wajue kwamba kuna MAOMBI YA KIMYA KIMYA YANAENDELEA NCHI NZIMA SIJUI HAYO WATAYADHIBITI VIPI....Labda kwa kutumia watu wasiojulikana ambao Mungu ANAWAJUA VIZURI SANA....Tusubiri matokeo.