Awamu ya nne ya mzee Kikwete tulishuhudia ufisadi mkubwa ukifanyika, tuliona jinsi walivyojigawia pesa za EPA, jinsi walivyochota pesa za Tegeta Escrow, ufisadi wa Meremeta na TANGOLD nk. Lakini angalau ufisadi huo ulikuwa ukijadiliwa bungeni na wawakilishi wa wananchi na serikali kutoa ufafanuzi na mwisho serikali kujivua lawama.
Serikali ya awamu hii ni tofauti, hiyo nafasi ya kujisafisha kupitia bunge haipo tena, serikali imejaa kiburi, haioni sababu ya kuwa please wananchi wake hata kwa kuwadanganya kupitia bunge. inafanya ufisadi nje nje kwa sababu inajua wananchi imewaziba midomo hata kama wakijua hawana cha kuifanya, wanaojitokeza kuhoji wanaishia kutandikwa risasi, kutekwa, kupotezwa na wengine kuishia jela.
Serikali inakiuka sheria ya manunuzi wazi wazi, inabadili matumizi ya bajeti bila woga wowote, imenunua ndege bila idhini ya bunge imekataa kukaguliwa, imejenga uwanja wa ndege wa Chato bila idhini ya bunge imekataa kukaguliwa, imetumia zaidi ya 1.5t nje ya bajeti haitaki kujadiliwa na mengine mengi, sasa imeamua kutoshirikiana kabisa na CAG ili kuendelea kuficha ufisadi inaokusudia kuutenda.
Huu ndio unaitwa kula bila kunawa, awamu ya nne ilikuwa na ufisadi wake lkn ilikuwa na uwezo wa kuji 'defend' bungeni na hata mahakamani. Ila wajue rekodi za CAG huwa hazifutiki kwa kutojadiliwa na bunge zitafufuliwa hata baada ya awamu hii kupita, tuliona ufisadi wa Kiwira na ANBEN uliofanyika wakati wa serikali ya awamu ya Tatu lkn ukaja kujadiliwa awamu ya Nne.