Serikali ya awamu ya Nne angalau ilikula na kunawa, awamu hii inakula waziwazi bila kunawa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Awamu ya nne ya mzee Kikwete tulishuhudia ufisadi mkubwa ukifanyika, tuliona jinsi walivyojigawia pesa za EPA, jinsi walivyochota pesa za Tegeta Escrow, ufisadi wa Meremeta na TANGOLD nk. Lakini angalau ufisadi huo ulikuwa ukijadiliwa bungeni na wawakilishi wa wananchi na serikali kutoa ufafanuzi na mwisho serikali kujivua lawama.

Serikali ya awamu hii ni tofauti, hiyo nafasi ya kujisafisha kupitia bunge haipo tena, serikali imejaa kiburi, haioni sababu ya kuwa please wananchi wake hata kwa kuwadanganya kupitia bunge. inafanya ufisadi nje nje kwa sababu inajua wananchi imewaziba midomo hata kama wakijua hawana cha kuifanya, wanaojitokeza kuhoji wanaishia kutandikwa risasi, kutekwa, kupotezwa na wengine kuishia jela.

Serikali inakiuka sheria ya manunuzi wazi wazi, inabadili matumizi ya bajeti bila woga wowote, imenunua ndege bila idhini ya bunge imekataa kukaguliwa, imejenga uwanja wa ndege wa Chato bila idhini ya bunge imekataa kukaguliwa, imetumia zaidi ya 1.5t nje ya bajeti haitaki kujadiliwa na mengine mengi, sasa imeamua kutoshirikiana kabisa na CAG ili kuendelea kuficha ufisadi inaokusudia kuutenda.

Huu ndio unaitwa kula bila kunawa, awamu ya nne ilikuwa na ufisadi wake lkn ilikuwa na uwezo wa kuji 'defend' bungeni na hata mahakamani. Ila wajue rekodi za CAG huwa hazifutiki kwa kutojadiliwa na bunge zitafufuliwa hata baada ya awamu hii kupita, tuliona ufisadi wa Kiwira na ANBEN uliofanyika wakati wa serikali ya awamu ya Tatu lkn ukaja kujadiliwa awamu ya Nne.
 
Awamu ya 4 ilikuwa na madhaifu yake ikiwemo kutozuia huo ufisadi lakini watu waliishi kwa furaha.

Ila hii ya Jiwe Mungu ndio anajua tunakoelekea
 
Enzi za JK watu walikuwa wanapiga bila UBABE, Procedures zote zilikuwa zinafuatwa ila madudu yalikuwa mengi ndio kama yale Jezi Moja ya Kijana aliuzwa kwa Laki moja lakini utaratibu umefuatwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka ukaguzi wa halmashauri moja mahesabu yalionyesha ndizi moja ilinunuliwa kati ya elfu 5 na elfu 7, lkn utaratibu wote ulifuatwa na signature zote zilikuwepo, huo ndio wizi wa akili bila kutumia nguvu wala ubabe.
 
Teh teh sasa mbona sasa mlimuita dhaifu? Hahahahha

Ndio alikuwa dhaifu kwa kuwa alishindwa kuwakabili wezi waliofichuliwa na taasisi huru alizoziweka kama BUNGE, MEDIA, TAKUKURU na CAG.

Jiwe yeye kaona badala ya kudhibiti Rushwa na ufisadi, yeye kadhibiti TAASISI ZOTE ZINAZOFICHUA na KUDHIBITI Rushwa na UFISADI kama BUNGE, CAG, MEDIA, Opposition na TAKUKURU.

Anachota na kutafuna bila KELELE.
 
Uwizi ni uwizi tu iwe wa kutumia kalamu au bunduki wote ni wahalifu tu hamna mwenye afadhali hapo.
 
Ni aibu kubwa sana kwa nchi , nimeona mahali wadau wa nchi za nje wakiipuuza kabisa Tanzania , haimo tena kwenye group la nchi zinazoheshimika
 
Ndio alikuwa dhaifu kwa kuwa alishindwa kuwakabili wezi waliofichuliwa na taasisi huru alizoziweka kama BUNGE, MEDIA, TAKUKURU na CAG.

Jiwe yeye kaona badala ya kudhibiti Rushwa na ufisadi, yeye kadhibiti TAASISI ZOTE ZINAZOFICHUA na KUDHIBITI Rushwa na UFISADI kama BUNGE, CAG, MEDIA, Opposition na TAKUKURU.

Anachota na kutafuna bila KELELE.

Nimemsiki Msiba kuhusu NSSF miradi miwili tu nikachoka kabisa. Mzee Ruksa alikuja na Azimio la Zanzibar kuonesha kufuta lile la Arusha la Nyerere.

NSSF wakaja na mradi wa nyumba Azimio kulipizia zile nyumba Nyerere alizo zitaifisha kwa kuongezea zero kwenye gharama. Mfano ni manunuzi ya ardhi eti Tanzania ekari moja Dege kigamboni 800,000,000/- Arusha ekari moja 1,400,000,000/- angalia sifuri hizo zililivyotumika kulipizia ule utaifishaji. Na mradi ukaitwa Azimio ili kumkebehi Nyerere kuendeleza kilicho anzishwa kule Zanzibar.

Sasa hujuma za kuhujumu awamu ya 5 ziko njenje kwa kila mtu kuona. Washika dau wa hujuma hizo jiongeze haihitaji akili nyingi.
 
Kama walivyowahi kusema Zitto na Lissu, huu ni utawala wa kishamba sana kuwahi kutokea, wanaiona hazina kama ya ukoo hawajui hesabu huwa hazijifichi, kuna siku Tanzania itakuja kupata kiongozi kichaa zaidi yao akaamua kufukua makaburi yote.
 
Nimemsiki Msiba kuhusu NSSF miradi miwili tu nikachoka kabisa. Mzee Ruksa alikuja na Azimio la Zanzibar kuonesha kufuta lile la Arusha la Nyerere.

NSSF wakaja na mradi wa nyumba Azimio kulipizia zile nyumba Nyerere alizo zitaifisha kwa kuongezea zero kwenye gharama. Mfano ni manunuzi ya ardhi eti Tanzania ekari moja Dege kigamboni 800,000,000/- Arusha ekari moja 1,400,000,000/- angalia sifuri hizo zililivyotumika kulipizia ule utaifishaji. Na mradi ukaitwa Azimio ili kumkebehi Nyerere kuendeleza kilicho anzishwa kule Zanzibar.

Sasa hujuma za kuhujumu awamu ya 5 ziko njenje kwa kila mtu kuona. Washika dau wa hujuma hizo jiongeze haihitaji akili nyingi.
Halafu ukiangalia ukweli halisi,ni kipindi cha Dau na huyu Assad pale nssf ndio Zitto alikuwa top kimapato hadi kufikia kuwa mbunge pekee aliyekuwa anatumia HUMMER !,gari la bei mbaya kabisa kwa viwango vya mapato na mshahara wa mbunge.

Lakini kwa ajili ya kuwa mweyekiti wa ile kamati inayohusika na NSSF ,ndio ilikuwa kipindi cha mavuno na ndio kipindi pia Zitto alipokwapua zile 360mlns.kwenye ule mradi fake wa LEKADUTIGITE !!.

Na ikumbukwe kuwa Assad ni mmoja wa wasimamizi wa ndoa mojawapo ya ZITTO iliyofungwa kiislam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ludicrous
Wamenunua, ndege, wamenenga uwanja wa ndege chato, wamefanya mambo nje ya budget! Well and good,

Kikwete EPA zimeliwa, Tegeta Escrow zimeliwa, Tangold zimeliwa, kodi zimeliwa, huoni tofauti? Unalinganisha Mwizi na .......?
Kikwete alikuwa mwizi

Huyu ana ubabe lakini tunaona mambo,
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom