Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Naibu Waziri – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Dkt. Mary Mwanjelwa amesema watumishi wa umma 4,160 kati 15,189 walioondolewa kazini kwa kuwa na vyeti vya kughushi wamerudishwa.
Dkt. Mwanjelwa amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwa Watumishi hao waliondolewa kimakosa.
====
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa amesema watumishi 4,160 walioondolewa katika mchakato wa kuwaondoa wenye vyeti feki wamebainika kuondolewa kimakosa au kwa uonevu na wamerejeshwa kazini.
Dk Mwanjelwa aliyasema hayo bungeni jana wakati wa kujibu swali la Mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Manyinyi (CCM) na kuongeza kuwa kati ya watumishi waliorejeshwa kazini, watumishi 3,057 ni watendaji wa vijiji, mtaa na kata.
Katika swali lake, Manyinyi alisema serikali katika kuhakikisha inapata watumishi bora wenye sifa, iliamua kuwaondoa watumishi wasio na sifa pamoja na wenye vyeti feki, hivyo alitaka kujua ni kwanini serikali isiunde timu maalumu ili ipitie kila halmashauri kupitia taarifa juu ya zoezi hilo ili haki itendeke hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kwenda wizarani.
Pia alitaka kujua kama serikali haioni kuwa watumishi waliojiendeleza kielimu zaidi ya darasa la saba na wameondolewa kwa kosa la udanganyifu kuwa ni bora kuliko ambao hawajajiendeleza. Akijibu maswali hayo, Dk Mwanjelwa alisema katika zoezi hilo watumishi 15,189 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mshahara.
Alisema baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi na vyanzo vingine kuhusu watumishi kuondolewa kimakosa au kwa uonevu katika orodha ya mishahara, serikali imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa karibu ikiwa ni pamoja na kuunda timu za ufuatiliaji wa utekelezaji wa zoezi hilo.
PIA, SOMA:
- Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi