Serikali: Uchomaji wa Matofali kwa kutumia kuni marufuku

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali imepiga marufuku uchomaji matofali kwa njia ya tanuri kwa kutumia nishati ya kuni hasa katika maeneo ya mijini na badala yake imewataka wachomaji hao watumie pumba kama nishati mbadala.

Onyo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu wakati alipozungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita ikiwa ni ziara yake kwanza ya kikazi kwa mikoa ya kaskazini magharibi tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Kanyasu alisema uchomaji matofali kwa kutumia nishati ya kuni umekuwa ukichangia upotevu mkubwa wa misitu hali inayotishia sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa.

Alifafanua kuwa matofali yachomwe kwa kutumia pumba za mazao badala ya kuni hali itakayosababisha kunusuru nchi kuwa jangwa huku akiagiza kamati hiyo ya mkoa huo kuanza kulisimamia agizo hilo mara moja.

Alisema sehemu kubwa ya nchi kwa sasa uharibifu wa mazingira umeongezeka kutokana na ukataji miti ovyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa matofali kwa kutumia kuni.

“Mimi sipo tayari kuona nchi inageuka kuwa jangwa, ni lazima nisimamie kwa kuanza katika maeneo ya mjini ikiwemo Geita ambapo unakutana na tanuri za kuchoma matofali kwa kutumia kuni, hili sikubaliani nalo,” alisisitiza.

Alisema kwa mujibu wa takwimu, Tanzania imekuwa ikipoteza zaidi ya hekta 372,000 za misitu kila mwaka. Katika hatua nyingine, Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ihakikishe inasimamia ipasavyo mipaka mipya ya baadhi ya misitu ya hifadhi mkoani Geita ambayo imehaulishwa kwa kuhakikisha imetangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

Aidha, ameutaka uongozi wa mkoa huo kutii agizo lilitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alilolitoa mwaka jana la kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka, kwa kulitekeleza ipasavyo.
 
Udongo wa huko mzuri sana kuchoma nyumba inakuwa njema.
Kuna siku tutaambiwa kuchoma kwa gesi tofali.
Watu hali ya chini ndo njia rahisi kupata nyumba bora, cement kidogo tu kujengea
 
Serikali imepiga marufuku uchomaji matofali kwa njia ya tanuri kwa kutumia nishati ya kuni hasa katika maeneo ya mijini na badala yake imewataka wachomaji hao watumie pumba kama nishati mbadala.

Onyo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu wakati alipozungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita ikiwa ni ziara yake kwanza ya kikazi kwa mikoa ya kaskazini magharibi tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Kanyasu alisema uchomaji matofali kwa kutumia nishati ya kuni umekuwa ukichangia upotevu mkubwa wa misitu hali inayotishia sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa.

Alifafanua kuwa matofali yachomwe kwa kutumia pumba za mazao badala ya kuni hali itakayosababisha kunusuru nchi kuwa jangwa huku akiagiza kamati hiyo ya mkoa huo kuanza kulisimamia agizo hilo mara moja.

Alisema sehemu kubwa ya nchi kwa sasa uharibifu wa mazingira umeongezeka kutokana na ukataji miti ovyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa matofali kwa kutumia kuni.

“Mimi sipo tayari kuona nchi inageuka kuwa jangwa, ni lazima nisimamie kwa kuanza katika maeneo ya mjini ikiwemo Geita ambapo unakutana na tanuri za kuchoma matofali kwa kutumia kuni, hili sikubaliani nalo,” alisisitiza.

Alisema kwa mujibu wa takwimu, Tanzania imekuwa ikipoteza zaidi ya hekta 372,000 za misitu kila mwaka. Katika hatua nyingine, Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ihakikishe inasimamia ipasavyo mipaka mipya ya baadhi ya misitu ya hifadhi mkoani Geita ambayo imehaulishwa kwa kuhakikisha imetangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

Aidha, ameutaka uongozi wa mkoa huo kutii agizo lilitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alilolitoa mwaka jana la kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka, kwa kulitekeleza ipasavyo.
Pumba za mazao hupatikana wakati wa mavuno, sasa sijui wanahakikishiwaje upatikanaji wa pumba muda wote wenye matanuri ya kuchoma matofali!!?
 
Hivi yule waziri wa mazingira hasikiki akikemea uharibifu wa mazingira
 
Back
Top Bottom