Serikali:tunapenda kujua hatma ya wale ''tuner-fish'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali:tunapenda kujua hatma ya wale ''tuner-fish''

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Teamo, Jul 17, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wengi wetu tulifurahia ''uwingi'' wa tani za wale samaki gharama kabisa duniani ''tuna-fish'' waliokutwa kwenye meli ya wa-asia.

  Wengi wetu huenda tulimfurahia sana magufuli kwa kile tunachoweza kuita ''kazi nzuri'' aliyoifanya

  Wengi wetu pengine tulichekelea sana kuwaona wale waasia kwa luninga wakiburuzwa mahakamani-keki-mahakamani!

  SWALI LANGU SASA:NIni ilikuwa hatma/suluhisho la serikali:
  -wale samaki walikwenda wapi baada ya kuchukuliwa?
  -wale wa-asia kesi yao ni aje ni vipi?

  Ndugu zangu wana jamii nimeuliza hili makusudi tu,kwasababu sitaki kujiongezea hasira au chuki dhidi ya hii serikali na maamuzi yake mengi.Nimeuliza hili ndugu zangu kwa sababu sitaki kuamini kile ninachokihisi

  Mtu mwenye data zozote juu ya hili sakata naomba anitoe dukuduku......
   
  Last edited: Jul 17, 2009
 2. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha Tuna?
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hao hao mzeya!
   
 4. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Swali zuri mkuu, hope raia watatoa data.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapa mkuu wangu, mimi ningependa sana kuelewa nchi yetu tunafanya nini kuhakikisha samaki hao wanazalishwa nchini na kusafirishwa nje kama wanavyofanya hao Wa ASIA..Tuna fish wana soko kubwa dunia nzima yaani naweza sema soko lake ni kubwa kuliko samaki yeyote.. sisi kina Uchumi Tunao Tunaukali.( UTUTU) . kaazi yetu ni sawa na yule nyoka wa mdimuni, kugonga watu wanaukuja chuma wakati hatuli ndimu hizo..
  Lini sisi tutaondoka ktk fuko hili la umaskini wa akili?.. Wa asia wanakuja nchini kuchua samaki madini na kadhalika kuelepeka China (Hong Kong) sisi tunashindwa kipi kuwawezesha wananchi waifanye biashara hizo hizo kisheria.
  Leo hii nchi imejaa matapeli wa kila aina kwa sababu wanajua fika wananchi wetu hawawezi kufikkisha mzigo yaani tumepata bahati wanunuzi (walanguzi) wanakuja hadi nchini bado hatujashtuka wakati hizi sii biashara haramu.
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hao "Tuner" lol nina uhakika watu wameshakula dili, nilikuwa naangalia kwenye habari (CNN) samaki mmoja anafika hadi $1000! kwenye soko la Japani. Sasa hapo unafikiri wazee wetu wa 20% watazubaa?!!?
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  GT kwani umesikia kitu gani? ...hili suala zuri sana ambalo jibu lake sidhani kama ni jepesi kupatikana.
  samaki wameenda wapi?
   
 8. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Samaki bado wamehifadhiwa katika kampuni ya Bahari Foods wakisubiri amri ya mahakama kuu wapigwe mnada. Kesi ipo mahakama ya Kisutu lakini inatakiwa kuamishiwa mahakama kuu ndio maana amri ya mwanzo ya mahakama ya kisutu ya kuuza wale samaki imesimamishwa.
  Wale waasi wanataka kupewa dhamana na mahakama imeamuru meli yao ifanyiwe valuation ili itumike kuwadhamini wale waasia.
   
 9. R

  Rayase Member

  #9
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  jamaii tatizo langu me ni mahakama mpaka leo wameshindwa kutoa maamuzi kesi inaendelea na storage charges zinaongezeka! Me nadhan wanasheria waanze kuendezesha kesi kibiashara zaidi manake mpake kesi iishe hasara inaweza kuwa kubwa kuliko! Nadhani kuna haja ya kufikilia namna ya kuwasaidia mahakimu na mfumo wetu wa mahakama hapa kwetu! There is a problem ktk uchunguzi!
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mpaka kukamatwa kwa hao Tuna serikali haijafanya lolote wanaoza tu bora wagawe ferry pale kila mlalahoi anunue kwa bei ya kutupwa.
  Kingine licha kuonekana hao samaki wapo kwa wiki kwenye mipaka yetu baharini serikali inaendelea na uvivu wake ule ule wa karne hadi karne imeshindwa kujitengenezea mazingira ya soko wa hii bidhaa adimu duniani wamebaki kusinzia si bora waachie tu hao wavuvi haramu maana mnawashikilia samaki wanazaliana kwa wingi mnashindwa hata kupanga mikakati endelevu ya kuvuna samaki aina hiyo sasa hii ni nini?
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  kwa nijuavyo tangu siku zile wanapakua samaki .....ni kwamba magufuli alisema wana majokofu yenye uwezo wa kuhifadhi hao samaki kwa more than 10 yrs,sasa tukiamni kwamba wamehifadhiwa...ukishapita mwaka mmoja tu,nobody will ask for that...kwahiyo itakuwa diloi lao,itz better tujue what nex there..........
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Vichekesho nchi hii, kwanza tujiulize serikali ilitaka kuachieve kitu gani kwa kukamata meli ile na shehena yake. Meli imeshikwa haifanyi kazi na inaharibika bandarini shauri ya sea corrosion, samaki wapo sehemu ambapo storage charges ni kubwa kuliko kawaida mabaharia wako ndani muda wote toka meli iliposhikwa.

  Mpaka hapo utaona serikali yetu ina liabilities tatu meli kuharibika kwa kutotumika, samaki kuhifadhiwa kwa gharama kubwa na kuwanyima uhuru mabaharia wa meli hiyo.

  Chukua scenario hii upande wa mashtaka unashindwa kuthibitisha kesi na mabaharia wanachiwa, mwenye meli atafungua kesi dhidi ya serikali kudai fidia ya loss of business, kuharibika meli, kuharibika bidhaa zake. Mabaria nao wanaweza kufungua madai kwa kufunguliwa kesi isivyo halali. In that situation serikali italipa kiasi kikubwa sana, na hatutaachive kitu apart from international reputation.

  Walipa kodi tusiombee hiyo scenaio itokee we will pay through our noses.
   
Loading...