Serikali: Tunafuatilia suala la Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini kuzuia ndege ya ATCL. Ni kufuatia Hermanus P. Steyn kufungua shauri

Itaachiwa Muda Siyo Mrefu Sana
Tupo Kwenye Light Track
Hao Watashindwa Mabeberu
 
Nafikri mwenyeki wa SADC aingilie kati.hatuwezi kuwa tunashirikiana na mwafrica mjinga.Mnasema eti mahakama ziwe huru but consultation ingeweza kufanyika kabla yakutoa maamuzi ambayo yanaumiza mwenzako!!
 
HOME OF PURE FACTS & FREE EDUCATION: ...KWANINI NDEGE YETU AIRBUS INASHIKILIWA HUKO SOUTH AFRICA? ....FACTS are Wakati wa Utawala wa Awamu ya Kwanza Mzungu Hermanus Steyn alitaifishiwa Mali zake nyingi hapa Nchini akakimbilia Ulaya na kufungua kesi against Serikali ya Awamu ya Kwanza na Mahakama ikaamua Serikali ya Awamu ya Kwanza imlipe Mzungu huyo Fidia ya Mali zake jumla ya USD $36M ....Mzungu hakulipwa pesa zake lakini Mwaka 1994 Mahakama ilikumbusha Serikali yetu kumlipa Mzungu huyo yakafanyika mazungumzo marefu nje ya Mahakama na Mzungu akakubali kupunguza malipo kutoka USD $ 36M mpaka USD $ 30M ....Mwaka 2012 kwa mara ya kwanza Seeikali yetu ilimlipa Mzungu huyo jumla ya USD $ 20M zikawa zimebakia USD $ 10M ambazo kwa sababu zisizojulikana ni majuzi tu ndio Serikali ya sasa IMEGUNDUA KWAMBA ALIKUWA BADO HAJALIPWA .....baada ya Mzungu huyo kufungua kesi mpya huko South Africa akidai malipo yake hayo ya toka Awamu ya Kwanza ....Cha kusikitisha sana ni kwamba THE FACTS are Mzungu huyu Styein mwenye umri wa Miaka 76 sasa hivi KWENYE HII KESI HUKO SOUTH AFRICA ANAWAKILISHWA NA MWANASHERIA MTANZANIA MWENZETU KUTOKA MOSHI (JINA NALIHIFADHI KWA LEO) katika kulishitaki Taifa letu huko ugenini ....Mazungumzo ya KISHERIA na KIDIPLOMASIA baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanaendelea sasa hivi ili kulitatua tatizo hili dogo sana na la muda mrefu na Serikali ya Awamu hii imeamua kulivalia njuga tatizo hili baada ya kuligundua majuzi na soon ndege yetu itaruhusiwa kuendelea na kazi zake! ...MUNGU AIBARIKI TANZANIA! VIVA MAGUFULI! KANYAGA TWENDE TUMECHELEWA SANA! KANYAGA! and THIS CASE IS CLOSED! - @lemutuz_superbrand
 
Very cheap politics.

Anyways tuchukulie ni kweli basi, kwann sasa hamumlipi babu wa watu. Kwani serekali yetu sio majambazi, we Mobimba huyo babu mwenzio unashauri angefanya nini zaidi ya kwenda mahakamani, na mahakama ingefanyann zaidi ya kukazia hukumu?

Hivi unahisi huyo babu mwenzio kakosa kabisa mawakili dunia nzima Hadi achukue wakili mTz? Na hata kama ni kweli, kazi ya wakili ni kupigania haki sasa unataka mawakili wawe wanachagua wateja hata kama wanajua mtu anadhulumiwa wasimsaidie?

Hata hivyo hapa nahisi we mzee Mobimba unajaribu kuhamisha mjadala kwa kuleta uzwazwa kufunika deni la kweli ambalo nahisi ni mpendwa wetu namba moja alishiriki kutuletea watanzania ili kumziba na kashfa ingine due to kukurupuka
 
Itachiwa hv karibuni kuna beberu mmoja kafungya kesi ya kijinga sana halafu anaemtetea mtz kama wakili hapo ndio utashangaa saaana. Madai yake ya enzi za nyerere yani.
 
Mapambano gani yasiyokuwa na plan unapambana bila kujua unapambania nini na matokea yake ni nini Utatembea zigzag kama unakwepa risasi mpaka lini zama za kubebwa huko hakunaga.Mambo yamenyoooooka kama mstari wa equator mzee.Fahamu
We mwenye plan ya kunyooka, nyooka tu.
Kwa case hii, plan gani unaongelea? Nchi hii tumeshalewa siasa.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ameomba radhi kwa usumbufu ulijitokeza kwa abiria wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) waliokuwa wasafiri kutoka Johannesburg kwenda jijini Dar

Ameomba radhi hiyo kutokana na abiria hao kushindwa kusafiri kutoka uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg baada ya ndege hiyo kushindwa kufanya safari kama ilivyopangwa kutokana na kuzuiwa

Kwa mujibu wa taarifa ambayo Serikali imepokea, ndege hiyo imezuiwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafuatilia ili ndege iachiwe

View attachment 1188590
DAWA YA MOTO NI MOTO. WAKAMATE NAO ZILE BOEING 737 ZINAZOFANYA SAFARI KATI YA DAR NA JOHANNESBURG.
 
Tovuti ya eturbonews imeripoti kuwa ndege ya Tanzania inashikiliwa kutokana na deni TZS 9.272 bilioni ambalo Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) linaidai Tanzania (ATCL), lililotokana na mkopo lililoutoa kutokana na na makubaliano ya kibiashara waliyoingia mwaka 2002.

Hata hivyo Tanzania ilivunja mkataba huo mwaka 2006 kutokana na kupata hasara, hatua iliyopeleka SAA kuuza hisa zake 49% ilizokuwa inamiliki ndani ya Shirika la Ndege la Tanzania.

SAA ilienda mahakama ikitaka mahakama iiamuru ATCL kulipa deni hilo.
FB_IMG_1566650747564.jpg
 
Sababu Za ndege hiyo kukamatwa Bado hazijawekwa wazi. Tusianze kuhukumu kabla ya kujua chanzo ni nini? Tusifikirie kuliombea taifa mabaya. Lets Advise each other guys.
 
Kwa hiyo kitu kimenyakwa hapo Oliver Tambo dawa ya deni ni kulipa.
NdoroboAir the Wings of Burigi.
 
Back
Top Bottom