Serikali: Tumeshagawa milioni 50 kila kijiji kama tulivyoahidi kwenye Kampeni 2015

Serikali kupitia msemaji wake, Hassan Abbas imesema imeshagawa milioni 50 kila kijiji kama ilivyoahidi kwenye kampeni za mwaka 2015

Milioni hizo 50 kila kijiji zimetolewa kupitia elimu bure na ujenzi wa fly over


Basi sawa
 
Kwani kuna mtu na akili timamu kabisa, aliamini ipo siku serikali itagawa fedha kila kijiji kama walivyo danganya kwenye kampuni?
By the way, umaskini kamwe hauondoki kwa kumgawia fedha maskini
 
Haya ya dhahiri shahiri yanayonekana tu mnatudanganya je yaliyojificha? Asante msemaji wa serikal kwa kutudanganya
 
Kweli hii ni hatua kubwa sana tumepiga, fly over kila kijiji Mungu atupe nini tena, teh teeehe
 
Hii sasa ishakuwa serikali ya kimzaha, usanii na kudharau wananchi huku ikilazimisha kusifiwa kwa mauzauza yake....amesahau na bomba-dear nazo no ndani ya milioni hamsini kwa kila kijiji...sasa waliposema kuwa zitakopeshwa kwa vikundi vilivyosajiliwa walikuwa na maama gani.....viongozi hawa kwa kweli wanatakiwa wakapimwe mikojo kwa haraka kabla hawazidi kuchefua watu kwa matamko yao.
 
Back
Top Bottom