Serikali tumbueni viongozi wa BAKWATA

Serikali tumbueni viongozi wa BAKWATA

Tatizo ni serikali, hao wanaunda kalenda ya kila mwaka ambayo inaonesha siku fulani ni ya mapumziko. Hadi sikukuu za kiislamu wanazikadiria hivyo, pasipo kufuata sheria za dini husika.

Walipoona hilo suala la kalenda kuwa linaingiwa na ugumu, ndipo wanapowatumia BAKWATA ilimradi kupindisha ukweli kwa manufaa ya kisiasa.

BAKWATA haikuwahi kuanzishwa na mwislamu, limeanzishwa kwa kuvunjwa jumuiya halisi ya kiislamu kimabavu. Usitarajie litakuwa kwa manufaa ya waislamu, na kuacha maslahi yaliyopelekea kuanzishwa kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kWA hawa watu, kutofautiana ni jambo la kawaida
 
Hivi unaelewa kweli kuhusu masuala ya dini au umejibu kwa kukurupuka? Mtume Swallallahu alayhi wasalaam amesema tufunge siku ya Arafa(ni siku ambayo mahujaji wapo katika viwanja vya Arafa) na siku ya pili yake ni sikukuu, Sikukuu hii inafungamana na ibada ya hijja inayofanywa sehemu moja ulimwenguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole Sana
 
Kwani, sababu ya/za kufunga siku ya Arafa ni zipi?

Na je, inawajibika kufunga siku ya Arafa kwa kuangalia wenzetu wanaosimama Arafa? Au tufuate mwezi kwa maana ni siku inayojitegemea ipo mahususi ndani ndani ya mwezi huu kwamba ni ibada/ funga inayojitegemea kwa kufuata masiku yake ya mwezi pasipo kuangalia mahujjaji wanafanyaje?

Swali jengine, kuna yamu tashrik;ni masiku matatu,katika haya masiku inawajibika kusali siku yoyote hii Eid adh'ha?

Lengo ni kutaka kufahamu.

Dharra, massoud
 
Swaumu ya Arafa inafungamana na wale walioko kwenye kisimamo cha arafa na si vingnevyo.Na baada ya Arafa kinachofuta ni idd ya kuchinja na vingnevyo .haikuwah kutokea kipnd cha mtume kwamba leo Arafa halafu keshokutwa idd!!!!!!!!!. Na jua hakuna nchi yoyote duniani inayotofautiana na nchi nyingne kwa masaa 24 .

Kwa vyovyote kuna baadhi ya masaa yata match na yale ya mchana wa Arafa kwa nchi ya Saudia Arabia. Mfano waweza ukakuta Marekani ni saa Moja Asubuhi lakini Saudia Arabia ni Saa Tisa Jioni(bado ni mchana wa arafa), au Kuna nchi ambazo zinaitangulia saudia masaa , Lakini mpaka wnamaliza mfungo wao lazima kisimamo cha Arafa kitakuwa kimeshaanza huko Saudia .N.K
 
Bakwata maana ya bakwata. In baraza kuu LA waislam kila muislam anatakiwa kuitambua bakwata na si vinginevyo haijalishi uko dhebu lipi LA kiislam. na imesajiliwa kwa kisheria ya Baraza ufahamu si kitu cha kukikejeri na wiisla anaagiza utiifu kwa uongozi. Ulichosema kinachojiita bakwata sioni kama uko sahihi. Isiwe nakosea labda uko tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani BAKWATA viongozi wanateuliwa na serikali?
 
Swaumu ya Arafa inafungamana na wale walioko kwenye kisimamo cha arafa na si vingnevyo.Na baada ya Arafa kinachofuta ni idd ya kuchinja na vingnevyo .haikuwah kutokea kipnd cha mtume kwamba leo Arafa halafu keshokutwa idd!!!!!!!!!. Na jua hakuna nchi yoyote duniani inayotofautiana na nchi nyingne kwa masaa 24 .

Kwa vyovyote kuna baadhi ya masaa yata match na yale ya mchana wa Arafa kwa nchi ya Saudia Arabia. Mfano waweza ukakuta Marekani ni saa Moja Asubuhi lakini Saudia Arabia ni Saa Tisa Jioni(bado ni mchana wa arafa), au Kuna nchi ambazo zinaitangulia saudia masaa , Lakini mpaka wnamaliza mfungo wao lazima kisimamo cha Arafa kitakuwa kimeshaanza huko Saudia .N.K
Ayna Dalili? Nipatie dalili( ushahidi) ili nikiulizwa na mimi niwe na la kujibu.

Kingine kuna sababu za Arafa kufunga. Kwenye hizo sababu ndipo hoja mbalimbali zinaibuka, na ndipo zinazoibuka Asbab za kufunga Arafa hazifungamani na kisimamo cha Arafa. Binafsi mwisho wangu wa kufunga ni Leo.

Nataka kufahamu hayo mambo yanakuaje
 
Sioni tatizo hapo umeharakisha tu kupanick na unajua kabisa Eid inategemea mwezi so unadhani ikiwa j4 watashindwa kutangaza..?
Sometimes sio lazima ufate wenzako pengine mwezi ukaandama j5 bakwata ndo wakawa na makadirio sahihi
Aihusiani na mwezi (moon)
 
Kwa mujibu wa taasisi inayojiita Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, siku ya Jumatano ndiyo ya Umul Eid el Hajj.

Mimi binafsi nimeshindwa kujua kwanini siku hii imekuwa tofauti na mataifa mengine ya Afrika Mashariki kama Kenya na Uganda. Ikumbukwe kuwa itikadi ya BAKWATA ni kuwa sambamba na Kenya na Uganda haswa kwa ishu za mwandamo wa mwezi. Sasa imekuwaje safari hii BAKWATA imeamua kuiarifu Serikali kuwa sikukuu ya Eid el Hajj ni Jumatano wakati kwa wenzetu wa Kenya na Uganda ni siku ya Jumanne ya tarehe 21 Agosti?

Na sio Kenya na uganda tu bali ni karibu mataifa yote ya dunia. Swali langu ni kwa hao masheikh wa BAKWATA; ina maana hao ndio wajuzi saana wa kutafsiri hadith pamoja Quran kuliko masheikh wa hayo mataifa mengine?

Kwa hili ndio maana nimeona ni vyema Serikali ikaamua kuutumbua uongozi wa BAKWATA kwani inaonekana wanatumia visivyo nafasi ya kusikilizwa na Serikali. Lingine BAKWATA ifahamu kuwa haitaweza kuwadanganya waislam wote wa Tanzania kwa wakati wote.

View attachment 842225View attachment 842226

Sent using Jamii Forums mobile app
Huna haja ya kuumiza kichwa.
Dawa nikuwaachia hilo li Iddi lao ya J5 wasali peke yao Siku nyingine watatia akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAKWATA BAKWATA BAKWATA.ukiangalia vizuri viongozi wao wamesoma elimu ya dini vizuri ila wanapindisha ukweli kwa maslahi ya dunia.wataenda kujibu vizuri kwa mola wao.leo tareh 20 mahujaji wapo ktk viwanja vya arafa na leo sisi wengine tunapaswa kufunga tusiokwenda huko maka.na kesho tarehe 21 ni iddi ya kuchinja hii ni kwatalatibu na mafundisho ya mtume wetu.

ila hawa waliochukua jukumu la kuongoza hii taasisi kwa makusudi yao bila izini ya mola wao wamepanga wafunge kesho tareh21 na iddi yao itafanyika tareh 22 kwamafundisho yao wenyewe siyo ya mtume MUHAMMAD(SAW) hao ndio BAKWATA.
Kitu cha kusikitisha zaidi TZ ndio itakuwa nchi pekee Duniani kusali Iddi Siku ya J5.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zipo karenda za kiislam zinaonesha na mwezi pia lkn kuu ni arafa ndo inatoa tasmin halisi idd ya kuchinja ni lini

Uliza mahujaji wanasimama arafa lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom