loosimingori
JF-Expert Member
- Oct 30, 2017
- 920
- 1,146
Kwa mujibu wa taasisi inayojiita Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, siku ya Jumatano ndiyo ya Umul Eid el Hajj.
Mimi binafsi nimeshindwa kujua kwanini siku hii imekuwa tofauti na mataifa mengine ya Afrika Mashariki kama Kenya na Uganda. Ikumbukwe kuwa itikadi ya BAKWATA ni kuwa sambamba na Kenya na Uganda haswa kwa ishu za mwandamo wa mwezi. Sasa imekuwaje safari hii BAKWATA imeamua kuiarifu Serikali kuwa sikukuu ya Eid el Hajj ni Jumatano wakati kwa wenzetu wa Kenya na Uganda ni siku ya Jumanne ya tarehe 21 Agosti?
Na sio Kenya na uganda tu bali ni karibu mataifa yote ya dunia. Swali langu ni kwa hao masheikh wa BAKWATA; ina maana hao ndio wajuzi saana wa kutafsiri hadith pamoja Quran kuliko masheikh wa hayo mataifa mengine?
Kwa hili ndio maana nimeona ni vyema Serikali ikaamua kuutumbua uongozi wa BAKWATA kwani inaonekana wanatumia visivyo nafasi ya kusikilizwa na Serikali. Lingine BAKWATA ifahamu kuwa haitaweza kuwadanganya waislam wote wa Tanzania kwa wakati wote.
Sent using Jamii Forums mobile app