Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya

Nderakindo amkana Samuel Sitta; Nderakindo amkana Samuel Sitta - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akisema ofisi yake imewakutanisha na kumaliza mgogoro baina ya wabunge wawili wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), mmoja wa wabunge hao, Dk Nderakindo Kessy amesema hakuna kitu kama hicho.
 
Sasa kilicho mpelekea kulala rumande ni kitu gani? Ai alikosa nyumba ya wageni? Kila kitu hata ambavyo vinaonekana Nyie ni kikanusha tuu. Vijikaratasi vya kufunga maandazi vinaibomoa serikali yaCcm. Aibuuu

Ni wapi serikali imsema alilala rumande? Mtu umeambiwa hakupigana tena kwa tamko la serikali.Sasa kama hakupigana ulitegemea serikali ya Kenya imuweke rumande?
 
Ni wapi serikali imsema alilala rumande? Mtu umeambiwa hakupigana tena kwa tamko la serikali.Sasa kama hakupigana ulitegemea serikali ya Kenya imuweke rumande?

Wewe mtetee tu...

 
alipinga hoja ya suala la ardhi kuwa la Afrika Mashariki na siyo nchi washirika, na mpaka leo ni hivyo. Mkenya hawezi kuja kumiliki eneo huku Bongo, ila anaweza kulitumia kwa shughuli za kiuchumi tu na ni kwa mda maalum tu! Hivyo basi nampongeza sana mama huyu, anaweka maslahi ya taifa mbele halafu ya EAC baadaye!
 

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy

Serikali imetoa kauli bungeni, ikisema Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji, hakumpiga Mbunge mwenzake Nderakindo Kessy (pichani), bali Bunge hilo lina mgogoro ambao, kiini chake ni Spika wa Bunge hilo,Magreth Zziwa.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akitoa taarifa bungeni baada ya Khatib Said Haji (Konde-CUF), kuomba mwongozo wa Spika, kuhusu kinachoendelea kwenye Bunge hilo.

Sitta alisema: "Kinachotokea katika AELA kwa kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa Spika mwenyewe, ndiye chanzo cha matatizo mengi ambayo yamegawa bunge hilo katika makundi makuu mawili."

Alitaja makundi hayo kuwa ni linalotaka spika huyo aondolewe kwa madai kwamba hafai, huku lingine likimtetea abaki.

Alisema Tanzania inaonekana kuwa kikwazo katika mkakati wa kumuondoa Zziwa.

Alisema ili Bunge hilo liamue jambo lolote, lazima akidi ipatikane katika kila nchi na kwamba awali Tanzania waliunga mkono aondolewe, lakini sasa, wamekuwa na msimamo tofauti na kusababisha kuwapo aina fulani ya chuki.

"Kilichotokea kati ya Bhanji na Kessy, siyo kinavyoelezwa kwani Bhanji anahesabika kuwa ni shabiki mkubwa wa Spika, kiasi cha wenzake kumuona kama kibaraka vile," alieleza Sitta.

Alielezea kuwa madai ya Kessy kupigwa yalitokana na Bhanji kugongana naye kwa bahati mbaya wakati akiwahi usafiri, akipita katikati ya wabunge wenzake,Alisema mgongano huo ulitafsiriwa na Kessy kuwa ni shambulio, ambaye alihamaki na kwa kusaidiwa na baadhi ya Wabunge wa Uganda, akaenda polisi na kumtuhumu Bhanji kwamba amemtendea kosa la jinai.

Alisema hata hivyo, kwa jitihada za uongozi wa EALA, mpaka jana suala hilo halimo mikononi mwa polisi tena bali limemalizwa ndani ya Bunge.

Sitta alizungumzia madai mengine dhidi ya Shyrose kwamba alifanya mambo ya ‘ovyo' takriban miezi miwili iliyopita kwamba bado yapo mikononi mwa Tume ya EALA, itakapomaliza kulishughulikia litatolewa taarifa.

"Kwa sasa hatuwezi kufanya lolote, mpaka tutakapopata taarifa kutoka EALA, nikizipata nitaziwasilisha kwa Spika wetu na hapo ndipo sisi kama jimbo la uchaguzi tutakapojadili kuona ukweli ni upi na kuamua hatua za kuchukua," alieleza Sitta.

Chanzo
:Nipashe
 
Hiyo hoja haiwezi kuzuia mtu anaetaka kumiliki ardhi ashindwe, wapo wengi tu wamenunua ardhi kwa pesa zao na wamejenga mpaka hoteli huko meserani Arusha tunawajua, ukiwa na hela nchi hii hakuna kinachoshindikana, mradi watanzania hatuna vitambulisho, na ukinunua ardhi huulizwi umezaliwa wapi.
 
Kwa nini kila siku anasemwa Shyrose Bhanji na sio wabunge wengine kutoka Tanzania. Mimi ninaamini kuna tatizo hapo japo wakubwa wanalitetea.
 

Mimi sio Pro SHYROSE... Lakini hapo inaonyesha hawa Wabunge wa nchi JIRANI i.e UGANDA; RWANDA; KENYA wanatafuta sababu za kutuondolea Umoja wetu...

Ni Wabunge 7 tu kati ya 9 wa TANZANIA ndio wanaomkubali Madame Speaker.. Sasa wanatafuta visa kuwachafua baadhi na wanaona SHYROSE being not 100% ndio wa ku attach hana nguvu... hawakujua kuwa Tanzania NYERERE alituelimisha BILA MATABAKA kama hizo nchi zao...
 
Kwa nini kila siku anasemwa Shyrose Bhanji na sio wabunge wengine kutoka Tanzania. Mimi ninaamini kuna tatizo hapo japo wakubwa wanalitetea.

Hao waafrika wa UGANDA RWANDA na KENYA wana ule UKOLONI kuwa BIAS na ku attach a weakest point yao ni Rangi ya SHYROSE sababu wabunge 7 wa Tanzania wako Upande wa SPEAKER
Shakidinkili
 
Kama unaweza kuwa pigisha kura watu waliokufa utashindwa kuja kuongea utumbo kama huu... Sitta angejikali kimya, ni mtu mzima lakini ni mkosa akili sana, kwa ulaghai aliofanya katika kura za katiba pendekezwa kwa sasa angekuwa ananya debe kwa nchi zenye utawala wa kisheria ... kajishushia sana heshima yake, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kumsiliza huyu ....
 

Kumbe pia alifanya mambo ya hovyo takribani miezi michache iliyopita!Hivi kwa akili ya darasa la kwanza,inakuwaje apite katikati ya wabunge wengine alafu amgonge adui wake?eti alikuwa anawahi usafiri kwa hiyo alikuwa anakimbia?alikuwa anakimbilia hiace?mimi ninaona huyo Shyrose anafaa zaidi kuwa mhudumu wa baha awe anashikwa makalio.
 

Kama hilo halitekelezeki basi siyo kosa lake Shy Rose. Ni uzembe wetu sisi watanzania. Yeye kama mbunge wa Tanzania huko EALA ameshafanya part yake!
 

Wewe personally una evidence kuwa kafanya hayo madudu? au unasikia tu na kulipuka.
 
Ngoja ije ithibitike kuwa alipigana sijui huyu mwendawazimu Sita ataficha wapi uso wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…