Serikali: Shy-Rose hakupigana Kenya

msemakweli

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,627
Reaction score
880
SERIKALI imesema Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shy-Rose Bhanji hajapigana nchini Kenya, na wanasubiri Tume ya EALA ili kujua ukweli wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.

Kwa muda sasa, Shy-Rose amekuwa katika mzozo na wabunge wenzake wa EALA, kwanza akituhumiwa kuwatukana wakiwa safarini Ubelgiji na juzi akituhumiwa kupigana na mwenzake kutoka Tanzania, Dk Nderakindo Kessy.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta awali alilieleza Bunge jana mjini hapa kuwa kiini cha mzozo wote ni mgogoro dhidi ya Spika wa EALA, Margaret Zziwa wa Uganda.

Sitta alisema yapo makundi mawili sasa ndani ya Bunge hilo, moja likitaka kumng'oa Spika huyo na lingine likimkingia kifua kwamba hapaswi kuondolewa.

"Katika hili (la kumng'oa Spika), Tanzania ni kikwazo, kwa sababu ili Spika aondolewe ni lazima akidi itimie, na akidi hiyo ni kupata kuungwa mkono kwa idadi fulani ya wajumbe wa kila nchi. "Sasa Tanzania wamefuta hoja ya kutaka Spika huyo aondolewe na hii ndiyo imesababisha chuki yote," alieleza Sitta kabla ya kujibu hoja kuhusu Shy-Rose.

Sitta alisema Shy-Rose hakupigana au kumpiga mbunge mwenzake kama ilivyoandikwa katika magazeti jana.



Chanzo
:Nipashe
 
SIASA BWANA UONGO HUWA KWELI NA KWELI HUWA UONGO
Ndugu zangu mnaotaka kujiingiza kwenye siasa kigezo cha kwanza ni kutokuwa na soni
 
SERIKALI imesema Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shy-Rose Bhanji hajapigana nchini Kenya, na wanasubiri Tume ya EALA ili kujua ukweli

Sasa wakisema hakupigana(maana yake wana uhakika) na wanasubiri kujua ukweli,(maana yake hawajui kilichotokea), TZ viongozi wanakurupuka sana
 
Kama tanzania imekataa kuungana na wenzao kwa nini kila siku ni shyrose tu? kwani yeye ndio mbunge pekee wa kutoka tanzania? ficheni maovu yenu humu ndani, ila nje yatafichuliwa tu.
 
We bwana mdogo sita,watu hatu iman kabisaaa na hii serikali,hata Mr.tezi dume anajua hilo.
 
Mti wenye maembe ndio unaotupiwa mawe.Shyrose ni jembe.Usifanye mchezo.Ni mbunge anayejua kazi yake.Na hatishwi wala kutetereka.

kwa hiyo kama ni jembe, ndio afanye hayo madudu? au unataka kutuaminisha huwa wanamfuata chumbani na kumpeleka kituo cha polisi? Kama ni jembe hebu nipe hoja moja tu amabayo aliitoa na ikaleta manufaa kwenye nchi hizi za afrika mashariki, isiwe kupinga kila hoja ndio ujasiri tu.
 
SERIKALI imesema Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shy-Rose Bhanji hajapigana nchini Kenya, na wanasubiri Tume ya EALA ili kujua ukweli wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.....
Anasema hakupigana, ila pia anasubiri taarifa kujua ukweli!! Sasa kama anasubiri taarifa, iweje afanye ruling kwamba hakupigana?
 
SERIKALI imesema Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shy-Rose Bhanji hajapigana nchini Kenya, na wanasubiri Tume ya EALA ili kujua ukweli wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.
Ndio umekanusha nini sasa ikiwa hujui na kwamba unasubiri nawe uelezwe na waliokuwepo? Kwanini usisubiri hiyo tume kwanza ndipo uhitimishe? Hata hivyo hii sio habari tena. Habari ya mujini ni Escrow ya Tegeta.
 
Tumtazame kwa umakini Shujaa huyu Shai Rose, isije kuwa ana ushujaa unaowatisha maadui wa Utanzaniauliotukuka kizalendo zaidi. Tumsapoti hadi pale tutakapo dhibitisha kuwa ana kosa.
 
Huyu ndiye mzuri wa kuolewa , unakuwa ufungi milango kwani ni ulinzi tosha, akija mwizi unasema shy, shy shy miji, miji. Mwizi anatimka.
 
Ndio umekanusha nini sasa ikiwa hujui na kwamba unasubiri nawe uelezwe na waliokuwepo? Kwanini usisubiri hiyo tume kwanza ndipo uhitimishe? Hata hivyo hii sio habari tena. Habari ya mujini ni Escrow ya Tegeta.
Mh. Zitto anasema tena bungeni kuwa wizi wa escrow ac unaweza kutokea tu kwenye nchi isiyo na serikali mfano Somalia au Congo DRC. Sasa ni kweli umetokea Tanzania tayari na hiyo serikali iliyosimamia wizi huo ndio inatoa hili 'kanusho' ...unataka kithibitisho gani kuyaamini maneno ya Zitto!?

 
Sasa kilicho mpelekea kulala rumande ni kitu gani? Ai alikosa nyumba ya wageni? Kila kitu hata ambavyo vinaonekana Nyie ni kikanusha tuu. Vijikaratasi vya kufunga maandazi vinaibomoa serikali yaCcm. Aibuuu
 
huyu 6 nae anataka ku2fanya cc wajinga, kasema shy-rose hakupgana, sasa wanasubiri ripot ya nn wakat kasha conclude, duh
 

Mkuu kwenye post yangu sidhani kama niliungana na mkanushaji, na wala sidhani kama nilihitaji uthibitisho zaidi ya kumtaka mkanushaji asubiri taarifa kwanza ndipo afanye ruling. May be you misquoted me Sir.
 
Kila siku ni habari za kukanusha kuhusu matendo ya huyu mbunge!kwa nini yeye tu?

Na kwa nini habari mbaya atupiwe yeye tu? tena na watu wale wale toka Rwanda?
 
The government need to stick on principles rather than favouritism. The statement shows that government stands with Shyrose and it has issued a historic background to support its stance. That tell every one that rule of law, leadership principles and standards are not to be abided by some people. This amount to impunity and rise of "mafia" law in our society
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…