Serikali: Sheria za barabarani kuongezewa makali ili kubabiliana na tatizo la ajali nchini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amesema wizara ipo kwenye mchakato wa kuangalia upya sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuziongezea makali ili kukabiliana na tatizo la ajali nchini

Alisema lengo ni kukabiliana na watumiaji wa vyombo vya moto wakiwamo madereva wa pikipiki ambao wengi wao wamekuwa wakivunja sheria mara kwa mara na kusababisha ajali zinazoweza kuepukika.

Masauni aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akitoa zawadi kwa wanafunzi na shule za msingi zilizoshinda michoro yenye ujumbe wa usalama barabarani visiwani Zanzibar kwa mwaka 2019 katika mafunzo yaliyofadhiwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma na Shule ya Msingi Mkunazini kushika nafasi ya kwanza na kukabidhiwa Sh. milioni nne.

"Ajali za barabarani zimeendelea kupungua siku hadi siku, lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto na hasa waendesha bodaboda wanavunja sana sheria za barabarani hawa tumeshawaundia mkakati.

"Tumeamua atakeyakamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani kwanza awekwe mahabusu na kisha apelekwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Wanavunja sheria kwa kuamini sheria sio kali sana, sasa tumeamua na tutawadhibiti ipasavyo kwa watakaoendelea kutoheshimu sheria zilizopo," Masauni alisema.

Alisema kuna umuhimu jamii ya Watanzania kwa upande wa Bara na Visiwani kuendelea kupatiwa elimu inayohusu usalama barabarani pamoja na matumizi sahihi ya barabara.
"Hivyo nitumie nafasi hii kuipongeza Kampuni ya Puma Tanzania kwa uamuzi wake wa kutoa elimu hii, kwa hapa Zanzibar shule tano za msingi zimepata elimu hiyo na tunaamini itasaidia kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika," Masauni alisema.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma, Dominic Dhanan, alisema programu hiyo ilihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani katika shule za Msingi Mwembeshauri, Kisiwandui, Shule ya Msingi Jang’ombe, Shule ya Msingi Nyerere na Shule ya Msingi Mkunazini.

"Wanafunzi wasiopungua 6,500 wamepata elimu na uchoraji wa michoro inayohamasisha matumizi sahihi ya barabarani na kufuata sheria zilizopo," alisema.

Alisema programu hiyo ya usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka 2013 na zaidi ya shule 80 zimefikiwa na jumla ya wanafunzi 106,500 wamepata mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Ruvuma, Dodoma na sasa visiwani Zanzibar.

Kwa upande wake mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkunazini, Raya Zuberi, ambaye ameibuka mshindi wa kwanza kwa mwaka 2019 kwa kuchora mchoro bora wenye ujumbe wa usalama barabarani Raya Zuberi, aliishukuru Puma kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi atakuwa balozi wa kueleza matumizi sahihi ya alama za barabarani.
 
Tatizo sio madereva, tatizo ni barabara nyembamba sana. Ukiyumba kidogo hata kama uko spidi 40 basi kama sio mtaro basi wewe kichaka ni chako. Ujerumani kwenye autobahns unaendesha spidi yoyote na ajali ni cache kuliko Tanzania. Sababu barabara ni bora na pana. Zinakupa nafasi ya kujinafasi.
 
Alisema lengo ni kukabiliana na watumiaji wa vyombo vya moto wakiwamo madereva wa pikipiki ambao wengi wao wamekuwa wakivunja sheria mara kwa mara na kusababisha ajali zinazoweza kuepukika.
Hili jambo la kuongeza makali ya sharia limepitwa na wakati. Ajali nyingi zinasababishwa na kutokuwepo barabara sahihi. Unapochanganya magari, pikipiki, baiskeli, wanyama na watembea kwa miguu unategemea nini?
 
Hizi passo ict spaxio ukipiga shimo kamekata zlink uko ukichakani wapunguze kodi watu wanunue bmw na dodge.
 
Yaani sikusimama kwenye zebra unamsweka mtu ndani na kumpeleka mahakamani? Mumeona rushwa zimekuwa adimu kwani faini zinipwa kwa mpesa mnakuja na ujinga mwingine, safari hii tunagoma nchi nzima
 
Yaani sikusimama kwenye zebra unamsweka mtu ndani na kumpeleka mahakamani? Mumeona rushwa zimekuwa adimu kwani faini zinipwa kwa mpesa mnakuja na ujinga mwingine, safari hii tunagoma nchi nzima

Goma mwenyewe
 
Unaongelea bmw zipi?

Mbona hizi bmw 3/5/7 series used bei zake ukiitoa japan zinafanana tu na bei za toyota za class hio hio.

Shida ni maintanance cost za bimmer.
Hizi passo ict spaxio ukipiga shimo kamekata zlink uko ukichakani wapunguze kodi watu wanunue bmw na dodge.
 
Back
Top Bottom