Serikali pigeni marufuku pombe nchini

Serikali pigeni marufuku pombe nchini

Africa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
1,504
Reaction score
2,275
Kwakuwa nchi yetu bado changa kiuchumi ni bora Serikali ingepiga marufuku uuzwaji wa pombe nchini ili watu wafanye kazi. Watu wengi wanashindwa kumudu majukumu mbalimbali kutokana na unywaji wa pombe, hivyo hupelekea kutokufika malengo yaliyokusudiwa.

Hivyo ushauri wangu kwa Serikali ipige marufuku unywaji wa pombe kwa raia wake na ipige marufuku uuzwaji pia utengenezaji wa pombe hapa nchini. Ipige marufuku hata kwa muda wa miaka 10 - 15 hivi

Nawasilisha.
 
Nchi hii ni tajiri" na utajiri sio kwa pombe....
Mojawapo ya chanzo kikuu ya mapato ya serikali ni pombe na sigara.
Je una vyanzo mbadala baada ya kukataza pombe? Au unataka wakakusanye kodi kanisani na misikitini???....
 
Unajua TRA wanakusanya ngapi kwa makampuni ya pombe? Ni kiburudisho kizuri hasa baada ya kazi . Chakula ukizidisha unavimbiwa na kushindwa kufanya kazi, nayo pombe usizidishe. Kunywa kistaarabu kama mimi ninavyopiga viserengeti viwili.
 
Back
Top Bottom