SERIKALI NI DUDE KUBWA SERIKALI NI NDOA.

SERIKALI NI DUDE KUBWA SERIKALI NI NDOA.

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,531
Reaction score
2,911
Ndugu zangu tunajisahau sana, kila kukicha mnalichokonoa hili Dubwana. Raia wote mnapaswa kujua Hatari kubwa sana inaweza kupata endapo utataka shindana na Serikali. Kwa uhalisia Serikali yoyote dunian inapaswa kuwa na nguvu kukabiliana na maadui wote wanaoonekana na wanaofikirika.

Kuna madhara makubwa sana yanaweza ikumba jamii endapo Raia watakuwa na nguvu sawa na serikali. Itambulike raia wote wanaipa nguvu serikali sasa iweje tena ka kikundi cha watu kawe na nguvu sawa na serikali.

Mifano hai ipo mingi inayoonyesha yapi yatatokea endapo serikali ikidodoshwa, nchi kama Libya, Sudan, Congo, Haiti, na nk. mara nyingi Raia wanalishwa maneno ya uwongo kuona kwamba serikal yao haina faida ila hali hubadikika pale tu wanapoisaliti na kuidondosha.

Serikali ni kama Ndoa, ewe raia usije tamani serikali ya taifa lingine ukizania raia wake wana nafuu.. kitanda usichokilalia hujui kunguni wake hivyo vitanda vya nchi nyingine raia wanaliwa marinda laivu. Wewe hii serikali yako na tabia zake ndio chaguo lako raia tuendelee kuvumilia tuu ivi tukiachika serikali gani itatupokea?

Na serikali zote huwa zinakula nyama za watu. Hao watu wanaweza kuwa wa serikali nyingine au watoto wake wenyewe!
 
Back
Top Bottom