Serikali ndo chanzo cha migogoro ya ardhi

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Nimeona tangazo waziri Lukuvi anasema wanakuja na utaratibu mpya ..
Viwanja ambavyo wenyewe hawapo kwenye sijui vitambulisho vya Taifa..watanyang'anywa na vitapigwa mnada...

Toka serikali ianzishe utaratibu wa kubadili policy zinazohusu ardhi na sheria zake karibu kila mwaka .. migogoro imeongezeka badala ya kupungua..

Wakati wa serikali ya wakoloni kulikuwa hakuna kabisa migogoro ya ardhi
Mtu akinunua kiwanja ndo keshanunua
Serikali za watu weusi ndo chanzo cha matatizo..mara offa ..ziko zaidi ya moja..
Mara hati zaidi ya moja kiwanja kimoja
Mara sheria zimebadilishwa zipo mpya zinasema hiki ...mradi kila siku matamko na sheria mpya zinazo ongeza tatizo badala ya kutatua...

Hii ndo Ile wazungu wanatuambia hatuwezi kujitawala...
 
Kukurupuka kutoa matamko ambayo hayapo kisheria ndio chanzo cha matatizo, sheria zenyewe wamerithi toka kwa mkoloni kipi kinachowashinda kuzifuata? wanaleta ujuaji wenyewe ndio maana mambo yanawashinda kila kukicha.

Sijaona mahali kwenye Land Act 1999 panaposema mtu anaweza kunyan'ganywa ardhi yake kama hatakuwa na kitambulisho cha taifa, nachojua mtu hunyan'ganywa ardhi kama hajaiendeleza kwa miaka kadhaa.
 
1. Nadhani tutakua tunaionea Serikali kwenye hili. Kwa maoni yangu, migogoro imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wafanyakazi wa wizara ambao wamekua sio waaminifu, ambao wamekua wakitoa nyaraka za umiliki mara mbili au zaidi kwa kipande kimoja cha ardhi.

Ingawa pia, siku zinavyozidi kusonga, tuelewe kwamba migogoro ya ardhi itazidi kuongezeka kwa sababu (a) idadi ya watu inaongezeka, lakini ukubwa wa ardhi upo palepale, kwahiyo uhitaji unakua mkubwa, na hilo pekee linaweza pelekea kuwepo kwa migogoro ya ardhi hasa maeneo ambayo yameshakuwa na miundo mbinu, kama barabara, umeme, vyanzo vya maji nk. (b) Migogoro inaongezeka/ itaendelea kuongezeka kwakua siku zinavyosonga uelewa wa watu/ watanzania juu ya thamani ya ardhi pia unaongezeka, jambao ambalo linapelekea watu kuitafuta ardhi kwa gharama kubwa ( kama vile kutumia pesa, na madaraka nk.).

2. Swala la utambuzi wa wamiliki wa ardhi kwa kutumia kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni muelekea mzuri, endapo Serikali itajiridhisha kwamba kila mwenye kitambulisho cha NIDA ni raia wa Tanzania ( maana kuna uwezekano mkubwa raia wa Kenya, na Congo wakawa na kitambulisho hiko). Na pia, Serikali ijihakikishie kwamba kila Mtanzania anayestahili kupewa kitambulisho amepatiwa kitambulisho ili awe na nafasi ya kumiliki ardhi. Sina hakika kama mpaka kufikia July 2021, wananchi wa Kigoma vijijini wanaomiliki ardhi watakuwa wamepatiwa kitambulisho cha NIDA, vinginevyo naliona zoezi hili ni endelevu, kulingana na kasi ya utoaji wa vitambulisho. Hata hivyo, Wizara tayari imeshaweka muongozo

Kiujumla, swala la kitambulisho cha NIDA halikwepeki, huko tuendapo NIDA ndio itatumika katika ofisi zote kama nyaraka KUU ya utambuzi, na ni bora kwa kila mtanzania ambaye hajapata kitambulisho hiko afanye jitihada kukipata.
 
Mimi niliwahi sema, serikali imeharibu kabisa mfumo wa shughuri za kijamii kwa kukosa weledi. Sheria imeweka wazi mtu ama taasis za uma na binafsi wanapochukua ardhi ya mtu basi wanapaswa kulipa fidia kwa mwenye eneo. Lakini katika kulipa fidia ni TANROAD tu ndiyo wanatekeleza, halmashauri zote zinapima maeneo ya watu na kuyatenga kwa ujenzi wa miradi lakini hawatoi fidia. Migogoro ya ardhi inasababishwa na halimashauri zetu za wilaya na miji.
 
Kitu kibaya kuliko zote ni kubadili sheria kila mara...
Sio watu wote wanaojua sheria zimebadilishwa
 
1. Nadhani tutakua tunaionea Serikali kwenye hili. Kwa maoni yangu, migogoro imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wafanyakazi wa wizara ambao wamekua sio waaminifu, ambao wamekua wakitoa nyaraka za umiliki mara mbili au zaidi kwa kipande kimoja cha ardhi.

Ingawa pia, siku zinavyozidi kusonga, tuelewe kwamba migogoro ya ardhi itazidi kuongezeka kwa sababu (a) idadi ya watu inaongezeka, lakini ukubwa wa ardhi upo palepale, kwahiyo uhitaji unakua mkubwa, na hilo pekee linaweza pelekea kuwepo kwa migogoro ya ardhi hasa maeneo ambayo yameshakuwa na miundo mbinu, kama barabara, umeme, vyanzo vya maji nk. (b) Migogoro inaongezeka/ itaendelea kuongezeka kwakua siku zinavyosonga uelewa wa watu/ watanzania juu ya thamani ya ardhi pia unaongezeka, jambao ambalo linapelekea watu kuitafuta ardhi kwa gharama kubwa ( kama vile kutumia pesa, na madaraka nk.).

2. Swala la utambuzi wa wamiliki wa ardhi kwa kutumia kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni muelekea mzuri, endapo Serikali itajiridhisha kwamba kila mwenye kitambulisho cha NIDA ni raia wa Tanzania ( maana kuna uwezekano mkubwa raia wa Kenya, na Congo wakawa na kitambulisho hiko). Na pia, Serikali ijihakikishie kwamba kila Mtanzania anayestahili kupewa kitambulisho amepatiwa kitambulisho ili awe na nafasi ya kumiliki ardhi. Sina hakika kama mpaka kufikia July 2021, wananchi wa Kigoma vijijini wanaomiliki ardhi watakuwa wamepatiwa kitambulisho cha NIDA, vinginevyo naliona zoezi hili ni endelevu, kulingana na kasi ya utoaji wa vitambulisho. Hata hivyo, Wizara tayari imeshaweka muongozo

Kiujumla, swala la kitambulisho cha NIDA halikwepeki, huko tuendapo NIDA ndio itatumika katika ofisi zote kama nyaraka KUU ya utambuzi, na ni bora kwa kila mtanzania ambaye hajapata kitambulisho hiko afanye jitihada kukipata.
Kukipata jitambukisho cha nida n Kama kutafuta kucha za simba mwaka wa nne huu Nina namba ya nida Sina kitambulisho ukienda ofisi zao n blah blah Kuna mmoja alinijibu wenzako Wana mwaka wa sita hawajapata vitambulisho sembuse wewe miaka 2 kumbuka hapo n nida makao makuu

N wazo jema ila serikal inajifelisha yenyewe kupitia taasisi zake Kama nida na maafisa ardhi

Toka nida ianzishwe imetoa 24% tu ya vitambulisho nvhi nzima unadhan hil zoez litafanikiwa kirahis hvyo mpaka lukuvi atastaafu siasa zoez litakuwa halijafanikiwa
 
Back
Top Bottom