Serikali na watendaji wake hawawathamini wazee waliostaafu

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,135
2,000
Kuna kila dalili kuwa ukishastaafu serikali haikuthamini Tena. Au hii tuiweke kuwa pengine serikali Ina Nia nzuri lakini haitaki tu kuwasikiliza Hawa wazee.

Manispaa ya Musoma Ni kielelezo Cha ulaghai na ukiukwaji wa haki za wastaafu. Wapo wastaafu tangu 2017 Hadi 2020 hawajapewa mapunjo yao yanayotokana na kubadilishiwa madaraja ya mishahara toka ngazi mbalimbali. Wahusika wako kimya kwa kisingizio kuwa madai yanashughulikiwa na hazina.

Kikubwa kwenye post yangu Ni namna watendaji kwa maana ofisi ya mkurugenzi isivyowajali wastaafu wake. Hivi inakuja akilini mtu kustaafu 2019 au 2020 Hadi Leo hajapewa hela ya kusafirisha mizigHii

Hii ofisi Ina vituko. Wakati wa promotions toka daraja moja kwenda nyingine waliojaliwa waliandika barua za kukubali madaraja na Kisha kuomba mapunjo kwa kuandika barua na kujaza fomu. Kituko kikaja kuwa waje Tena kuandika upya na kusogeza tarehe za mbele.

Nieleze hili vizuri. Ninaowazungumzia ni waliopandishwa vyeo vya madaraja 2015 August. Wengi ambao Sasa hivi Ni wastaafu walijaza fomu na kuandika barua Kama ilivyoelekezwa kabla ya January 2016 na barua na fomu zao za madai kupitishwa kwa ajili ya malipo. Hadi hii leo hakijulikani Ni Nini inaendelea licha ya kuitwa Mara zaidi ya 2 kuja kubadili tarehe ya kuandika barua ya madai kusomeka 2019.

Kwangu hii nauita ubabaishaji, na kwa sababu hakuna mwakilishi wa wastaafu Basi vijana walioko ofisi ya utumishi wanafanya watakavyo. Kuna vituko vingine pia. Mtu umestaafu kazi iwe kwa hiari au kwa lazima 2018 na kujaza particulars zako kikamilifu ikiwemo daraja ulilostaafia halafu unashituliwa baadaye Sana November 2019 kufutiwa promotion ( daraja la kustaafia).

Kama yupo mtu serious ambaye anamuogopa Mungu Basi atembelee manispaa hii ya Musoma akutane na Hawa wazee wasiojua Nini hatima ya malipo Yao. Najua Kuna viongozi wapo wanaofuatilia.
Tulishiriki site kuijenga nchi tukishastaafu tupewe haki zetu.

Kuimba mapambio jukwaani wakati lipo kundi linanyimwa haki zake siyo sahihi. Hatuna utamaduni wa kunyanyua mabango kuonyesha hisia tunavyojisikia.

Tunachohitaji ni haki tu Basi.
 

TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
910
1,000
Mkuu unavyosema ni ukweli mtupu , na hadi ofisi zetu zinakuwa zinaitaji kujuana aku udai kimenomeno sana....

.... ni sehemu ambayo uwezakono wa kupew haki yako ni ngumu kwa 75% hasa maslai
IMG_20211027_073451.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom