Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

raha ya deni kulipa, asilete swaga za majukwwani ya siasa kwenye mambo ya msingi
 
Kila mmoja ataguswa kwa wakati wake na kama unadhani mbowe anaonewa nenda mahakamani ukamsaidie.Mbona mbowe mwwnyewe yuko kimya weee kimekuuma nini?

Naamini kama serikali ingelegea kidogo tu jengo la Bilicana lingeishia mikononi mwa Mbowe. Tayari alishaanza kuimba ngonjera za kutumia mabilioni kukarabati jengo!!!
 
Na raha ya mafisadi, wezi, wala rushwa ni kuwekwa lupango wachezee mvua nyingi pamoja na kufilisiwa siyo kuleta usanii wa "sifukui makaburi ya zamani" Hakuna sheria yoyote nchini ambayo inamzuia kufukua kaburi za zamani ni usanii wake tu wa kutaka kuwakingia kifua mafisadi wenzie kwa sababu anajua fika yeye mwenyewe ni mchafu kupindukia.

raha ya deni kulipa, asilete swaga za majukwwani ya siasa kwenye mambo ya msingi
 
Huyo DC anatafuta kiki tu kwa bilionea Mbowe. Yeye masuala ya kodi yanamhusu nini? Njaa mbaya sana.
 
Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
Wewe ndiye msemaji wa hotel ya mbowe au msemaji wake binafsi??
 
Kama taifa tukisema tuanzishe oparesheni ya wakwepa kodi, yawezekana Mbowe akawa wa mbali sana asijadiliwe kabisa. Lakini tumefikaje hapa? Hakuna chuki ya kisiasa naomba majibu?

Hapa tunadanganyana tu! Kwa ujumla hizi ni siasa za visasi na kukomoana, hakuna cha Kodi wala Mazingira hapa!
Hivi tangu lini DC akafuatilia ulipaji kodi na utunzaji wa mazingira?
Kuna TRA na NEMC ndio wahusika katika madneo hayo mawili. Sasa huyu DC kichwa maji anaingiliaje maswala hayo?
Lakini pia hata kama ni kweli kuwa Mbowe ana tatizo hilo la kutolipa kodi,vipi kuhusu Viongozi wa CCM wenye biashara zao wanalipa kweli?
Namshauri Mbowe na CHADEMA wafanye utafiti kwenye biashara za vigogo wa CCM kama kina Rais mstahafu Mkapa na mkewe, Rostam Aziz, Riz Kikwete, Antony Diallo na wengineo kama kweli hawadaiwi?
 
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Kwani ni Mbowe tu anayedaiwa kodi? Kuna ma kampuni mangapi yanapambana kulipa kodi za nyuma kimya kimya? Mbowe kama mwana siasa was to be a role model....kuandikwa ni matokeo ya nafasi yake kwenye jamii
....ila wapo wengi tu wanaobanwa
 
Mbowe pekee yake ndiyo siyo mlipaji kodi tanzania....

OvA
Bakhresa kwani ni mwanasiasa? Mbona akibanwa na akalipa? Manji si katimuliwa juzi juzi pale Quarity plaza?
 
Huyo dc njaa tu, hata trafki akitaka umpe rushwa atakusumbua sumbua kwa kutafuta makosa ili mradi tu apate hela ya kubrush.
 
mleta mada sijaelewa lengo lako yaani unataka Mbowe asilipe kodi kwa kuwa wewe unaona kuwa anafanyiwa visasi?????

sisemi kuwa CCM wasafi hapana ila siasa ni mchezo mchafu na ndio maana kila mtu anajaribu kumchafua mwenzie kadri awezavyo..

yawezekana Kikwete na Mbowe wanafichiana siri nyingi sana maana sio kwa kashfa zile walizokuwa wanamtupia ila akawanyamazia tuu
 
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Taja na wengine wasiyolipa mkuu bila kujali itikadi zao.

Lakini pia kuwa mzarendo wa nchi yako kwa kusema kuwa kiongozi inatakiwa awe ni mfano wa kuigwa. Kiongozi Kama halipi kodi je atakusanya kodi??
Alipe kodi tu. Maendeleo hayawezi kuja kama watu hawalipi kodi.

Hongera Mh. Rais kwa kupambana na wakwepa kodi. Tunaendelea kukuombea ili ushinde hii vita.
 
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Bro, acha mambo ya ujanjaujanja yy inatakiwa kulipa kodi kwani hiyo ndo mantiki mambo ya TANESCO kudai serikali ni jambo jingine kabisa, kwa hoja yako huyo kamanda Mbowe ni vema kudaiwa kwasabu2 TANESCO inadai serikali?
 
Nae huwa alikua anasema serikali legelege haiwezi kukusanya kodi. Au alikua anamaana gani?
 
Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
Kama mimi mkuu nilishalipa mkopo wangu wa bodi ya mkopo tena kwa mkupuo mmoja na risti wakanipa. Leo hii jina langu lipo kati ya wadaiwa sugu. Nimekwenda pale hakuna rekodi yo yote kuonyesha kuwa nililipa japo risti ninayo na wamethibitisha siyo feki. Mtu kachukua pesa hizo na kwenda kujengea mhekalu wake sasa hivi huko aliko anakenua meno na wanawe na jamii si ajabu inamwona kuwa ni mjanja. Kumbe jizi tu linalopaswa kuvishwa tairi shingoni, kumwagiwa wese na kutiwa kiberiti.

Ila Mbowe naye alipage kodi jamani aaaargh!!!
 
Trilioni moja!!!

Gharama za hizo ndege mbili wala haizidi 15% ya hiyo trilioni moja!

Tatizo la Tanesco ni kama ilivyokuwa ATCL kipindi cha nyuma. Tatizo lake ni zaidi ya fedha!
 

Kwa hiyo mbowe hatakiwi kulipa kodi!
Wafichue wana ccm wasiyolipa kodi awamu hii ni ya tofauti sana watashughulikiwa kama anavyoshughulikiwa mbowe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…