Iceman 3D
JF-Expert Member
- Sep 3, 2016
- 20,611
- 67,110
HahahaTutajie wengine unaowafahamu
Mi nimeuliza swali hapo, je katika nchi yenye wafanyabiashara zaid ya milion 5 mkwepa kodi ni mmoja tu!?
HahahaTutajie wengine unaowafahamu
raha ya deni kulipa, asilete swaga za majukwwani ya siasa kwenye mambo ya msingiJANGA JINGINE KWA MBOWE
![]()
Na OMARY MLEKWA-HAI
MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.
Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.
Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.
Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.
Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.
Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.
Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.
“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.
“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.
Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.
“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.
“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.
Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.
Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.
Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.
Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.
Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.
Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.
Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.
“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.
“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.
Kila mmoja ataguswa kwa wakati wake na kama unadhani mbowe anaonewa nenda mahakamani ukamsaidie.Mbona mbowe mwwnyewe yuko kimya weee kimekuuma nini?
raha ya deni kulipa, asilete swaga za majukwwani ya siasa kwenye mambo ya msingi
Wewe ndiye msemaji wa hotel ya mbowe au msemaji wake binafsi??Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
Kama taifa tukisema tuanzishe oparesheni ya wakwepa kodi, yawezekana Mbowe akawa wa mbali sana asijadiliwe kabisa. Lakini tumefikaje hapa? Hakuna chuki ya kisiasa naomba majibu?
Kwani ni Mbowe tu anayedaiwa kodi? Kuna ma kampuni mangapi yanapambana kulipa kodi za nyuma kimya kimya? Mbowe kama mwana siasa was to be a role model....kuandikwa ni matokeo ya nafasi yake kwenye jamiiNaamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Bakhresa kwani ni mwanasiasa? Mbona akibanwa na akalipa? Manji si katimuliwa juzi juzi pale Quarity plaza?Mbowe pekee yake ndiyo siyo mlipaji kodi tanzania....
OvA
Huyo dc njaa tu, hata trafki akitaka umpe rushwa atakusumbua sumbua kwa kutafuta makosa ili mradi tu apate hela ya kubrush.Hapa tunadanganyana tu! Kwa ujumla hizi ni siasa za visasi na kukomoana, hakuna cha Kodi wala Mazingira hapa!
Hivi tangu lini DC akafuatilia ulipaji kodi na utunzaji wa mazingira?
Kuna TRA na NEMC ndio wahusika katika madneo hayo mawili. Sasa huyu DC kichwa maji anaingiliaje maswala hayo?
Lakini pia hata kama ni kweli kuwa Mbowe ana tatizo hilo la kutolipa kodi,vipi kuhusu Viongozi wa CCM wenye biashara zao wanalipa kweli?
Namshauri Mbowe na CHADEMA wafanye utafiti kwenye biashara za vigogo wa CCM kama kina Rais mstahafu Mkapa na mkewe, Rostam Aziz, Riz Kikwete, Antony Diallo na wengineo kama kweli hawadaiwi?
Taja na wengine wasiyolipa mkuu bila kujali itikadi zao.Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Alipe kodi tu. Maendeleo hayawezi kuja kama watu hawalipi kodi.
Hongera Mh. Rais kwa kupambana na wakwepa kodi. Tunaendelea kukuombea ili ushinde hii vita.
Bro, acha mambo ya ujanjaujanja yy inatakiwa kulipa kodi kwani hiyo ndo mantiki mambo ya TANESCO kudai serikali ni jambo jingine kabisa, kwa hoja yako huyo kamanda Mbowe ni vema kudaiwa kwasabu2 TANESCO inadai serikali?Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Nae huwa alikua anasema serikali legelege haiwezi kukusanya kodi. Au alikua anamaana gani?Hapa hakuna kuangalia sura ya mtu
Mbowe ni mtanzania kama watanzania wengine
Lazima afuate utaratibu na sheria za nchi kama raia wengine.
Kulipa kodi ni lazima
Kukwepa kulipa kodi ni kosa kubwa
Nchi nyingine hawezi kuwa kiongozi kabisa.
Kama unadhani mbowe mkubwa
Mkubwa CDM
Sisi lazima afuate sheria.
Unapo kosoa na kuwa mpinzani
Inakupasa uanze kujisafisha wewe
Mbowe anajua kukosoa wenzie kumbe yeye ni mchafu zaidi
Kama mimi mkuu nilishalipa mkopo wangu wa bodi ya mkopo tena kwa mkupuo mmoja na risti wakanipa. Leo hii jina langu lipo kati ya wadaiwa sugu. Nimekwenda pale hakuna rekodi yo yote kuonyesha kuwa nililipa japo risti ninayo na wamethibitisha siyo feki. Mtu kachukua pesa hizo na kwenda kujengea mhekalu wake sasa hivi huko aliko anakenua meno na wanawe na jamii si ajabu inamwona kuwa ni mjanja. Kumbe jizi tu linalopaswa kuvishwa tairi shingoni, kumwagiwa wese na kutiwa kiberiti.Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
Trilioni moja!!!Hapana inawezekana kabisa Mkuu! Mbona imewezekana kununua ndege kwa cash kwa trilioni moja!? Sasa kama imewezekana kulipa trilioni moja kununua ndege iweje washindwe kulipa deni la TANESCO la 125 billion!? Hawana nia ya kulipa deni hilo pamoja na kujua fika kwamba hali ya fedha katika shirika hilo ni mbaya sana. Labda uniambie hii tuliyoambiwa kwamba ndege zimenunuliwa kwa cash nao ulikuwa ni uongo mwingine uliotukuka.
Hapa tunadanganyana tu! Kwa ujumla hizi ni siasa za visasi na kukomoana, hakuna cha Kodi wala Mazingira hapa!
Hivi tangu lini DC akafuatilia ulipaji kodi na utunzaji wa mazingira?
Kuna TRA na NEMC ndio wahusika katika madneo hayo mawili. Sasa huyu DC kichwa maji anaingiliaje maswala hayo?
Lakini pia hata kama ni kweli kuwa Mbowe ana tatizo hilo la kutolipa kodi,vipi kuhusu Viongozi wa CCM wenye biashara zao wanalipa kweli?
Namshauri Mbowe na CHADEMA wafanye utafiti kwenye biashara za vigogo wa CCM kama kina Rais mstahafu Mkapa na mkewe, Rostam Aziz, Riz Kikwete, Antony Diallo na wengineo kama kweli hawadaiwi?