Serikali na Kesi za Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na Kesi za Uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ngoshwe, Apr 8, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi (National Election Act, 2010) pamoja na Kanunizi za Kupinga Matokeo ya Uchaguzi (Election Petition Rules, 2011, mgombea yeyote wa ubunge/udiwani anayetaka kupinga matokea au taratibu za uchaguzi anatakiwa katika maombi yake (Petition) kumuunganisha Mwansheria Mkuu wa Serikali. Kwa upnde mwingine, matakwa haya ya sheria kwa namna moja au nyingine yanaiweka Serikali ya chama tawala katika wakati mgumu hasa pale inapotaka kumpigania mgombea wake aliyeshindwa aweze kurejea kwa staili nyingine (kwa amri ya mahakama).

  Imebainika katika kesi nyingi za kupinga matokeo ya uchaguzi, wagombea wa CCM wamekuwa wakileta hoja ambazo ndizo wapinzani na wananchi wengi wameziipua na kulalamikia kuwa "Uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na dosari kibao za watendaji Serikalini ikiwemo wasimamizi wa Uchaguzi (Returning Officers) kutumia mbinu za medali kufanikisha ushindi wa wale walio wao!.

  Cha kusikitisha, wapo pia mawaziri wastaafu ambao walitumika katika Serikali ya CCM lakini leo wamefungua kesi kudai kuwa watendaji wa Serikali ya Chama Chao (CCM) walichakachua matokeo na kusababisha wapinzania kushinda...
  Wakati wamemuunganisha Mwanasheria Mkuu katika kesi hizo, ni dhairi kuwa walalamikaji hao ambao ni wanachama hai wa CCM wanaishtaki Serikali ya chama chao ambapo kwa upande mmoja au mwingine wakishinda katika kesi hizo wanataka walejeshwe kwenye mchakato ili waje kuwa wawakilishi kwa chama ambacho Serikali yake haizingatii haki wala taratibu..

  Hata hivyo, ikiwa mahakama itaona inafaa uchaguzi urejewe, ni wazi kuwa utarejewa kwa gharama ya Serikali..Hata hivyo, kwa upande wa Serikali nia ni kuhakiksha kuwa uchaguzi haurejewei hata kwa gharama yeyote ile. Katika kesi hizi za uchaguzi ndipo unapoweza kuona Mwanasheria Mkuu akiungana na Wapinzani ili kuitetea Serikali ya chama tawala kwa lengo la kupingana na mwanachama wa chama tawala..
   
Loading...