S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 82
Iwapo tuliona vi-Hiace havifai sijui ilikuwaje tukaona Bajaji zinafaa..!!
Ni kweli 'Bajaji' si suluhisho la matatizo ya usafiri kwenye jiji letu.
Lakini kuhusiana na ajali za barabarani nadhani tatizo si Bajaji (au aina ya chombo cha usafiri). Tatizo kwa sehemu kubwa ni madereva wa vyombo vya usafiri na namna gani wanakuwa regulated (licencing process is so poor).
Kwa mfano:
Tukitaka kupunguza ajali za barabarani ni lazima tuanze na madereva na si vinginevyo.
- Madereva kutofuata/zingatia alama na sheria za barabarani. Ukitizama sehemu nyingi madereva hawazingatii kabisa alama zinazoonesha kiasi cha juu cha mwendo kinachoruhusiwa kwenye baadhi ya maeneo ya barabara zetu. Angalia pia jinsi wanavyo overtake magari mengine, hawako makini kabisa!
- Wimbi kubwa la 'madereva' wasio na ujuzi wa kutosha hasa pikipiki,bajaji, daladala nk.
- Madereva wa magari kudhani kwamba kutumia barabara ni yao peke yao au iko juu kuliko watumiaji wengine (baishkeli, bajaji, wende kwa miguu nk). Dereve kusimama kwenye alama za pundamilia anaona kama vile anatoa favour kwa waenda kwa miguu!
- Je ni madereva wangapi tunaowaona barabarani na vyombo vya moto wamepata leseni kihalali? (i.e. wamekuwa tested na idara inayohusika kama wana uwezo wa kuendesha barabarani au kuendesha magari ya abiria au magari ya mizigo nk nk).
Apart from kulinganisha usawa wa vyombo hivi vya usafiri - Buses, Dalalas, Lorries, Saloon Cars, 4wheel drive cars, Bajajis, Pikipikis, Bicycles - sijui kama vyote vinalipiwa road licence fee, sijui drivers wana class tofauti za endeshaji etc. Ila VIONGOZI WA HII NCHI YA TANZANIA, WANGEFIKIRIA KU-REPLAN MJI WA DAR ES ALAAM. IMAGINE ASUBUHI WANANCHI WA MKOA WA DAR, WANAKUJA SEHEMU MOJA - CITY CENTRE - ndiko ofisi zote zilipo - soko kubwa la Kariakoo etc. Laiti ofisi nyingine zingekuwa KIBAHA - ZINGINE BAGAMOYO - TEMEMKE ETC. AT LEAST MJI UWE NA MATAWI (KAMA MTI VILE) - HILO NI WAZO LANGU - JEE WANA JF MNAONAJE?

Habari za Kitaifa
Polisi vitani na bajaj
Imeandikwa na Veronica Mheta; Tarehe: 17th April 2009 @ 21:00
Habari Leo
Kutokana na ajali nyingi zinazosababisha watu kupoteza maisha au kupata ulemavu, Polisi Dar es Salaam itaanza operesheni maalumu kukamata pikipiki aina ya bajaj na madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani.
Operesheni hiyo itaanza keshokutwa, kwa kukamata madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani, kufungiwa leseni na kufungwa ili iwe fundisho kwa wengine. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema ajali nyingi zinazotokea hivi sasa zinazotokana na pikipiki aina ya bajaj.
Alisema kati ya Januari mwaka jana hadi Machi mwaka huu, Mkoa wa Kinondoni uliongoza kwa ajali 84 za bajaj na kusababisha vifo vya watu 19 na 82 kujeruhiwa. Mkoa wa Ilala ajali sita, kifo cha mtu mmoja na 10 kujeruhiwa wakati Temeke ilipata ajali 11 na kujeruhi watu 12.
Alisema ajali hizo zimesababisha baadhi ya watu kujeruhiwa, kupata ulemavu na wengine kufa kutokana na uzembe wa madereva hususani wa bajaj, ambao hawana leseni au hata kama wanazo hawajui sheria za barabarani.
Kwa kuwa ajali nyingi zinazotokea sasa zinasababishwa na madereva wa bajaj, alisema Polisi itafanya msako Dar es Salaam kwa lengo la kukamata madereva wasio na leseni, wenye leseni bandia na wanaopita pembeni au nje ya barabara.
.