Serikali na Bajaj: Tunaelekea wapi?

kaisa079

Member
Nov 16, 2007
20
0
Bajaj sasa kuwa 'ambulance'

SERIKALI itatoa pikipiki za magurudumu matatu (bajaj) kwa vituo vyote vya afya na zahanati nchini, ili kukabiliana na tatizo la usafiri kwa wagonjwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, alisema wizara yake tayari imetenga fedha kwa ajili ya kununua pikipiki hizo, ambapo kwa kuanzia, zitanunuliwa 350 na kusambazwa katika vituo vya afya 481 katika wilaya zote.

Alisema pikipiki hizo zitafungwa vitanda na wagonjwa kusafirishwa kutoka vituo vya afya kwenda katika hospitali za wilaya.

"Tunaamini tutakaposambaza bajaj hizo tutakuwa tumefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza vifo vya wagonjwa ambavyo vingine vinatokana na kukosekana kwa usafiri wa wagonjwa," alisema Profesa Mwakyusa.

Alisema kwa kuwa mpango huo utaanza na pikipiki chache, ikilinganishwa na idadi ya vituo vya afya, ambavyo ni ya 481, wizara itaangalia wilaya ambazo zitaonekana kuwa na tatizo kubwa la usafiri, ambapo wataanza na Muleba mkoani Kagera, ambapo pia mgao huo utaangalia wilaya nyingine 26 ambazo kasi ya malaria iko juu.

Kuhusu mapambano dhidi ya malaria, Profesa Mwakyusa alisema Serikali inahimiza wananchi kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa na kuwataka wafukie madimbwi ya maji machafu, ambamo mbu hufanya mazalio na makazi yao.

Alisema wakati wananchi wakiendelea na mapambano dhidi ya malaria, kuna mtu amejitokeza kwa ajili ya kuisaidia Tanzania vyandarua milioni 12, ili viweze kusambazwa katika vituo vya afya kwa ajili ya wananchi.

Alisema mtu huyo anaishi Marekani na amekuwa rafiki mkubwa wa Serikali ya Tanzania, lakini hakutaka kuliweka jina mtu huyo hadharani.

"Nimekuwa na mawasiliano mazuri na mtu huyo na kuzungumza naye kuhusu vyandarua hivyo, lakini awali alishakutana na Rais Jakaya kikwete, Marekani, na kuelezea nia yake ya kutusaidia baada ya Rais kumweleza mikakati na sera za afya nchini, katika mapambano dhidi ya malaria," alisema.

Pia aliwataka wananchi kutumia dawa za ALU kutibu malaria, kwani uwezo wake ni mkubwa ikilinganishwa na SP na klorokwini, ambazo uwezo wake ni mdogo kutokana na kutumika muda mrefu na kuwa sugu.

Kuhusu upatikanaji wa vifaa na dawa katika vituo vya afya, alisema kwa sasa umeandaliwa mpango maalumu ambao utasaidia kuondoa kero iliyopo kwa baadhi ya maeneo ambapo wananchi wamekuwa wakilalamika kukosa dawa na vifaa kwa wakati.

Kuhusu maambukizi ya UKIMWI, Profesa Mwakyusa alisema kutokana na kampeni ya upimaji kwa hiyari iliyoanza Julai 14 mwaka huu, mafanikio yapo kwani watu wamejitokeza kwa wingi na kupima afya zao.

Alisema hali hiyo imeleta mtazamo mpya, kwani siku zote Serikali imekuwa ikitangaza kuwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ni asilimia 7 wakati hali iliyopo sasa inaonesha kasi imepungua na kufikia asilimia 4.9.

Hata hivyo, wakati kasi ikionekana kupungua, mkoa wa Iringa unaongoza kwa kasi ya maambukizi mapya ya UKIMWI kwa asilimia 12.6 ukifuatiwa na Mbeya ambao una asilimia 12.1.

Wakati mikoa hiyo ikiwa juu, mkoa wa Kigoma ni wa mwisho kasi ya maambukizi ambayo ni asilimia 1.2, ukifutiwa na Manyara asilimia 1.6 na Kilimanjaro asilimia 1.7.

Pia alisema Mkoa wa Dar es Salaam umeonekana kupungua kasi ya maambukizi ikilinganishwa na miaka iliyopita kwani takwimu zilizopo zinaonesha kuwa kasi ya maambukizi kwa mkoa huo ni asilimia 5.9.

Kuhusu ebola, Profesa Mwakyusa alisema Serikali inaendelea kujipanga vyema katika kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini kwa kupeleka wataalamu katika mikoa ya mipakani, ili waweze kufuatilia kwa makini dalili za ugonjwa huo.

Kuhusu Mfuko wa Bima ya Afya, alisema nchi karibu zote zilizoendelea zinatumia utaratibu huo wa kutumia huduma za bima ya afya, hivyo aliwataka wananchi kuunga mkono mpango huo.

Profesa Mwakyusa akizungumzia suala la kuboresha huduma za afya Mkoa wa Dar es Salaam alisema tayari mpango wa kujenga Hospitali ya Mkoa umekamilika na itajengwa Msasani eneo la TIRDO.

Alisema CCBRT ilijitolea kujenga hospitali hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa ambapo Wizara ya Afya imetenga sh. milioni 600 katika kusaidia ujenzi huo.

Kuhusu Ripoti ya Sakata la upasuaji kimakosa, katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ripoti itatangazwa baadaye kutokana na kushindikana kutangazwa jana, kwa kuwa Profesa Mwakyusa anaratajiwa kwenda kijiji cha Partimbo, Kiteto kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Kiteto, marehemu Benedict Losurutia anayetarajiwa kuzikwa leo
 
Mmhh!?? Kazi kwei kwei mgosi, barabara zenyewe za bush jinsi zilivyo mbovu na mwendo wa bajaj jinsi ulivyo mdogo?Mvua ikinyesha kwa sana ndio basi tena- kwa mtaji huu bora tuendelee tu na punda!Naamini vyombo hivi ni lazima viwe vinaweza safiri fast kwenye barabara mbovu bila kujali kuna mvua au jua if they really mean to save people's life- .Halafu kwa jinsi ninavyoijua size ya bajaj-kitanda kitaenea kweli kwa nyuma?wataishia kuweka vijitanda vidogo which will be lots of troubles kwa ma giants kama mimi.
Again...hapa serekali inaendelea kung'ang'ana na WINGI badala ya kuzingatia UBORA. Nahisi kuna mtu keshavuta 10% yake hapa.....Hao waliotoa uamuzi huu inaonekana hata hawakuufanyia analysis huu mradi and I can understand why- Hivi unadhani waziri yeyote akipata ajali huko bush atapandishwa kwenye hiyo bajaj?Tungesign mikataba mizuri ya madini,kama mamilioni yetu yasingechotwa BOT, Mkataba bomu wa IPTL usingekuwa unatuumiza kila mwezi- hakyanani haya yote yasingetokea, huenda kila mkoa ungekua na kajihelkopta kake ka accident and emergency sasa, aaaaaaggghhhhhhhhhhh!
 
Bajaji iwe ambulance kubeba mgonjwa kutoka nanyamba kumpeleka mgonjwa Mtwara hospital, ambapo bara bara ni mbovu, wakati wa mvua haipitiki, lakini VX zipatazo 2000, zibebe mawaziri na wakurugenzi wa sirikali kutoka mikocheni kwenda posta ya zamani!!! kila siku, na kuwapeleka kwenye mashamba yao Goba, bila kusahau nyumba zao ndogo!!!

''Tanzania ni nchi ya amani na utulivu ulio jaa upendo na udugu''

Hapo ni sawa???
 
This is nonsense... Yes, it is nonsense!!!!

Haya yote yanakuja kutokana na serikali yetu kukosa miongozo (guidelines) katika utekelezaji wa shughuli zake. Maybe aliyetoa wazo la kutaka Bajaj zitumike kama ambulance hakufikiria kabla hajazungumzia hili suala. Kama angeutumia uwezo wake wa kufikiri kama profesa nafikiri ange-consult wataalam ama kutumia common sense before coming up with such a dissapointing comment.

Hivi tunaelewa What is the purpose of having an ambulance? Does our country has specifications for ambulances? I wonder!!!

Tukiwa na specifications za ambulances tuta-eliminate, pamoja na mambo mengine, risk ya nchi yetu kuwa dampo la ma-ambulance bomu).

Binafsi nina reservations zifuatazo:

- Vehicle performance ya Bajaj haifikii/haitafikia viwango (vya kimataifa na hata vya kitanzania - kama tukija kuviweka). Hii inatokana na kwamba Bajaj haina smooth, stable ride na vilevile Speed pamoja na acceleration yake havikidhi viwango vya ambulances, ingawa ina advantage moja kwenye upande wa fuel consumption (fuel range). Tusiangalie upande mmoja tu wa ku-save kwenye mafuta. Maisha ya watu yatakayookolewa kwa kutumia quality ambulance ni aghali mno kuliko gharama za uendeshaji wa bajaj

- Length, width & height ya Bajaj navyo vinatia mashaka. Hata ukifanya modifications---- still other factors might be affected. Mind you, capacity ya engine ya Bajaj inaweza isikuruhusu ufanye hizo modifications.

- Suspensions & shock absorbers za Bajaj (hapa sihitaji kusema - ndugu waziri akapande bajaj ili apate real life experience). Ukimweka mgonjwa humo na barabara zetu zilivyo utakua unachangia katika kuharakisha kifo cha mgonjwa badala ya kuokoa maisha yake.

- Kwenye Bajaj huwezi kuweka temperature controls ambazo zitawawezesha wagonjwa kusafirishwa na kufikishwa salama hospitalini.

Hapo nimezungumzia vitu basic tu. Bado kuna other necessities like electrical systems & components, life saving equipment, sehemu ya kuwekea vifaa kama stretchers, cots and litters, mambo kama oxygen & suction systems and equipment, resuscitators. Ukija kuweka na vitu kama public addressing systems na ukamweka dereva na one attendant, basi Bajaj haitaweza ku-gain acceleration.... Ukifanikiwa ku-gain acceleration basi hiyo haitakuwa ni Bajaj tena... Itabidi uiite jina jingine

Tanzania haijafikia hali ya umaskini kiasi hichi cha kushindwa kununua ambulance zenye standard ya kueleweka katika kila kituo cha afya nchini. It makes more sense wabunge kukopeshwa Bajaj na wagonjwa kununuliwa quality ambulance, na sio vice versa.

Kama kweli viongozi wetu wangekuwa ni critical thinkers na wenye kufanya kazi zao kwa kuzingatia priorities, wangeweza kugundua kwamba gharama ya kununua Ndege ya Mkapa (Gulfstream) ilikua inatosha kununua quality ambulance zinazokidhi viwango (sio Bajaj) kwa kila manispaa hapa nchini. Viongozi wetu wangekuwa creative na kuacha kuwa selfish basi nchi yetu ingeweza kujitosheleza kwa kila kitu. Kumbuka, Mauritius hawana madini wala Mlima Kilimanjaro wala Serengeti, ILA wametuacha mbali ki-per capita. Aibu, aibu!!!!!
 
Huu ndio upumbavu mwingine ambao mtu hastahili kuwa na Phd kujua kwamba Bajaj KAMWE, narudia KAMWE haiwezi kuwa ambulance. Wangepunguza safari za kwenda kutibiwa UK, US, Germany, SA, India na pia kupunguza gharama zisizo za muhimu za serikali basi kila mkoa Tanzania ungeweza kuwa na at least ambulance tano kwa mikoa midogo na jiji kama la Dar ambulance za kileo 5 mpaka 10 kila wilaya.
 
Jamani hii si aibu! NI vituko na mbwembwe za watu waliochangayikiwa! Labda wajaribu kusema kwamba hizi bajaj zitakuwa zinawapeleka wagonjwa lakini siyo ambulance! Haya ni matusi! Yaani hata katika umaskini wetu tunajua ambulance ni nini!
Nikifufukanimekwisha amechambua vyema mapungufu lakini naomba niongeze, hivi tairi za bajaj zitapita wapi, hata kwenye lami kukiwa na shimo haipiti!
Wanataka kutuua tu, hao watawala wetu!
 
This is nonsense... Yes, it is nonsense!!!!

Haya yote yanakuja kutokana na serikali yetu kukosa miongozo (guidelines) katika utekelezaji wa shughuli zake. Maybe aliyetoa wazo la kutaka Bajaj zitumike kama ambulance hakufikiria kabla hajazungumzia hili suala. Kama angeutumia uwezo wake wa kufikiri kama profesa nafikiri ange-consult wataalam ama kutumia common sense before coming up with such a dissapointing comment.

Hivi tunaelewa What is the purpose of having an ambulance? Does our country has specifications for ambulances? I wonder!!!

Tukiwa na specifications za ambulances tuta-eliminate, pamoja na mambo mengine, risk ya nchi yetu kuwa dampo la ma-ambulance bomu).

Binafsi nina reservations zifuatazo:

- Vehicle performance ya Bajaj haifikii/haitafikia viwango (vya kimataifa na hata vya kitanzania - kama tukija kuviweka). Hii inatokana na kwamba Bajaj haina smooth, stable ride na vilevile Speed pamoja na acceleration yake havikidhi viwango vya ambulances, ingawa ina advantage moja kwenye upande wa fuel consumption (fuel range). Tusiangalie upande mmoja tu wa ku-save kwenye mafuta. Maisha ya watu yatakayookolewa kwa kutumia quality ambulance ni aghali mno kuliko gharama za uendeshaji wa bajaj

- Length, width & height ya Bajaj navyo vinatia mashaka. Hata ukifanya modifications---- still other factors might be affected. Mind you, capacity ya engine ya Bajaj inaweza isikuruhusu ufanye hizo modifications.

- Suspensions & shock absorbers za Bajaj (hapa sihitaji kusema - ndugu waziri akapande bajaj ili apate real life experience). Ukimweka mgonjwa humo na barabara zetu zilivyo utakua unachangia katika kuharakisha kifo cha mgonjwa badala ya kuokoa maisha yake.

- Kwenye Bajaj huwezi kuweka temperature controls ambazo zitawawezesha wagonjwa kusafirishwa na kufikishwa salama hospitalini.

Hapo nimezungumzia vitu basic tu. Bado kuna other necessities like electrical systems & components, life saving equipment, sehemu ya kuwekea vifaa kama stretchers, cots and litters, mambo kama oxygen & suction systems and equipment, resuscitators. Ukija kuweka na vitu kama public addressing systems na ukamweka dereva na one attendant, basi Bajaj haitaweza ku-gain acceleration.... Ukifanikiwa ku-gain acceleration basi hiyo haitakuwa ni Bajaj tena... Itabidi uiite jina jingine

Tanzania haijafikia hali ya umaskini kiasi hichi cha kushindwa kununua ambulance zenye standard ya kueleweka katika kila kituo cha afya nchini. It makes more sense wabunge kukopeshwa Bajaj na wagonjwa kununuliwa quality ambulance, na sio vice versa.

Kama kweli viongozi wetu wangekuwa ni critical thinkers na wenye kufanya kazi zao kwa kuzingatia priorities, wangeweza kugundua kwamba gharama ya kununua Ndege ya Mkapa (Gulfstream) ilikua inatosha kununua quality ambulance zinazokidhi viwango (sio Bajaj) kwa kila manispaa hapa nchini. Viongozi wetu wangekuwa creative na kuacha kuwa selfish basi nchi yetu ingeweza kujitosheleza kwa kila kitu. Kumbuka, Mauritius hawana madini wala Mlima Kilimanjaro wala Serengeti, ILA wametuacha mbali ki-per capita. Aibu, aibu!!!!!

mkuu ulioyaeleza yamenitoa machozi.

maneno manene na mazito.

ya reeet wangetusikia na kuyafanyia kazi.

maana jibu likisadifu swala shaka huondoka
 
I totally agree with you.

Hivi wajameni this is truly another USANII at it climax.

Hivi hizi bajaji zina uwezo wa kujaza/kubeba watu wangapi kwa mpigo?

Hesabu ya haraka haraka, ili iwe kama gari ya kubebea wagonjwa baridi (not critically ill patients) unahitaji at least watu wanne.
1. Dereva na msaidizi wake. In case kama bajaji itakwama kwenye tope msaidizi atashuka chini asukume hiyo bajaj.
2. Nesi mmoja.
3. Mgonjwa baridi ambaye at the lowest level angalau atakaa kwenye kigoda wakati anasafirishwa.
Hapa hujaweka kitanda kwa yule mgonjwa ambaye hatakuwa stable kuweza kukaa kwenye kigoda.
Vilevile hujaweka vifaa muhimu kama vile mtungi wa Okisijeni etc. AIBU TUPU.
Is this one of the reasons it is sometimes called a Black Planet???????.

Kama tungekuwa na nia ya kusevu pesa ya mlipa kodi kwenye mafuta, basi hata hayo magari ya VX tusingekuwa tumeyakimbilia.

Mungu awe pamoja nasi anyway.
 
Naomba kuuliza wakuu, hivi zile piki piki au scooter za kubebea abiria zinauzwa wapi na bei yake ni kiasi gani? Natanguliza shukrani.
 
Mkuu zile zinauzwa na wahindi,kuna mdosi mmoja anaitwa Divis peres yupo hapo karibia na Co cabs ya zaman pale kwenye trafic light ya mnaz mmoja corner ya mtaa wa Jamhuri hapa Dar Es salaam.

Bei yake ni kuanzia milion 4,kila kitu inclusive.
 
Ni Adui Mkubwa Sana Wa Taix Wanaziogopa Sana Na Zinaleta Pesa 17,000 Kwa Siku Tegemea Na Maeneo
 
Kumekuwa na ongezeko la ajali nyingi zisizolipotiwa kuhusiana na suala la pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu kubeba abiria. Suala hili limejitokeza zaidi hivi karibuni baada ya gari ya 'mtu maarufu' 'kugongana' na pikipiki ya miguu mitatu (soma: Bajaji).

Tukiangalia hili suala na majadiliano bungeni yaliyopelekea kubadilishwa sheria za usalama barabani ( soma hapa :http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-14-3-2009.pdf) utaona ya kwamba hisia zilitawala zaidi katika kufanya mabadiliko hayo bila ya hata kuyafanyia utafiti wa kina.

Nchi za Asia zinatumia usafiri huu mijini kutokana na msongamano mkubwa wa watu (Overpopulation) kulinganisha na Tanzania. Tanzania ni kama serikali inakwepa katika kutengeneza miundo mbinu ya usafiri hasa katika jiji lake la Dar Es Salaam. Wenzetu wanatengeneza 'subways' na kupanua miundo mbinu sisi tunarudi zama za kale bila hata kujali usalama wa raia. Bajaji na baiskeli ni harzadous kwa usalama wa Mtanzania na si suluhisho bali Tatizo la msingi ni kwa serkali kujenga miundo mbinu ya kisasa.

Chukulia pesa zilizokombwa na mafisaidi zingeweza kujenga barabara ngapi za kisasa? Kwa nini serikali isiingie ubia wa kujenga miundo mbinu itakayo kizi miaka zaidi ya 50 na kung'ang'ania masuluhisho ya muda mfupi yaliyojaa hasara kuliko faida?

Wabunge mlifikiria nini kuruhusu vyombo hivyo kubeba abiria Dar Es Salaam? Je, mlifikiria pia usalama wa abiria? Mnakumbuka ajali ya gari taka magomeni lililoua mama na mwana au mpaka 'mtu maarufu hausike ndiyo 'radar screen' zenu zianze kufanya kazi?

This is the read flag...bajaji na pikipiki kubeba abiria ni hatari kwa usalama wa raia. Serikali please tafuteni tiba ya usafiri na ajira Tanzania lakini hili la vibajaji ni hatari.
 
Ni hoja ya msingi. Mie naona kuruhusu Bajaj ni tatizo na si suluhisho la usafiri Jijini Dar.
 
Kama kawaida yetu ni wavivu kufikiri. Tunapenda "cheap and quick fix" solutions.

"Gridlock" ya magari inalinyemelea jiji la Dar. Ilitekelezwa "njia tatu" ikachemsha. Sasa inatekelezwa "askari kushinda barabarani". Hii nayo karibuni itachemsha. Soon Dar itakua kama Lagos na itabidi mji mkuu uhamishwe.

Vitu vya maana vya kuangalia ni kama Metro trains, subway trains, city buses (still on the drawing board after years), upanuzi na uboreshaji wa miundombinu (ringroads, feeder roads, backstreets, cycling and pedestrian lanes) na congestion charging.

Bajaj na pikipiki is just too cheap a fix.
 
Infact miji mikubwa karibia yote ya far east imepiga marufuku Bajaj na pikipiki kwasababu "inachafua" miji. Wametambua suala la msingi ni kuboresha public transport systems na infrastructure.

Ni India tu ndo wamezing'ang'ania kwasababu ndo wanaozitengeneza. Ona miji ya kihindi ilivyo "michafu" (kwa moshi na wingi wa vibajaji).
 
Back
Top Bottom