Serikali mulikeni haya matumizi ya energy drink!

Lombo

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
4,810
2,000
Nipo mkoa fulani kwa miezi kadhaa sasa.

Nimeshangazwa na matumizi makubwa ya energy drink, husasani kwa vijana. Kuanzia za Mo hadi Azam.

Sielewi chanzo cha matumizi haya ni nini. Nafikiri Serikali inatakiwa kuelimisha bayana madhara ya hivi vitu!

Jana nimesoma maelezo kwenye chupa moja kuwa "Usinywe kabla ya kwenda kulala, asitumie mama mjazito au anayenyoyesha, pili asitumie ambaye anadhuriwa na caffeine"

Zuio hili wataalamu wanatakiwa walitolee ufafanuzi. Mfano, nitajuaje ninadhuriwa na vitu vyenye caffeine.

Kwanza hiyo caffeine ni kitu gani? Cha ajabu maelezo yalimo kwenye vinywaji hivi yameandikwa kwa Kiingereza.

Inashangaza kidogo, lazima kuna kitu hapa!
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
5,993
2,000
Mkuu hivi vidude vinakufanya unakua addicted navyo. Mimi mwenyewe ni mhanga hapa napambana na uraibu wa kuacha kuvitumia. Nilianza kimasihara nikawa navitumia viniboost nisilale nikaishia kuwa navitumia hata mchana, leo siku ya tatu sijavitumia maana nimedhamiRia kuacha kabIsa maana kuna effects naziona kwenye afya yangu.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,545
2,000
Mkuu hivi vidude vinakufanya unakua addicted navyo Mimi mwenyewe ni mhanga hapa napambana na uraibu wa kuacha kuvitumia. Nilianza kimasihara nikawa na vitumia viniboost nisilale nikaishia kuwa navitumia hata mchana, leo siku ya tatu sijavitumia maana nimedhamilia kuacha kabsa maana Kuna effects naziona kwenye afya yangu
Effects zipi ndugu tueleze. Kwanza kampuni zote hizo mlizozitaja kuwa zinatengeneza mbona za Kiislam??? Nembo ya "Hallal" imetumika vibaya hapo. Poleni mnao falakatia kila kiwekwacho mbele yenu.
 

Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
1,055
2,000
Sasa mkuu mbona hoja yako inashangaza sana, serikali ifanye nini tena kuhusu energy drink ambazo zinatoa maelekezo ya matumizi yake, ukitaka kujua kama vitu vya caffein vinakudhuru kafanye check up, halafu kama zimeandikwa kiingereza hiyo lugha si inafundishwa tangu std one mkuu ndio ushindwe kung'amua hata vi maelezo baada ya kuisoma miaka saba pengine na zaidi? Unataka Energy drinks zipigwe marufuku au?
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,744
2,000
Tufahamisheni maana wengine sisi zinatusaidia hasa wakati wa kuendesha gari mwendo mrefu zaidi ya masaa 8, na inakata kweli (Fatigue) mradi zisizidi kopo 2
cc Nafaka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom