ryan riz
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 422
- 675
Yaani huu sasa unakuwa ni utoto na kufanyana wajinga. Mnaahidi kulipa malimbikizo yao ya madeni ya mishahara na fedha za likizo tena na kuwaletea fomu wajaze madai yao, ila cha kushangaza wakishajaza na kuwaletea mnawapotezea, viongozi wa kisiasa wa huko juu wakisharopoka huko kuhusu madai hayo, tena mnawaletea mafomu ya madai wanazijaza na kuwaambia haupiti mwezi kila mtu atapata haki yake, wakiwaletea mnawaachia vumbi miezi inaendelea kukata tu.
Yaani mtumishi hujikuta fomu za madai yale yale kajaza zaidi hata ya mara ishirini. Sasa sijui hizo fomu huwa mnazipeleka wapi mkishaletewa? Kulipa hamlipi na hata mkilipa kwenye halmashauri madai ya watu mia mbili mnalipa watu sita na kutangazia nchi nzima halmashauri fulani tumelipa madai ya wafanyakazi wetu wote, tena kwa mbwembwe kibao!
SIASA INAHARIBU NCHI HII KWA KWELI!