Serikali msiwafanye watumishi haya mnayowafanyia mara kwa mara

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
239
250
Yaani huu sasa unakuwa ni utoto na kufanyana wajinga. Mnaahidi kulipa malimbikizo yao ya madeni ya mishahara na fedha za likizo tena na kuwaletea fomu wajaze madai yao, ila cha kushangaza wakishajaza na kuwaletea mnawapotezea, viongozi wa kisiasa wa huko juu wakisharopoka huko kuhusu madai hayo, tena mnawaletea mafomu ya madai wanazijaza na kuwaambia haupiti mwezi kila mtu atapata haki yake, wakiwaletea mnawaachia vumbi miezi inaendelea kukata tu.

Yaani mtumishi hujikuta fomu za madai yale yale kajaza zaidi hata ya mara ishirini. Sasa sijui hizo fomu huwa mnazipeleka wapi mkishaletewa? Kulipa hamlipi na hata mkilipa kwenye halmashauri madai ya watu mia mbili mnalipa watu sita na kutangazia nchi nzima halmashauri fulani tumelipa madai ya wafanyakazi wetu wote, tena kwa mbwembwe kibao!

SIASA INAHARIBU NCHI HII KWA KWELI!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,572
2,000
Serikali ya awamu ya tano kwangu ni ya hovyo kupitiliza. Haiwezekani tangu mwaka 2015 mpaka leo hakuna cha kupanda daraja wala nyongeza ya mshahara!

Uongo umewajaa na visingizio lukuki huku vingi vikiwa havina kabisa uhusiano! Yaani Serikali ya CCM nitaichukia milele.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom