Zile pesa hakuna ubishi kuwa hazikuwa za mtu binafsi, hata ukigoogle ili upate tafsiri ya neno Escrow account, utapata tafsiri ya kuwa ni akaunti maalum inayofunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi pesa kutokana na pande mbili ambazo bado hazikubaliani na ukokotoaji wa gharama.
Kwa maana hiyo TANESCO walikuwa wanaweka kwenye akaunti hiyo kama capacity charge, ambapo ukokotoaji wa İPTL ulikuwa unabishaniwa na TANESCO kuwa ulikuwa ni bei ya 'kuruka'
Kwa maana hiyo pesa hizo zinakuwepo kwenye akaunti hiyo hadi hiyo dispute iwe resolved.
Kwa hiyo inashangaza sana kwa JK kuzikana pesa hizo za shirika lake la umma la TANESCO, kuwa pesa hizo siyo za umma!
Swali la msingi la kumuuliza JK, hivi kama kauli yake ya kuziita siyo za umma, imekuwaje pesa hizo za mtu binafsi Singa singa kama anavyodai, pesa hiyo ile 'vichwa' vya akina Werema, Maswi, Tibaijuka na 'kiporo' Muhongo hadi amelazimika kulitangaza baraza jipya la mawaziri muda mfupi uliopita?!