Serikali Msitudanganye Fedha za ESCROW ni za Umma

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,311
2,000
Wakuu naomba kuendelea kusisitiza kuwa tena kwa Kiswahili na maneno mepesi kabisa ili kila mtu aelewe, naona serikali na watu baadhi hapa wanapotosha sana.

Pesa za ESCROW zilihifadhiwa Benki Kuu na TANESCO ili kupisha na kusubiri uamuzi wa mahakama ya usuluhishi ya Uingereza juu ya tozo/gharama kubwa ambazo TANESCO ilikuwa inailipa IPTL, hivyo TANESCO ikalalamika.

Kabla ya uamuzi kutolewa na mahakama ya usuluhishi {ambapo tayari sasa umetoka} pesa hizo zikatolewa kinyemela.

PESA NI ZA UMMA AU SI ZA UMMA?

Sehemu ya pesa hizo zingekuwa za UMMA (TANESCO), IPTL, na TRA. Mahakama ya usuluhishi ingekubaliana na hoja kuwa ni kweli IPTL TANESCO gharama kubwa hivyo wakokotoe tena, basi TAIFA lingepata mgao wake hapo halali na IPTL ikapata mgao wake halali, TRA nayo ikapata mgao wake

Sasa tatizo nini?

wezi hawa hawakutaka kusubiri maamuzi ya mahakama ya usuluhishi hivyo baada ya kuwarubuni viongozi wa serikali nao wakarubunika kirahisi.
 

Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
606
500
Kwani mmesahau ya epa kila baada ya miaka 10 anapoingia Rais mpya lazima zitafutwe fedha looze ili zichotwe na kambi fulani ndani ya CCM. Kikwete atusaidie kulijua kambi hilo tulibwage wezi wakubwa, kuna pesa isiyo ya umma hapo, hata IPTL wapo ili kuhudumia umma, wao kuwa na pesa ni uwezo wa kutoa huduma nzuri zaidi. Acheni uongo wa mchana.
 

GOTILANGU

Senior Member
Aug 23, 2013
182
0
Naona kwa akili ya kawaida sana Tanesco ni kiwakilishi cha wananchi Tanzania na ni shirika la wananchi lilipewa madaraka ili kuwapatia nishati ya umeme Watanzania.
Kwanini Tanesco nishati ya umeme ni nishati muhimu sana na yenye soko kuwachia watu binafsi ni hatari sana.
Hivyo basi mkataba wowote wanaoingia Tanesco wanawakilisha wananchi au umma.
Hivyo pesa yoyote ya Tanesco ni ya wananchi au umma.Tanesco walipokuw wanahifadhi pesa pale tegeta escrow zilikuwa za umma maana akaunti ya escrow ilikuwa sio account ya kulipia bali ya dhamana.
Inakuwa ya IPTL inapotoka mikononi mwa Tanesco na kwenda IPTL hata kama ilikuwa akaunti ya pamoja ilikuwa kati ya iptl na tanesco lakn tanesco ndio waliokuwa wanalipa na iptl walistahili kutoa receipts baada kupata malipo.
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Ndiyo ZIMESHAPIGWA ndugu zangu,na kwa hulka ya Serikali yetu,issue imekwisha maisha yanaendelea as if hakuna kilichotokea.
 

nguvu za nyani

Senior Member
May 21, 2013
141
195
Fedha hizo ni za umma kwani iptl alikuwa hajalipwa bado akisubiri ukokotoaji kwa mujibu Wa amri ya mahakama.Ningependa wanaowania Uraisi watumie mud a huu kutoa misimamo yao kuhusu kadhia hii ni za umma au sio za umma ? Hii itasaidia kufahamu utawala ujao kama utaendeleza ufisadi au vipi
 

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,381
2,000
Yaani Mkuu umenena kitu ambacho badi hakiingii akilini kwangu pia. Je pesa hizi ni za umma au la? Kama ni za Umma Je JK alilidanganya taifa? Wako wapi Maprofesa wa siasa Tanzania watusaidie kuchambua hili
 

kyalankota

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
2,459
2,000
Yaani Mkuu umenena kitu ambacho badi hakiingii akilini kwangu pia. Je pesa hizi ni za umma au la? Kama ni za Umma Je JK alilidanganya taifa? Wako wapi Maprofesa wa siasa Tanzania watusaidie kuchambua hili
Utata mtupu mkuu na hakuna wa kuongea ukweli katika hili!
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,081
2,000
Hili sakata la Escrow bado bichi sana, wala Wakwere wenzie pale Ikulu waliopokea rushwa ya milioni 800 toka kwa Ruge lini na wao wanajiuzulu!? Wamelipa kodi kiasi gani kwa pesa zao haramu walizopokea!? Mama Wama naye kapokea bilioni 5 amelipa kodi kiasi gani? Majina ya wala rushwa waliopokea kupitia Stanbic mbona bado yanafanywa siri? Ruge na wanae nao wamelipa kodi kiasi gani!? Mbona DHAIFU anakuwa mzito kufanya maamuzi? Yeye ni mhusika Mkuu wa sakata la Escrow yeye naye ajiuzulu kwa kupokea rushwa toka kwa Ruge.
 

Olecranon

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,371
2,000
Kama si za umma kwa nini watuhumiwa wamejiuzulu, wengine kutimuliwa? Hatimaye baraza jipya kusukwa!
Ukijiuliza sana kuhusu yanayoendelea utaishia kuwa kama avatar yako. Hii nchi haina pilot na kama yupo basi anarusha Aibus 320 wakati ana uwezo wa kurusha Foker. Matokeo yake tumepotea kama ile ndege ya Malasyia. Mimi nilidhani mawaziri wangeteuliwa kwa nafasi zile zilizowazi, sasa hili la kubadilisha mawaziri kwenda wizara nyingine wakati muda uliobaki kabla ya uchaguzi ni kiduchu lina tija kweli? Ama kweli tunakazi kubwa.
 

ganda

JF-Expert Member
Nov 10, 2014
468
195
mwizi wa escrow ni yuleyule aliyesema hela siyo za umma, alidhani watu wanyamaza kwa uongo huo.
 

kyalankota

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
2,459
2,000
Ukijiuliza sana kuhusu yanayoendelea utaishia kuwa kama avatar yako. Hii nchi haina pilot na kama yupo basi anarusha Aibus 320 wakati ana uwezo wa kurusha Foker. Matokeo yake tumepotea kama ile ndege ya Malasyia. Mimi nilidhani mawaziri wangeteuliwa kwa nafasi zile zilizowazi, sasa hili la kubadilisha mawaziri kwenda wizara nyingine wakati muda uliobaki kabla ya uchaguzi ni kiduchu lina tija kweli? Ama kweli tunakazi kubwa.
Only in Tanzania!
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,952
2,000
Zile pesa hakuna ubishi kuwa hazikuwa za mtu binafsi, hata ukigoogle ili upate tafsiri ya neno Escrow account, utapata tafsiri ya kuwa ni akaunti maalum inayofunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi pesa kutokana na pande mbili ambazo bado hazikubaliani na ukokotoaji wa gharama.

Kwa maana hiyo TANESCO walikuwa wanaweka kwenye akaunti hiyo kama capacity charge, ambapo ukokotoaji wa İPTL ulikuwa unabishaniwa na TANESCO kuwa ulikuwa ni bei ya 'kuruka'

Kwa maana hiyo pesa hizo zinakuwepo kwenye akaunti hiyo hadi hiyo dispute iwe resolved.

Kwa hiyo inashangaza sana kwa JK kuzikana pesa hizo za shirika lake la umma la TANESCO, kuwa pesa hizo siyo za umma!

Swali la msingi la kumuuliza JK, hivi kama kauli yake ya kuziita siyo za umma, imekuwaje pesa hizo za mtu binafsi Singa singa kama anavyodai, pesa hiyo ile 'vichwa' vya akina Werema, Maswi, Tibaijuka na 'kiporo' Muhongo hadi amelazimika kulitangaza baraza jipya la mawaziri muda mfupi uliopita?!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom