Serikali mpya ya Syria ni mpango wa Urusi?

Nikilewa mniache

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
19,273
Reaction score
51,845
SIASASYRIA
Putin ampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria
Bakari Ubena
01.08.20251 Agosti 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea kwa mazungumzo Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al-Shibani na kumueleza dhamira ya Kremlin ya kuanzisha uhusiano na uongozi mpya wa nchi hiyo.

Siku ya Alhamisi, al-Shibani alikutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov na kumueleza kuwa serikali ya Damscus ingependelea kuiona Urusi ikiwa upande wao. Lavrov aliushuru utawala mpya wa Syria kwa hatua zake huku akielezea msimamo wa Moscow.

"Msimamo wetu wa kuunga mkono suala la kuendeleza ushirikiano na Jamhuri ya Kiarabu ya Syria ni thabiti na unalenga kuimarisha uhusiano wenye manufaa ya pande mbili. Msimamo huu hautegemei hali ya kisiasa au mabadiliko ya serikali lakini unatokana na desturi za muda mrefu za urafiki na kuheshimiana."

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa juu wa serikali mpya ya Syria tangu kupinduliwa mwezi Desemba mwaka jana kwa mshirika wa muda mrefu wa Urusi Bashar al-Assad.

Najiiliza nini kinaendelea Syria sababu utawala wa sasa uliingia kwa mbwembwe ukiegemea upande wa marekani na washirika wake lakini baada ya kuona Israel inawashambulia hovyohovyo naona wanataka kuomba msaada Urusi kama serikali iliyoondolewa madarakani
 
Unafiki wa marekani na washirika wake unazidi kujulikana hadi kwa washirika wake.

Israel iliwashambulia sana wakati wao ndio walisaidia kuondoa utawala wa Asad uliokua mwiba kwa marekani na Israel
Urusi ikirudi Syria na Iran itarudi kuendelea kupambana na utawala haramu wa Israel. Je, Israel haioni kuwashambulia hawa jamaa ndio kumepelekea waanze kuungana na Iran pamoja na Urusi? Hesabu yao ni ipi?
 
Wao ni binadamu kama ww .wanakosea hesabu hio ni kawaida.
Tatizo watu wamejiekea kitu kua Israel ndio number moja Kila kitu hawaezi shindwa kumbe mambo ni tofaut
Binadamu wote ni sawa

Urusi ikirudi Syria na Iran itarudi kuendelea kupambana na utawala haramu wa Israel. Je, Israel haioni kuwashambulia hawa jamaa ndio kumepelekea waanze kuungana na Iran pamoja na Urusi? Hesabu yao ni ipi?
 
SIASASYRIA
Putin ampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria
Bakari Ubena
01.08.20251 Agosti 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea kwa mazungumzo Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al-Shibani na kumueleza dhamira ya Kremlin ya kuanzisha uhusiano na uongozi mpya wa nchi hiyo.

Siku ya Alhamisi, al-Shibani alikutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov na kumueleza kuwa serikali ya Damscus ingependelea kuiona Urusi ikiwa upande wao. Lavrov aliushuru utawala mpya wa Syria kwa hatua zake huku akielezea msimamo wa Moscow.

"Msimamo wetu wa kuunga mkono suala la kuendeleza ushirikiano na Jamhuri ya Kiarabu ya Syria ni thabiti na unalenga kuimarisha uhusiano wenye manufaa ya pande mbili. Msimamo huu hautegemei hali ya kisiasa au mabadiliko ya serikali lakini unatokana na desturi za muda mrefu za urafiki na kuheshimiana."

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa juu wa serikali mpya ya Syria tangu kupinduliwa mwezi Desemba mwaka jana kwa mshirika wa muda mrefu wa Urusi Bashar al-Assad.

Najiiliza nini kinaendelea Syria sababu utawala wa sasa uliingia kwa mbwembwe ukiegemea upande wa marekani na washirika wake lakini baada ya kuona Israel inawashambulia hovyohovyo naona wanataka kuomba msaada Urusi kama serikali iliyoondolewa madarakani
Hapo ndipo napoonaga kuwa Israel na USA ni kama wanakurupuka kwenye mahesabu.
Syria ilishakubali kuungana nao mkono,ila kitendo cha kulipua makao ya jeshi ndani ya Damascus aisee hata awe rais kichaa kwa kiasi gani hawezi kubaliana na hili.
Na kama Syria imeenda Kremlin basi tutarajie na Iran kurejesha kambi Syria kwa namna yeyote .
 
Inashangaza kweli
 
Ni kweli mkuu ila huu utawala mpya uliingia kwa mbwembwe ukiiunga mkono marekani huku ukiitosa urusi..
Nini kimeukumba huu utawala hadi kutuma waziri wa mambo ya nje kwenda kupiga goti Urusi?
Kuna mdau alisema viongozi wa syria wana asili ya urusi,kuanzia wakati huo bashar al assad na wengine walokua karibu yake,uenda mbegu ya urusi imeenea sana uko Syria na ndo maana huyu katembelea huko.
 
Urusi ni mshirika asie mnafiki kama marekani
We hata mkoa wa morogoro ujaelewa historia yake.Alafu unakuja kujibu majibu ya kahawa ya mpira kufikiria urusi kama unavyojua .Unafahamu alicho sababisha kwa bashiri huko.
 
Kuna mdau alisema viongozi wa syria wana asili ya urusi,kuanzia wakati huo bashar al assad na wengine walokua karibu yake,uenda mbegu ya urusi imeenea sana uko Syria na ndo maana huyu katembelea huko.
Wewe vipi mbona unaongea kama mlevi.? Mwarabu lini kawa na asili na mzungu. Wabongo elimu ndogo.
 
Urusi ikirudi Syria na Iran itarudi kuendelea kupambana na utawala haramu wa Israel. Je, Israel haioni kuwashambulia hawa jamaa ndio kumepelekea waanze kuungana na Iran pamoja na Urusi? Hesabu yao ni ipi?
Israel anatamani sana Urusi aendelee kuwepo Syria, na inasemwa ndiye aliweka pressure kwa utawala mpya usiwafukuze warusi kwenye ardhi ya Syria!
unajua kwanini?

Israel anajua ikitokea Urusi akaondoka mazima pale Syria, basi waarabu watakua na nguvu zaidi, na Turkey atazidi kumsogelea yeye (Israel) i.e ushawishi wa Turkey utakua mkubwa sana, sasa ili kubalance nguvu za turkey ni lazima awepo Russia!

NB/
Russia ni mshirika muhimu zaidi kwa Israel pengine kuliko US, hasa ukiongelea siasa za ME........... ni rahisi Israel kumwomna Russia awasaidie kupunguza vurugu za Iran na kudhibiti nguvu ya turkey (maana hao wote turkey na Iran, Russia ana ushirika nao wa karibu kuliko US)...... na hii ndio inaitwa geopolitics!

ukizungumzia geopolitics katika uhusiano wa kimataifa, ni sawa na unazungumzia umafia kwenye biashara za mafuta!.......geopolitics ni somo muhimu na very complicated kwenye international relation hasa kwa sababu kuna mwingiliano wa maslahi mkubwa sana baina ya maadui......
 
Israel anatamani sana Urusi aendelee kuwepo Syria, na inasemwa ndiye aliweka pressure kwa utawala mpya usiwafukuze warusi kwenye ardhi ya Syria!
unajua kwanini?

Israel anajua ikitokea Urusi akaondoka mazima pale Syria, basi waarabu watakua na nguvu zaidi, na Turkey atazidi kumsogelea yeye (Israel) i.e ushawishi wa Turkey utakua mkubwa sana, sasa ili kubalance nguvu za turkey ni lazima awepo Russia!

NB/
Russia ni mshirika muhimu zaidi kwa Israel pengine kuliko US, hasa ukiongelea siasa za ME........... ni rahisi Israel kumwomna Russia awasaidie kupunguza vurugu za Iran na kudhibiti nguvu ya turkey (maana hao wote turkey na Iran, Russia ana ushirika nao wa karibu kuliko US)...... na hii ndio inaitwa geopolitics!

ukizungumzia geopolitics katika uhusiano wa kimataifa, ni sawa na unazungumzia umafia kwenye biashara za mafuta!.......geopolitics ni somo muhimu na very complicated kwenye international relation hasa kwa sababu kuna mwingiliano wa maslahi mkubwa sana baina ya maadui.....
Aloo
 
Hapo ndipo napoonaga kuwa Israel na USA ni kama wanakurupuka kwenye mahesabu.
Syria ilishakubali kuungana nao mkono,ila kitendo cha kulipua makao ya jeshi ndani ya Damascus aisee hata awe rais kichaa kwa kiasi gani hawezi kubaliana na hili.
Na kama Syria imeenda Kremlin basi tutarajie na Iran kurejesha kambi Syria kwa namna yeyote .
Kwani unafikiri Israel na US hawajui matokeo ya wanacho fanya hapo.

Wao wanamtafuta Russia tu aingie vitan kiaina na hao droze Ili wapigane indirect kupitia hao droze.

Irani akijichanganya naepia ndio lengolao.
Wanatengeneza vita wakiwa na plan A,B,C,na kuendelea.

Wanataka kuwaweka bz Russia na Irani.
 
Back
Top Bottom