Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Serikali ya Tanzania imesema mazungumzo yanaendelea kati yake na Serikali ya Kenya kuhusu kuzuiwa kwa mahindi katika mpaka wa Namanga.
Zuio la mahindi kutoka Tanzania lilitolewa Machi 5 2021na Mamlaka ya Kilimo na Chakula ya nchini Kenya ikidai kuwepo kwa sumu kuvu katika mahindi yanayotoka Tanzania na Uganda.
Akizungumza jijini Dodoma leo Jumatatu Machi 8, 2021 msemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas amesema hadi sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu kukataliwa kwa mahindi kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya zaidi ya kikaratasi ambacho kimeonekana kwenye mtandao.
“Ni kweli mahindi ya Tanzania yamezuiwa kwenye mpaka wa Namanga lakini Hororo yanapita na mipaka mingine yanaendelea kupita sasa katika hali kama hiyo sisi Serikali kwa Serikali lazima tuzungumze,” amesema.
Amesema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na mazungumzo yanaendelea kati ya pande hizo mbili.
“Kwa nini katika mpaka wa Hororo mahindi kutoka nchini yanapita lakini Namanga yamezuiwa,” amehoji Dk Abbas.
Mwananchi