Asalaam alekyum wana ukumbi!
Jana nimeshuhudia walimu mbalimbali wilaya ya Nyamagana wakipaza sauti zao kwa pamoja; kupinga makato ya sh 10,000/= kwenye mishahara yao kwa lengo la kujenga maabara sekondari.
Kujenga maabara ni jambo jema sana tena sana! Lakini kitendo cha kukata pesa bila kuwashirikisha walimu ni uonevu na ukiukwaji na utawala wa kisheria.
Mbona pesa za kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba hazikuleta shida zilipatikana na mabilioni yaliteketea Dodoma? Kwa nini serikali isitafute pesa kama ilivyofanya kwenye bunge la katiba ili maabara zijengwe? Inakuwaje mtumie ubabe kwa njia kandamizi wakati wachache ndiyo wanafaidi keki ya Taifa walio wengi wanaumia!
Ukienda vijijini wananchi wanakamatwa eti hawakwenda kwenye maendeleo ya shule za kata na ujenzi wa maabara; hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila raia mpenda haki; na maendeleo, kwani ccm wanatumia nguvu za wanyonge kujinufaisha wenyewe.
Nawaomba msiwanyanyase walimu laana itawaumbua nyie wote mlio shika madaraka! Kwa nini hamkuwakata wajumbe wa bunge la katiba! badala yake wakatwe watumishi wa umma wakiwemo walimu ambao mishahara yao inaishia kwenye kulipa riba kwenye mabenki?
Watanzania acheni kulala usingizi fanyeni maamuzi magumu! Hii ni vita pambaneni haki itendeke kwani pesa zinatumika vibaya hili halikubariki.
Chanzo taarifa ya habari ITV.
Kichwa cha post yako ni kinzuri "
serikali mnawanyonga walimu" lakini kimanti ingekuwa "
serikali inajinyonga yenyewe endapo tu serikali inamaana ya watu (wananchi) hata hivyo ina maana pale tu wananchi wana maamuzi lakini kwa nchi yetu serikali ni "
mchwa" huu ni msamiati mpya kutoka kwa mkuu wa kaya aliyoitoa wiki iliyopita akimaanisha watumishi wa serikali ambao ni serikali yenyewe. Sasa neno "Mchwa" lina maana nyingi kwakuanza tu hawa sio watu ni "
wadudu"
.............. endelea na nyingine.
Kimsingi hata kumshirikisha tu mwalimu kukatwa mshahara wake ilikuchangia ujenzi wa maabara ni kosa kwani walimu kama raia wengine wa nchi hii wana mitaa yao hivyo walitakiwa kupitia serikali za mitaa yao wachangishwe kama wananchi wengine. Tambua hata kama watashirikishwa walivyowanyonge wangeweza kukubali hata kama hawapendi kwani wengi wao ni waoga hata kwenye haki zao.
Wa kulamiwa na kulaniwa ni yule aliyetoa tu wazo an wote waliosapoti na wanaoendelea kusapoti kwani jambo hili lina madhara makubwa kuliko hata kawaida. Busara ya walimu na silaha yao kuu kwa miaka ya hivi karibuni ni migomo baridi (passive resistance) ambayo hata hivyo wanaoumia ni masikini wenzao na wenyewe. Hasira za walimu zitaishia kutofundisha, je madhara yatakuwa kwa nini? Kimsingi suala hili haliwahusu walimu tu japo wao ndiyo waathirika wa mojakwamoja lakini sisi masikini ni waathirika wa pili ambao ndio tutakao pata madhara makubwa.
Watanzania tunapaswa tusilifumbie macho jambo kama hili kwani lina madhara makubwa. Hivi watanzania wenzangu, tumesema Richmond, EPA, Katiba ni jambo la wanasiasa(UKAWA) Mwangosi, ulimboka ya waandishi wa habari, kubomolewa nyumba ya wale wanaojenga barabarani, kunyang'anywa viwanja kwa wasiojua sheria, kukatwa mishahara la walimu, sasa lipi la kitaifa?, lipi litatokea sisi watanzania tutasema hiki ni kilio cha wote??. Nahisi kama tanzania sio "
Taifa?"
"Kwa mwanaume mwenye akili timamu hatapenda hata kushirikishwa kama mwanaume mwenzake anapenda wawe na uhusiano wa kingono kwani jambo lenyewe tu ni baya"