Serikali mnawanyonga Walimu!

Mwaka huu BRN itapeleka mpaka div 60. Ndo mkakati wa sasa. Jipange waalimu kwq matokeo makubwa sasa bila big salary ghafla. Oyeerrrrr waalimu.
 
Watu mnahasira sana! Tuwaombee walimu jamani wainusuru nchi yetu kwani wao wakiamua changes will come!

Karumbeta ndugu yangu, siyo hasira aisee. Mi naomba nitofautiane Na wewe kuhusu suala la kuwaombea. Naomba tusimhusishe Mungu katika hali hii tunayoiona kwa waalimu.
Maarifa wanayo lakini hawataki kuyatumia, hata Kama wamefungwa akili sisi tunaoona tunwaambia wabadilike hawataki. Sisi tutasemaje Karumbeta? Mungu alishawafanya wakawa wengi, silaha ambayo hutumika kufanya mazuri Na mabaya (rejea katiba mpya). Nao basi watumie huo wingi wao wafanye kitu cha kuwakomboa.
 
Naam naam!! Nakubaliana na wewe bila chenga ndugu! Walimu wamuunge mkono mwalimu Nyerere haya wanayofanya ccm hasa katiba mpya hayafai hata kidogo! Walimu wanatuangusha naunga mkono hoja yako.
 
Acha wakatwe hata hiyo hela ni kidogo sana, walimu wengi ni wajinga ukubali au ukatae habari ndio hiyo kwani na mimi nilikua mwalimu kwa miaka miwili nilijionea mwenyewe ujunga wa walimu japo wamesomea lakini usomi wao walio wengi ni bure, kwanza hawajiamini hata kidogo hata mfagiaji wa ofisi ya mkurugenzi anawatisha mpaka wanapiga magoti walimu wenye degree zao. Kuwa mwalimu inakubidi uwe mjinga wa kupitiliza vinginevyo kazi itakushinda kama sisi tulivyoamua kuacha kazi tukaja mtaani ku burn CD. Ualimu ndio kazi ya mwisho kabisa ambayo kila mtumishi anajifunzia kutoa makaripio na kupiga biti. Acha walimu wakome kwanza ndio siku moja watajua nini maaana kuikataa CCM
 
Hii nchi kwa kweli inashangaza sana, kwann hiyo fedha ya kujenga maabara za shule za sekondari wasikatwe wale wajumbe waliopitisha rasimu ya katiba mpya kwa mabavu!!!! kwani yale mabilioni yaliyoteketea kule dodoma kwenye mchakato wa bmk yalitoka wapi!!!! mbona hatukuchangishwa wananchi wote manake ile katiba ni ya wananchi wote wa tanzania, kwani hizo maabara watakaofaidika nazo ni watoto wa walimu tu!!! huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa walimu wa tanzania na watumishi wote..
 
hii serikali ya CCM wanachosema na wanachofanya huwa havilandani hata kidogo

"machoni kama watu"
 
Ngugu! Ni hatariii!! Ungeona jana mama mmoja (mwalimu) alipokuwa akipaza sauti akitoa machozi ungelia ndugu! Tuwe na busara katika kufanya maamuzi hii ni nchi yetu sote tusikubali hata kidogo.

mdau hili suala linazungumzika,hakuna sheria inayolazimisha mtu kuchangia hii kitu,huyo mama analia bure tu yeye aende mahakaman,halafu naona CWT wapo kimyaaa kwenye hili
 
Mtwara manispaa walimu wanalazimishwa kuchanga
30,000 ya maabala.
13,000 ya mwenge
5,000 mfuko wa Elimu. HII NDIO SERIKALI SKIVU DUNIANI

Halafu kule Morogoro kuna watumishi wapo kwa kama wiki tatu sasa kwenye michezo, hivyo hizo pesa wanazolipana posho sizingepelekwa kwenye ujenzi wa maabara? kuna mchezo gani hapa unachezwa na serikali?
 
hao ni walim wa wapi hao???
 
ni kweli, mtaji wa CCM siku zote ni kwa watu wasiojielewa kama hawa - CCM hawana makosa acheni wawatumia wanavyotaka.
 
mdau hili suala linazungumzika,hakuna sheria inayolazimisha mtu kuchangia hii kitu,huyo mama analia bure tu yeye aende mahakaman,halafu naona CWT wapo kimyaaa kwenye hili

CWT Hawana lolote wanakula pesa za walimu bure nakujilimbikizia mali tena kama ni ufisadi uko CWT. wanaopaswa kwenda mahakani ni CWT na wala siyo mwalimu aliyelia upo hapo ndugu! Walimu amkeni
 
Mod, heading yangu hukuitendea haki! Serikali=ccm
 
walimu kwa kujitolea wanatupa elimu

walimu kwa kujitolea wanakuwa wazazi/walezi wetu

walimu hawahawa tunawatukana, tunawanyanyasa na bado wanajitolea kunyamaza

sasa hata kamsahara kao kadogo tunakatamani.....

Mungu tuepushie hii laana
 
Mwaka huu BRN itapeleka mpaka div 60. Ndo mkakati wa sasa. Jipange waalimu kwq matokeo makubwa sasa bila big salary ghafla. Oyeerrrrr waalimu.

BRN ni mpango wa kupiga pesa ya uchaguzi hakuna jipya!!
 
Hii nchi kwa kweli inashangaza sana, kwann hiyo fedha ya kujenga maabara za shule za sekondari wasikatwe wale wajumbe waliopitisha rasimu ya katiba mpya kwa mabavu!!!! kwani yale mabilioni yaliyoteketea kule dodoma kwenye mchakato wa bmk yalitoka wapi!!!! mbona hatukuchangishwa wananchi wote manake ile katiba ni ya wananchi wote wa tanzania, kwani hizo maabara watakaofaidika nazo ni watoto wa walimu tu!!! huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa walimu wa tanzania na watumishi wote..
 
Eti mkuu! Mimi nasikitika sana nchi hii mambo ya elimu ni "non priority" wala hakuna anaye jali lakini kwenye kulipana posho za BMK rais anaongeza siku na pesa zinakipwa wala hakuna anaye hoji! Tumevumilia sasa basi!
 
Kaka nakuunga mkono juu ya hii hoja yako,walimu bado sana tuna kawaida ya kugeukana wenyewe kwa wenyewe ni upuuzi mtupu yani watu tunapanga harakati za maana baada ya lisaa una kuta taarifa ishafika kwa mabosi.sasa huku sijui ni kujipendekeza ama ni ujinga ***** sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…