Serikali mbona kimya shule binafsi?

Salas

JF-Expert Member
Feb 15, 2009
382
82
Katika hali ya kustaajabisha jipu tambazi la ada za private school limeshindikana kutumbuliwa.

Huu ni mwanzo mbaya au dalili za kuanza kushindwa kwa kasi ya mabadiliko ya kudandia. Serikali ilijipambanua Ifikapo December 15 wangekuja na Muongozo lakini hakuna kitu.

Hakika mabadiliko bado sana huu ni mwanzo huenda na sekta nyingine wakaendelea kuitisha serikali.
 
Mkubwa akiona mahala umekosea unajirudi taratibu, siyo mpaka uambiwe.
 
Katika hali ya kustaajabisha jipu tambazi la ada za private school limeshindikana kutumbuliwa. Huu ni mwanzo mbaya au dalili za kuanza kushindwa kwa kasi ya mabadiliko ya kudandia. Serikali ilijipambanua Ifikapo December 15 wangekuja na Muongozo lakini hakuna kitu. Hakika mabadiliko bado sana huu ni mwanzo huenda na sekta nyingine wakaendelea kuitisha serikali.

Aliyetoa tamko hakushirikisha wadau na kufanya utafiti wa kina juu ya ada stahiki katika kipindi hiki.sasa hivi wakaguzi wanapita mashuleni kupata takwimu za ada zinazotozwa.
pia katika uchumi ambao serikali imeachia wafanyabiashara watoe huduma na serikali itoze kodi unapaswa ufikirie sana kuja na bei elekezi.
pia kuna shule za kimataifa zinazomilikiwa na wawekezaji toka nje mfano Ist ipo toka enzi za NYERERE ada ni tofauti na shule zingine na zipo mikoa mingi kwaajiri ya kusomesha watoto wa viongozi na wawekezaji.unaanzeje kuwapangia ada wakati waalimu wao wengi ni expert na mitaala wanayotumia na resources zao zote za nje?
 
Hivi mtoto akiwa nyumbani unaweza kumlisha na kumpatia malazi kwa 350,000 kwa mwaka?

Ikumbukwe kuwa Serikali inapeleka kwenye shule zake za bweni zaidi ya 3m kwa mwanafunzi.
 
Ripoti ya wakaguzi iliyoteuriwa na serikali kufanya utafiti Wa kina juu ya ada stahiki inakabidhiwa Leo. Ajabu mleta uzi Unakuja na majibu yako.
 
Kwa maoni yangu ni kuwa shule za binafsi ni kama biashara nyingine tu.. Serikali iboreshe shule zake ili wazazi wawe na uchaguzi wapi wawapeleke watoto wao! Ikiwa hivyo ada za shule binafsi zitashuka kabisa na hata shule nyingine kufa!
 
hao ni wachan?giaji wakuu wa ccm huwawezi they are so powerful ndio wezi wa paper
 
Hivi mtoto akiwa nyumbani unaweza kumlisha na kumpatia malazi kwa 350,000 kwa mwaka?

Ikumbukwe kuwa Serikali inapeleka kwenye shule zake za bweni zaidi ya 3m kwa mwanafunzi.
hzi taarifa has a za parandesi ya pili hazina hats chembe ya ukweli. Pitia chanzo chako
 
Hivi mtoto akiwa nyumbani unaweza kumlisha na kumpatia malazi kwa 350,000 kwa mwaka?

Ikumbukwe kuwa Serikali inapeleka kwenye shule zake za bweni zaidi ya 3m kwa mwanafunzi.

3m kwa mwanafunzi...!? Nijuavo mimi serikali inatoa wastani wa tsh.1500/= kwa siku Mwanafunz. Chakula,umeme,maji ni humohumo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom