Serikali: Marufuku watoto wa chekechea kuvaa majoho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali: Marufuku watoto wa chekechea kuvaa majoho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpalu, Sep 6, 2011.

 1. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,492
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  SERIKALI imewaagiza wamiliki wa shule binafsi za msingi na sekondari kote nchini, waache kuwavalisha majoho na kofia, wahitimu wa elimu wa ngazi hiyo kwa sababu kitendo hicho kinadhalilisha vazi hilo linalotumiwa na wahitimu wa elimu ya juu Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Ofisa Elimu, Idara ya Elimu ya Msingi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Donald Pambe, alipokuwa akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mazoezi ya Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

  “Hii ni dhana potofu ambayo kimsingi inalidhalilisha vazi hilo lenye heshima kubwa kwa wahitimu wa elimu ya juu,” alisema Pambe ambaye katika sherehe hiyo, alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamis Lihenga. Alisema tabia ya kuwavalisha majoho na kofia wahitimu wa elimu ya awali na msingi ni ghiliba inayofanywa na wamiliki wa shule hizo, ili kuvutia biashara zao.

  Pambe alisema elimu bora si mtoto kuvalishwa majoho, bali ni uchapakazi wa walimu katika kuwajenga watoto kitaaluma. “Ebu igeni mfano wa Shule ya Msingi Mazoezi Chang’ombe, wanafunzi wao wamevaa kawaida na wanapendeza kweli, hii inanipa imani kuwa wote watafaulu mitihani yao,” alisema Pambe.

  Pia aliwaagiza viongozi wa shule zote nchini zinazomilikiwa na serikali, kuanzisaha utaratibu wa midahalo ya Kiingereza ili kuwajengea uwezo wanafunzi wao kuhusu kuzungumza lugha hiyo kwa kujiamini.

  Alisema hilo litasaidia kuwashawishi wazazi kuzipenda shule za serikali badala ya kuwakimbizia watoto wao katiki shule za watu binafsi zinazofundisha kwa kutumia lugha hiyo

  “Leo tumeona jinsi wanafunzi wa shule hii walivyoendesha mdahalo kwa Kiingereza tena bila kujikwaa ulimini, kuna sababu gani ya kupeleka mtoto na kulipa fedha nyingi eti mwanao ajue kingereza, hizi nijitihada binafsi za walimu wa Chang’ombe ,basi walimu wote nchini waige mfano huu na midahalo ianze mara moja,” alisema Pambe.

  Akijibu hoja kuhusu serikali kuzuia michango shuleni, alisema suala hilo linaingiliwa na siasa na kwamba michango inaruhusiwa baada ya kamati ya shule kupanga jinsi ya kuiletea maendeleo shule.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Groria Mtenga, alisema katika shule yake jumla ya watoto 131, wanatarajia kufanya mtihani wa taifa wa kumaliza darasa la saba kesho na keshokutwa.

  “Wanafunzi wetu tumewaandaa vizuri na tunatarajia watafanya vizuri ili tuendeleze historia yetu ya shule ya Msingi ya Mazoezi Chang’ombe kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa,” alisema Mtenga. MWISHO
  source;mwananchi
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Majoho yanadhalilisha Elimu ya Juu yakitumiwa na watoto wa chekechea!?

  HOW!?
   
 3. C

  CLEMENCY JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Sasa naona tutaambiwa tusipewe zawadi za suti!
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  I find it tacky for nursery and primary school kids to wear them gowns

  But making a specific regular against that ......I don't know
   
Loading...