Serikali: Marufuku madereva na abiria kuchimba dawa (kujisaidia porini)

Mimi niiijuavyo kwenye treni ya reli ya kati wakati unajisaidia kwenye "choo"ambacho kinyesi kinadondoka relini,

Halafu anakuja huyu waziri baada kufikiri usiku kucha huu uharo nduo anakuja kutumwagia

Kuna watu tumbo la kuhara linamsumbua au ana kisukari anakojoa kila mara.....hii miwaziri mingine na huyo anaewachagua wametoka mapangoni ni baadhi ya vizazi vilivyobakizwa kutoka katika zana za kale za mawe.
 
Hao hawajui haja, kama vipi magari yawe na vyoo.

Maana barabara nyingi vyoo vipo kilomita zaidi ya 200 sasa hili si ni jaribu lingine kwa abiria wanaohara.
Hii si sawa Kabisa...yaani hii serikali sijui ya wapi hii,
Leo Ninatoka Dar kwenda Mwanza na Dar lux,tumefika Morogoro tumeomba kuchimba Dawa sawa,Baada ya hapo Wakasema Dodoma,kufika Dodoma Km zaidi ya 300km wanasema hapa Dom hamna mpaka Bahi,sawa baada ya Bahi Ni Mpaka Mwanza,kiss wanasema Sehemu nyingine hakuna Sehemu za Kuchimba Dawa, na Pia wana haraka!
Jamani,lazima Serikali wajipange Say kila Stand ya Mkoa ni Muhimu watu wachimbe Dawa Au Km 200.
LA sivyo watatuua vibofu vyetu,halafu soda maji wanagawa Sasa Utatolea wapi Output!
Matamko Mengine bana!
 
Badala ya kuja na wazo kama kujenga public toilets kila baada ya kama kilomita 20 au kuendelea wanakuja na vitamko tu.
 
Huyu msomi ameshuka toka sayari gani leo?

Huyu ni daktari, amezaliwa, kakulia hapa hapa na amesoma kwenye shule za hapa hapa nyumbani. Na sio ajabu bado anao ndugu zake kule vijijini, ambako pengine hata vyoo wanavisikia na kuvisoma magazetini au vitabuni.

Kwa hiyo msomi wetu huyu anaelewa kila kitu kuhusu hali ya jamii na mazingira hapa yalivyo.
Kwenye hayo maneno aliyoripotiwa kuyasema, sikuona popote alipotoa ushauri wa kuondoa matatizo ya swala analolizungumzia; yeye anatoa amri tu basi.

Je amezungumza na wajenzi wa barabara kuu au hata wizara ya ujenzi ili tatizo hilo liondolewe kwa kuweka vituo maalumu vya mapumziko katika barabara hizo?

Kwa hiyo leo katibu mkuu wa wizara kafanya kazi kubwa. Amesikika na kuandikwa kwenye vyombo vya habari, hata kama hakuna lolote la maana alilolifanyia kazi.
Ko unatakaa,serikali iwajengee vyoo misituni.labda serikali ya ufipa.kaungane na mboye
 
Ko unatakaa,serikali iwajengee vyoo misituni.labda serikali ya ufipa.kaungane na mboye
Wewe nakuacha na ujinga wako uendelee kukutafuna, kwa sababu hakuna unalolijua ktika dunia ya leo.
Sasa shukuru sana kwa kukujibu, kwa sababu hustahili jibu lolote.
 
Back
Top Bottom