Serikali: Marufuku madereva na abiria kuchimba dawa (kujisaidia porini)

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1542828257565.png
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa neno mbele ya Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Madereva wa mabasi yaendayo mikoani na abiria wametakiwa kuacha tabia ya kujisaidia

“Kuchimba dawa” katika maeneo yasiyo rasmi ili kutunza na kuepuka uharibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja kusababisha magonjwa ya milipuko.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua mkutano unaojumuisha Maafisa Afya kutoka mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini pamoja na wadau wa mazingira, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dkt. Mpoki amekemea tabia hiyo hatarishi kwa ustawi wa mazingira huku akiwataka maafisa Afya na wadau wa mazingira nchini kusimamia afua zilizowekwa zinaendelea kutekelezwa ili kulinda mazingira ambayo yanatuzunguka.

“Kuna watu wengine nimeshawahi kuwaona kwenye basi wanatupa taka ovyo na mabasi mengine yanasimama porini ili abiria wajisaidie, hii tabia siyo nzuri na inatakiwa ikemewe kwa nguvu zote, Idara ya Kinga Pamoja na wadau wao wanakuja na mpango mkakati wa kuondoa kabisa dhana ya watu kusimama kujisaidia porini, “sisi tunatakiwa kuwa msitari wa mbele kupiga marufuku mabasi kusafiri bila kuchafua mazingira”.

Dkt. Mpoki amesema ni aibu kubwa kwa taifa kuona watu hawafuati kanuni za usafi huku akiwataka Maafisa Afya kuhakikisha wanafanya kazi kwa nguvu ili ionekane kuwa kero kwa watu wengine na watakaobainika kuchafua mazingira wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.

Aidha, Dkt. Mpoki ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuzingatia matumizi ya vyoo bora na kunawa mikono mara baada ya kujisaidia ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kusababishwa na tabia ya uchafu ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kujisaidia ovyo porini ili kaulimbiu ya “Nyumba ni Choo” iweze kutekelezwa ipasavyo kwa kujenga vyoo vya kisasa katika maeneo mbalimbali ili huduma ipatikane mahala pote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema takwimu zinaonesha kaya zilizokua na vyoo bora mwaka 2012 zilikua asilimia 19.5 lakini hivi sasa nchi nzima kaya zenye vyoo bora ni asilimia 51.4.

Dkt. Subi amesema kutokana na takwimu hiyo inaonesha kuna mafanikio katika uhamasishaji kwa jamii kutumia vyoo bora na kuacha kutumia vyoo ambavyo havina viwango na salama kwa matumizi, na badala yake serikali inaendelea kutoa elimu na kusisitiza jamii kutumia vyoo bora ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuzuilika ikiwemo kipindupindu, magonjwa ya tumbo na kuhara.

Pamoja na hayo, maafisa Afya wametakiwa kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma, kuhamasisha usafi wa mazingira na kufikia maeneo ya mazalia ya vimelea vya ugonjwa wa Malaria ili kutokomeza ugonjwa huo ambao umekua hatari kwa jamii hasa kwa wanawake wajawazito na watoto.

Mkutano huo unaojumuisha Maafisa wa Afya nchi nzima una lengo la kutoa elimu na kubadilishana uzoefu wa kufanya kazi lakini msisitizo mkubwa ikiwa ni utunzaji wa mazingira na kuzingatia kanuni bora za afya pamoja na usafi wa mazingira na usafi na afya ya binadamu.
 
Hatarii Magugu Mdori Minjingu njia tamu sana ila twiga nusra aniletee tabu na gari mitaa ya Mdori mpaka nafika kisongo ndo nakagua gari maana sikuamini ile manuever ilipiga
 
Waache zao bwana, mie nishazoea wakati wa kuchimba dawa nashuka kujionea papuchi za aina mbalimbali asee....KE hawanaga aibu kabisa panapo haja teh!teh
 
Hao hawajui haja, kama vipi magari yawe na vyoo.

Maana barabara nyingi vyoo vipo kilomita zaidi ya 200 sasa hili si ni jaribu lingine kwa abiria wanaohara.
Hawa ni wataalamu na wanawajibika kusema ili hatimaye mamlaka husika kwa kushirikia na sekta binafsi wachukue hatua. Kiukweli hali ni ngumu na ukiwa safarini kuna nyakati huwezi kuzuia haja ya kujisaidia eti mpaka ufike mahali kuna choo cha umma!
 
Dkt. Mpoki amekemea tabia hiyo hatarishi kwa ustawi wa mazingira huku akiwataka maafisa Afya na wadau wa mazingira nchini kusimamia afua zilizowekwa zinaendelea kutekelezwa ili kulinda mazingira ambayo yanatuzunguka.

“Kuna watu wengine nimeshawahi kuwaona kwenye basi wanatupa taka ovyo na mabasi mengine yanasimama porini ili abiria wajisaidie, hii tabia siyo nzuri na inatakiwa ikemewe kwa nguvu zote, Idara ya Kinga Pamoja na wadau wao wanakuja na mpango mkakati wa kuondoa kabisa dhana ya watu kusimama kujisaidia porini, “sisi tunatakiwa kuwa msitari wa mbele kupiga marufuku mabasi kusafiri bila kuchafua mazingira”.

Huyu msomi ameshuka toka sayari gani leo?

Huyu ni daktari, amezaliwa, kakulia hapa hapa na amesoma kwenye shule za hapa hapa nyumbani. Na sio ajabu bado anao ndugu zake kule vijijini, ambako pengine hata vyoo wanavisikia na kuvisoma magazetini au vitabuni.

Kwa hiyo msomi wetu huyu anaelewa kila kitu kuhusu hali ya jamii na mazingira hapa yalivyo.
Kwenye hayo maneno aliyoripotiwa kuyasema, sikuona popote alipotoa ushauri wa kuondoa matatizo ya swala analolizungumzia; yeye anatoa amri tu basi.

Je amezungumza na wajenzi wa barabara kuu au hata wizara ya ujenzi ili tatizo hilo liondolewe kwa kuweka vituo maalumu vya mapumziko katika barabara hizo?

Kwa hiyo leo katibu mkuu wa wizara kafanya kazi kubwa. Amesikika na kuandikwa kwenye vyombo vya habari, hata kama hakuna lolote la maana alilolifanyia kazi.
 
Ni suala gumu hili. Haja huwa haijui uko wapi na utafika saa ngapi yenyewe inapotaka kutoka itoe hapo hapo.
Hawa ni wataalamu na wanawajibika kusema ili hatimaye mamlaka husika kwa kushirikia na sekta binafsi wachukue hatua. Kiukweli hali ni ngumu na ukiwa safarini kuna nyakati huwezi kuzuia haja ya kujisaidia eti mpaka ufike mahali kuna choo cha umma!
 
Back
Top Bottom